Vijana wakiume wapewe Elimu ya kuishi na wanawake waliowezeshwa (Empowered women)

Vijana wakiume wapewe Elimu ya kuishi na wanawake waliowezeshwa (Empowered women)

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Anaandika, Robert Heriel

Ipo haja ya kuundwa Kwa program maalumu ya kuwapa Elimu vijana wakiume ya namna ya kuishi na Wanawake waliowezeshwa(Empowered women).

Zamani tuliambiwa tuishi na Wanawake Kwa Akili Wakati Wanawake wenyewe hawakuwa Empowered, vipi sasa hivi wakiwa wamewezeshwa?

Mwanamke aliyewezeshwa ni Mwanamke ambaye amefikia nafasi ya kifursa sawasawa na Mwanaume kama vile;

I. Anaelimu ya kutosha kuanzia Diploma mpaka PhD.

2. Anazalisha na kumiliki Mali kama Nyumba, viwanja, mashamba, miradi na Mali zingine.

3. Anautambuzi na Uelewa WA wapi Dunia ilipotoka, ilipo na inapoelekea.

4. Anajua Haki zake, wajibu na Majukumu yake.

5. Anauwezo wa kuwania nafasi ya uongozi na kushiriki katika mambo ya Siasa iwe Kwa kuchagua au kuchaguliwa. Kutoa Maoni yake na kuwa na uwezo wa kuyatetea Kwa Hoja pasipo kujiona Duni pale anapopata upinzani.

6. Ambaye yupo kwaajili ya kuilea jamii yake kama Mama kwani ni jukumu la Mwanamke kuhakikisha malezi na Maadili ya jamii na taifa lake yanafuatwa.

Nafikiri ni Wakati wa wadau, serikali, asasi za kirai na mashirika kuanzisha Programu za kusaidia jamii hasa vijana wetu kuwapa Elimu ya namna ya kuishi na Wanawake waliowezeshwa kama nilivyoeleza hapo juu.

Lengo ni kuondoa matokeo hasi na kuijenga jamii yetu. Kwa sababu kumuwezesha Mwanamke ni Jambo moja zuri lakini kama haitatolewa Elimu Kwa Vijana ya namna ya kuishi na Wanawake waliowezeshwa basi italeta madhara maradufu Kwa Jami yetu hasa katika taasisi ya Ndoa.

Kwani kitakachotokea ni ongezeko kubwa la single Mother na watoto wengi hawatalelewa na Baba zao. Hii italeta madhara Hasi sio tuu Kwa kinababa Bali hata Wamama wenyewe.

Pia zianzishwe program za kuelimisha Wanawake waliokuwa empowered waelimishwe kuwa Bado wanaume na Vijana wengi wakiume wapo katika Fikra za zamani. Hivyo wawe na utambuzi huo na wafundishwe namna ya kuchangamana na wanaume Wenye mitizamo hiyo.

Zaidi, Taikon Ninashauri kuwa Elimu ya kuwawezesha Wanawake Ijikite katika kuileta jamii pamoja, na kuwafundisha Wanawake kuwa wanawezeshwa sio kwaajili ya ubinafsi wao Bali kwaajili ya kuunda familia Bora yaani Baba, Mama na watoto.

Women Empowerment inayoendeshwa na Wadau wengi ninaowasikiliza kwenye media mbalimbali, imejikita zaidi katika kuleta uadui baina ya Mwanamke na Mwanaume. Jambo ambalo linafanya wanawake watakaofanikiwa kuwezeshwa kuleta matokeo hasi zaidi ndani ya jamii kinyume na manufaa.

Nimeshuhudia Wanawake baadhi waliowezeshwa wakihamasisha wengine kuwa Maisha haijawezekana Bila mwanaume Jambo ambalo ni upotoshaji uliovuka mipaka.

Serikali, viongozi wa dini, na watu wenye nafasi zenye ushawishi Kwa namna moja ama nyingine ninyi ndio mnayeweza kufanya jamii zetu zikawa jamii Bora.

