SoC04 Vijana wakalie viti

SoC04 Vijana wakalie viti

Tanzania Tuitakayo competition threads

conorard

New Member
Joined
May 27, 2024
Posts
3
Reaction score
4
Kijana mwenye adabu kamwe awezi kukaa kwenye kiti iwapo kuna mzee kasimama, iwe kwenye daladala au sehemu nyingine, na hii ni kulingana na hii ni kulingana na utamaduni wetu wa kitanzania, lakini utamaduni huu unapokosa mipaka na kusambaa kila nyanja ya maisha ndipo ugeuka tatizo kama ilivyo leo katika nchi yetu pendwa ya Tanania, ambapo kijana kupewa kitu kikubwa cha kufanya maamuzi bado ni ngumu katika masuala ya kijamii na hasa viti vya juu kisiasa na kiserikali ambapo kuna muda umri utumika kama kigezo kuliko uwezo , jambo hili halifai na hatuna budi kuhakikisha tunaliondoa ndani ya miaka 20 ijayo kwa kuwaandaa vijana kuanzia malezi maalum ya utotoni kuwa viongozi.

Pamoja na kwamba kundi hilu husifika kwa kuwa na nguvu na utimamu wa kimwili na kiakili lakini sifa hizi azijawabeba kupata fursa za kukalia viti hivyo, amapo ni ngumu kumkuta kijana kwenye bodi za maamuzi, au akiwa kwenye ngazi za juu za uongozi wa taasisi na serikali na hata katiba yetu haijampa fursa kijana kugombea nafasi ya uraisi wa nchi, japo tunaona wanaharakati, wanamapinduzi na wanamaendeleo siku zote ni vijana kama ilivyokuwa kwa wapigania uhuru wetu akiwepo hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyeanza harakati za kudai uhuru akiwa bado ni kijana, na hata sasa wale wachache waliopewa nafasi hakika walio wengi kati yao tunaona namna gani wanavyovitendea haki viti hivyo na sio kustarehe wakiwemo wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na wakurugenzi

Tumfahamu kijana
Kulingana na sera ya nchi ya vijana ya mwaka 2007 inamtambua kijan kama mtu aliye kati ya muaka 15 hadi 35 ambapo ni sawa na asilimia 31.95% ya watanzania wote na hii ni kulingana na takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Kundi hili huwa na sifa za kipekee nyingi zikiwa nyingi ni chanya lakini zipo hasi ambazo ulikumba kundi hili ikiwemo tamaa ya mafanikio ya haraka, miemko ya kihisia hasa mahusiano ya kimapenzi, ulevi wa pombe na madawa ya kulevya, japo sifa zao chanya haziwezi kufunikwa na izo hasi walizonazo baadhi yao ikiwemo ubunifu, uvumbuzi, nguvu, hamasa, ujuzi wa kidigirali, ujasiriamali, kujitolea utaratibu, uwajibikaji na ushirikiano ambazo zingelifanya kundi hili kutegemewa japo hali haiko hivyo kwa sasa.

Changamoto kadhaa bado zunawakabili vijana wengi wa kitanzania pamoja na uwepo wa sera ambayo utekelezaji wake umekuwa dhaifu mno, miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na elimu duni, ukosefu wa ajira, matatizo ya kiafya, umasikini, ukosefu wa mitaji, ushiriki mdogo katika masuala ya maamuzi, mazingira duni ya kufanyia kazi, mazingira magumu ya kiuchumi, na mabadiliko kasi ya kiteknolojia.

Kwanini vijana hawajakalia viti mpaka sasa?

Miongoni mwa sababu ni pamoja na:
  • Ukosefu wa uzoefu; kufanya maamuzi muhimu , jamii huamini kwa watu wenye uzoefu pekee.
  • Mawazo potofu; jamii bado wana imani kwamba vijana hawana utulivu, subira, na hawafikirii kwa kina.
  • Kukosekana mifano ya kutosha ya kuiga; Hatuna mifano mingi ya vijana waliopewa nafasi na kufanikiwa katika mazingira yaliyotuzunguka.
  • Mwendelezo wa utamaduni; jamii nyingi zina desturi za kihistoria ambapo zimeweka watu wazima katika nafasi za maamuzi kwa vizazi vingi.
  • Hofu ya mabadiliko; Vijana mara nyingi huleta mawazo mapya na mabadiliko ambayo yanaweza kuonekana kama tishio kwa hali iliyopo
  • Ushawishi wa kisiasa; mfumo wa kisiasa unaweza kuwa na upendeleo kwa watu wazima ambao tayari wako madarakani na wana mtandao wa uhusiano na ushawishi.

Haya yote upunguza uwezekano wa vijana kutoa mchango wao katika maendeleo ya jamii wanamoishi.

Watawezaje kuvikalia hivyo viti?
- Elimu ya kiuongozi;
Mitaala yetu ya elimu ilenge kufanya vijana kuwa watu wakuchukua maamuzi na hii inaweza kuanza kuwapa madaraka uko katika elimu ya msingi na sekondari, programu za mafunzo ya uongozi na semina ili kupata ujuzi na maarifa yanayoitajika kwa uongozi bora.
- Kuwajengea vijana uwezo; Kuwajengewa vijana uwezo katika nyanja mbalimbali za maisha ,ikiwa ni pamoja na ujasiriamali ,teknolojia na masuala ya kijamii,hii itawawezesha kuwa na ujasiri na kujitokeza zaidi katika nafasi za maamuzi.
- Kutoa fursa za uongozi; Serikali ,mashirika ,taasisi za kiserikali na sekta binafsi zinaweza kuanzisha programu za kutoa fursa za uongozi kwa vijana.
- Kukuza ushiriki wa kisiasa; Ushiriki wa vijana katika siasa bado ni mdogo,bila shaka vyama vya siasa vinaweza kuboresha uwakilishi wa vijana kwa kuhakikisha kuna nafasi maalum za vijana na kuhamasisha vijana kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika siasa.
- Kuondoa vikwazo na kuimarisha mfumo wa kisheria; Jamii na serikali zinapaswa kuondoa vikwazo vinavyowazuia vijana kushiriki katika maamuzi na hii yaweza kupitia sera na katiba inayoruhusu vijana kupata nafasi kubwa.
- Kuwatambua na kuwapongeza vijana; Kutambua na kuwapongeza vijana wanaofanya vizuri katika nafasi za uongozi na kuwapigia debe kama mifano ya kuigwa,kuwepo na tuzo nyingi na hii itawapa motisha vijana wengine kujitokeza na kushiriki.
- Mitandao na ushirikiano; Kuwapa vijana fursa za kujenga mitandao na kushirikiana na viongozi waliopo, wataalamu na mashirika ya kitaifa na kimataifa, mitandao hii inaweza kuwasaidia kupata msaada na mwongozo muhimu kwa ajili ya kujenga uwezo wao wa uongozi.

Matokeo yatakuwaje ?
Vijana baada ya kuwa nao ni miongoni mwa wale waliokaa katika viti vya kufanya maamuzi kutakuwa na chachu mpya katika maendeleo ya nyanja mbalimbali za kijamii, kwa kuongeza imani na ushiriki wa vijana katika maendeleo, kuimarisha demokrasia na utawala bora, uvumbuzi, ubunifu na uwakilishi bora, na hii itajenga jamii bora yenye amani na ustawi bora na hiyo ndiyo Tanzania tuitakayo miaka 10 ijayo.
 
Upvote 13
UVCCM munaitana sie wapagani kisiasa hatuitwi tusapotioane na kwangu mkuu

 
Back
Top Bottom