Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Wakati suala la ajira, kuboresha elimu, matumizi ya teknolojia vikitawala, vijana wametaka dira ya Taifa 2050 ipunguze umri wa watu kustaafu kwa lazima hadi kufikia miaka 55 kutoka 60.
Hayo yamesemwa leo Desemba 18, 2024 wakati vijana wakitoa maoni yao kwenye rasimu ya Dira ya Taifa 2050 iliyozinduliwa Desemba 11, 2024 na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.
Akizungumza katika kongamano hilo, mratibu wa makongamano ya ukusanyaji maoni Sera ya Vijana, Omary Pumzi amesema katika mikutano mingi iliyofanyika, vijana wametaka kuona umri huo unapungua ili kuacha fursa kwao.
“Sasa hivi umri wa kustaafu ni miaka 55 kwa hiari na 60 kwa lazima, vijana wanataka umri huo ushuke hadi miaka 55 kwa lazima na 50 kwa hiari, hii miaka michache inayobakia vijana waitumie kufanya kazi na kujipatia kipato,” amesema.