Vijana wangu msiuache mfumo dume

Cha ajabu wanawake wao wakati wanadai 50/50 tena kwa vitendo kwa kuchukua majuku ya mwanaume bado wao wamesimama kwenye nafasi yao ya kuzaa na kupata heshima zao za kuleta viumbe duniani lakini wale wa jukumu la kula kwa jasho wapo wanalalamika kwanini waoe wanawake wasio na kazi?Ili wawasaidie kupungua kuvuja jasho? Na hata wakisikia shule za wanawake zinajengwa nyingi wao hawapambani zijengwe kwa usawa Ili watoto wa kiume wapate elimu nzuri waje kutumikia kula kwa jasho Ili wabaki kuwa juu na kubaki kwenye wajibu wao wa lazima wa kula kwa jasho, imagine mtu anaona mtu wa night shift na yeye anabaki nyumbani amelala huku akitafutiwa mkate? Zamani mwanamke akiwa na kazi za kujenga taifa waliachwa wawe watakatifu wa kutumikia jamii na ndipo nguvu ya mwaume ilionekana hapo labda kidogo walimu kwa vile wanarudi mapema kuchukua jukumu la nyumba kidogo walitupiwa jicho la kuwa mke, hivyo 50/50 kwasasa sidhani kama itakwepeka mume atalala ndani na mke atakaa hata mwezi mzima semina Ili alete pesa ndani za kuinua kipato kilichokosekana kwa mla kwa jasho.
 
Wapuuzi hawa waasisi wa huu mpango wa haki sawa
Mbona mpango umejileta wenyewe baada ya kuona Kuna upande umebeba laana mbili zote au unatumikia laana zote mbili? Ndo wakaona wale walioshindwa kutumikia laana yao basi washushwe au walinganishwe Kwanza na baada ya kuwa sawa baadaye watazidiwa Sasa hapo itakuja aliyejuu atamutawala aliyechini yake ndo hapo Sasa mume mmoja atazunguka nyumba hata ishirini au hata mia kama mpita njia bila makazi ya kudumu na huku wanawake wakibaki na usukani wa hizo nyumba ndo maana waliofunuliwa mapema hawezi kukubali kuingiliwa kwenye majukumu yake na kuwa chini hasa uchumi unaofanya mtu ale kwa jasho.
 
Ni hatua nzuri kwa kweli!

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Tushaingia mfumo jike, kijana analelewa na jimama kazi zake chache kumliwaza jimama na kulinda mipaka ya nyumba basi, kijana anajiongeza anashinda anapiga mitungi na mihadarati.
Huyo dawa yake fainali uzeeni!! Kama mke ndo atakuwa mtoa ulithi kwa kizazi chake Sasa sijui atajiweka wapi uzeeni.
 
Kabisaaaa

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Kwani busitanini Mungu hakuwa amewapa maagizo na maelekezo lakini Adam akazidiwa? Ndo hivyo Sasa inavyokuwa yaani imejirudia.
 

Isa 4:1​

Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu
Kwa hiyo hapo mwenye nguvu atakuwa mwanamke, wanawake Saba wenye uchumi wao wakila chakula Chao au wakiwa na uchumi wao maana yake wakiwa wamiliki wa mazingira yao wakuite Kila mmoja kwa wakati wake mwanaume uwe mpita njia kwenye nyumba zao kama mwanamke Malaya anavyokuwa mpita njia kwa kutumika kwenda kutimiza haja za mwanaume kweli hapo heshima ya mwanaume itabaki wapi? Kama maumbile ya mwanamke hayakumpa nguvu ya kutawala zaidi ya kutawaliwa ndivyo itakavyokuwa kwa mwaume yeyote atakaye tumia maumbile yake pekee kwenye mahusiano, Nguvu ya uchumi ndo Kila kitu kwa mwanaume na ndo maana akapewa kazi ya kutumia jasho lake hujiulizi kwanini hakuambiwa akale kwa kutumia maungo yake ya uzazi? Kwa vile mtu mwenye uchumi ananguvu kubwa kwenye kutawala na anayetawaliwa huwa uchumi wake au vigezo vingine lazima viwe juu kama elimu na ndo maana zamani wanawake wenye vipato na elimu kubwa walitumika kama watu wa kusaidiana na wanaume kujenga Nchi na siyo kuwa chini ya mwanaume kwa kuolewa.
 
Mbona Sasa yameshakuwa maji yaliyomwagikia ardhini? Kuna wanawake Wana nguvu za kuua dubu, Simba, nyoka na hata mapambano makubwa kuliko wanaume wasiofanya mazoezi, Kuna wanawake wenye elimu kubwa kuliko wanaume wasiofikia hizo elimu, Kuna wanawake wenye uchumi mkubwa kuliko wanaume wenye uchumi mdogo, Sasa mwaume alipewa kutawala na Ili utawale unatakiwa kuwa juu Sasa mume la Saba na mke ni PHD Sasa hapo nani atamutawala mwenzake kwenye maarifa hapo? Japo jinsia hazibadiliki lakini tayari huo usawa umekuja wenyewe baada ya wanawake kuwazidi ujanja wanaume kama pale busitanini tunavyomulaumu Adam kwanini alikubali kuzidiwa maarifa mpaka kula tunda? Ndo hivyo kizazi cha baadadaye kitavyoshangaa kwanini wanaume walikubali kuzidiwa maarifa kiasi cha kufanya aliyetakiwa kuwa chini yupo wewe unachukua aliyejuu yako bado ukitegemea utajiondoa kwenye usawa hapo? Labda fimbo zirudi kwa wanaume wote walioshindwa kutumia akili zao kiasi cha kuuza utawala wao.
 
Elimu na dini vimewafanya wanaume kuwa waungwana yaani diplomatic tofauti na wazee wetu.
Ila kiasili wanawake wengi upenda wanaume madikteta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…