Uchaguzi 2020 Vijana wanaosadikiwa kuwa ni wa CCM kurusha mawe kwenye msafara wa Lissu ni njama ya kuwafanya CHADEMA wajibu mashambulizi ili waonekane wanavurugu?

Uchaguzi 2020 Vijana wanaosadikiwa kuwa ni wa CCM kurusha mawe kwenye msafara wa Lissu ni njama ya kuwafanya CHADEMA wajibu mashambulizi ili waonekane wanavurugu?

Godfrey-K

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2016
Posts
1,925
Reaction score
3,672
Ililipotiwa huko Kagera kuwa msafara wa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu kupigwa mawe pale alipokuwa akipita mbele ya Jengo la CCM akielekea uwanjani kwenye mkutano , mwanzo nilidhani ni propaganda tu za wana CHADEMA

Jana akiwa Geita Mjini hali hiyo mbaya ya kutupa mawe imejitokeza tena akiwa barabarani karibu na ofisi ya CCM akielekea kwenye mkutano wake .

Je, iwapo wana CHADEMA wangeamua kujibu mashambulizi ya kuwapiga vijana wa CCM kusingetokea madhara? Kwani CHADEMA walikuwa wengi kuliko hao vijana wa CCM.

Je, huu ni mpango wa kutaka kuharibu kampeni za Tundu Lissu ili ionekane kuwa CHADEMA ni watu wa fujo na vurugu?

Tunaomba viongozi wa CCM mkemee tabia hii ili kuepuka maafa.

Naomba kuwasilisha.
 
Ililipotiwa huko kagera kuwa msafara wa mgombea uraisi kwa tiketi ya Chadema Tundu Lissu kupigwa mawe pale alipokuwa akipita mbele ya Jengo la CCM akielekea uwanjani kwenye mkutano , mwanzo nilidhani ni propaganda tu za wana chadema...
Hata Mwenyekiti wao Taifa ni mtunza visasi, mvunja katiba, mbabe, hana busara na hekima za uongozi, nk. Hivyo, wafanyavyo vijana ndivyo alivyo baba yao. Ni chama kinakosa uhalali wa kuongoza. Kinakufa.
 
Habari kama hii bila picha wala video ni uchonganishi tu nyie chadomo!
 
Ililipotiwa huko Kagera kuwa msafara wa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu kupigwa mawe pale alipokuwa akipita mbele ya Jengo la CCM akielekea uwanjani kwenye mkutano , mwanzo nilidhani ni propaganda tu za wana CHADEMA...
Kwa kadiri siku za kampeni za uchaguzi zinavyozidi kwenda ndipo uhalisia wa CCM kukosa uvumilivu na ukomavu wa kisiasa unavyozidi kuonekana. Na kitu cha ajabu si tume ya uchaguzi wala vyombo vya dola vinaonyesha kukerwa na matendo haya ya kifedhuli ya UVCCM.

Makada wa CCM waliamini kanda ya ziwa ni ngome yao kubwa ya kisiasa. Hivyo waliamini kabisa Tundu Lissu angalipata watu kiduchu ktk mikutano yake ya kampeni.

Ukweli juu ya hili ulifichuka baada ya mgombea wa CCM kuropoka kuwa picha za mapokezi na mahudhurio ya mikutano ya Tundu Lissu inachakatwa. Sasa wamebaini ya kwamba Lissu ni namba nyingine na wala hakuna wa kumzuia.

Kilichobakia sasa ni kuonyesha wivu ukifuatiwa na matendo yao ya kishenzi. ya kutaka kuwalazimisha watu wakose ustahimilivu na kulipiza kisasi ili wapate kuhusisha CDM na matendo ya vurugu.

That're last kicks of the dying horse. It's more than too late to stop Tundu anymore, since Tanzanians have already spoken. Hakuna tena namna, ni lazima neno hili la kinabii likapate kufikia utimilifu wake wote.

MENE, MENE, TEKELI & PERESI
 
Wanajidaganya,wawe na ngome wapi wakati kila mtanzania anaguswa na uogozi mbovu wa huyu Rais,Lissu anachopaswa kukifanya kwasasa ni kufukua maovu yote ya jiwe,ili tarehe 28/10 huyu mvunja katiba awe mtupu kabsa
 
Ililipotiwa huko Kagera kuwa msafara wa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu kupigwa mawe pale alipokuwa akipita mbele ya Jengo la CCM akielekea uwanjani kwenye mkutano , mwanzo nilidhani ni propaganda tu za wana CHADEMA..
KILA MAIGIZO NA PROPAGANDA ZENU ZINABUMA HARAKA SAANA. ILA KUMBUKENI OCTOBER NDO MTAJUA WATANZANIA HAWAPENDI KUUZA TAIFA LAO KWA MABEBERU.
 
Wao ni Mabeberu jee mbuzi jike unamjua??
Tutawagalagaza na kiki zenu za kutengenezewa na hao mabeberu, halafu mnajifanya eti mnamiujiza iliwatanzania tushobokeee MIUJIZA ya mtu anayetaka kuuza taifa letu. Tutawagalagaza hapo October, hadi mtueleze igizo lile mlilitengenezewaa na naniii
 
Sawa, hata mbowe ilisemekana alivamiwa na vijana wa CCM.
 
Ililipotiwa huko Kagera kuwa msafara wa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu kupigwa mawe pale alipokuwa akipita mbele ya Jengo la CCM akielekea uwanjani kwenye mkutano , mwanzo nilidhani ni propaganda tu za wana CHADEMA...
Kama itafika kipindi hao vijana wa uvccm wameendelea na huo upumbavu wao basi na sisi hatuna budi kujibu mapigo mara kumi zaidi
 
Back
Top Bottom