Kijana ambaye hajaelimishwa kuishi na Mwanamke aliyewezeshwa ni rahisi Sana kusababisha maafa, aidha Kwa kuachana bila ya sababu yenye Maana. Kisa tuu ni maelewano, ambapo kuna Wakati Mwanamke aliyewezeshwa ataonekana anakiburi au Jeuri.

Kijana lazima uelewa kuwa Mwanamke akitoka kazini anachoka kama wewe unavyochoka, kuna mambo ni madogo Sana ambayo mnaweza kuyamaliza ikiwa mtatumia Akili, busara na Hekima.

Mfano, kama ishu ni kupika, mnaweza ajiri HM(Housemaid) au Home personal Chef wa kuja na kuondoka kama hamtaki Jau nyumbani. Kuhusu kufua nguo mnaweza nunua Mashine za kufulia wala sio bei ghali, zipo nyingi Chini ya milioni moja.

Ni lazima wanafamilia kila mmoja amfikirie mwenzake kama anavyojirikiria yeye mwenyewe. Hiyo ndio namna ya kuunda familia Bora.

Taikon bado Ninashauri ingawaje hata Mimi ninachochea Women Empowerment Kwa namna moja ama nyingine lakini Jamii kamwe isiache kufuata mfumo Dume, lakini katika huo mfumo dume zile dhana potofu zisizo na mantiki lazima ziondolewe ambazo zinalenga kunyanyasa, kuumiza, kunyanyapaa, kudhalilisha na kufanya ukatili.

Vijana wakiume waelimishwe kuwa mfumo dume ni Haki, ukweli, Uhuru, upendo na kuiifanya jamii na dunia kuishi Kwa Amani.

Nawatakia Sabatonjema.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es salaam.
 
1. Elimu mnaionea Kwa kuijazia majukumu kila kukicha (Ujasiriamali, Elimu ya uzazi & kujamiiana=sexual and reproductive health education, ICT).

2. Ungeweka hata namba yako ya simu iwe rahisi kupata UTEUZI Wizara ya Maendeleo ya Jinsia na Ustawi wa Jamii kule panakufaa jomba.
 
1. Elimu mnaionea Kwa kuijazia majukumu kila kukicha (Ujasiriamali, Elimu ya uzazi & kujamiiana=sexual and reproductive health education, ICT).

2. Ungeweka hata namba yako ya simu iwe rahisi kupata UTEUZI Wizara ya Maendeleo ya Jinsia na Ustawi wa Jamii kule panakufaa jomba.

😀😀😀
Mkuu Elimu ni Elimu tuu hata iwe ya namna ya kumfungulia Jogoo Asubuhi ili atoke kwenda kuparamia mitetea ya Asubuhi.

Wengi wanaowakandamiza Wanawake wanahitaji Elimu zaidi, hata hivyo Wanawake nao waliokuwa- empowered nao wanahitaji Elimu zaidi ya kuishi kwenye jamii yenye wanaume wanaofikiri kutumia nguvu kubwa pasipo Akili ndio uanaume.

Kuhusu kitengo nimecheka Sana😀😀
 
To be honest, mwanamke akiwa na hivyo vitu tajwa hapo juu, alichokosa Ni ndevu tu ili awe mwanaume kamili, ndo maana wataliban wanawake hata hawakwenda shule, ili wawe wake Bora ndani ya nyumba. Kwa Hali hii lazima liibuke kundi la KATAA NDOA.
 
To be honest, mwanamke akiwa na hivyo vitu tajwa hapo juu, alichokosa Ni ndevu tu ili awe mwanaume kamili, ndo maana wataliban wanawake hata hawakwenda shule, ili wawe wake Bora ndani ya nyumba. Kwa Hali hii lazima liibuke kundi la KATAA NDOA.

Mwanamke asipoenda shule alafu akawa mkeo lazima umfanyie ukatili iwe kwa kupenda au kutokupenda.

Mwanamke asipofanya kazi moja kwa moja anavunja amri ya Mungu isemayo fanya kazi siku sita. Hii itamfanya anyanyasike na asiwe huru
 
Back
Top Bottom