Vijana waleta fuji kutaka aliyetengwa na kanisa azikwe kwa taratibu rasmi za kanisa

Vijana waleta fuji kutaka aliyetengwa na kanisa azikwe kwa taratibu rasmi za kanisa

Ujumbe uko kwenye video hapa chini kwa vijana wa Arusha

View attachment 2365876
Big up kwa vijana.. makanisa mengi yana unafki mtu akiwa tajiri hatengwi wala nini

Yani wanajuaje huko ulipoenda wao wanahaki gani ya kukutenga hatakama ulikuwa jambazi kuu??..

Mwambie huyo mchungaji wa mchongo akasome Yohana 8:7.. anafeliiiihh ndo maana tunawaambia kila siku Bangi ihalalishwe hamsikii

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Hawa viongozi wa kikristu wa KILUTHERI na KIKATOLIKI kanda ya kaskazini wamekuwa wababe na kujitengenezea taratibu ajabu sana. Yaani wanafukia msalaba? Mamlaka hiyo kawapa nani? Kama mmemtenga mtu waache ndugu zake na marafiki wake wamzike kwa heshima. Kuna baadhi ya matajiri na watu maarufu mbaona hawafanyi hivyo?
 
Kwanza Kwa Sasa Wanaojiita wachungaji na manabii wajitafakari.
Zipo dhambi nyingi sana.

Kwa Nini asilimia zaidi ya 70 ya waumini ni wazinzi na walevi Tena Wazinzi waliopo kwenye kiapo Cha ndoa lakini hawatengwi.
Wengine wamezaa mpaka na wake za watu lakini wanaojifanya kuwa Mungu hawaoni Kwa sababu TU wachungaji na Wazee wa kanisa hawajawatangaza .
Hata hao viongozi wapo wengi ni wazinzi lakini wanajipa mamlaka ya kuhukumu wengine.

Hivi kipi kibaya kati ya kuzini wanandoa au uasherati Kwa kijana ambaye hajaoa Tena hajafanya uasherati na mume wa mtu au mke wa mtu ni Vijana Kwa Vijana na wakati Mwingine Wana malengo ya kuoana .

Wachungaji na Mitume wameacha kukemea uzinzi Kwa wanandoa mana Wazinzi hao wengi ni wamama na wababa wenye Fedha.

Acheni kutoa kibanzi kwenye jicho la wengine.
Wakati macho yenu Yana maboriti.

Mtu akifa Kuna mitani ya kupina matendo yake . Kila mtu atauchukua mzigo wake mwanyewe.
Hakuna mzigo unaochukuliwa na Kanisa au kikundi Cha watu.
Yesu pekee ndiye anayejua watu wake na sio wachungaji .

Hongera vijana wa Arusha.
Siku kanisa Hilo Hilo mkoa Fulani waligoma kumzika mtoto wa siku Moja kisa wazazi wake walikua hawajafunga ndoa .
Nilikwazika sana nikaingilia na kumzika Kikristo bila kujali taratibu zao. Nikaongoza Ibada yote mwanzo Mwisho. Mtu amefiwa na mtoto wake halafu wakristo wanalazimishwa na Taratibu za Wazungu ili wasimfariji ndugu yao.
 
Dini siku hizi ni biashara

Graduates changamkieni fursa tengenezeni makanisa ya mchongo
 
Majamaa wametisha sana. Neema hajawahi kuwa na baya.
 
Back
Top Bottom