Vijana wengi wa Kitanzania ni wavivu kupindukia, wanataka mteremko


Picha kwanza mkuu!!
kusafisha shamba la heka 3 sio mchezo!! unastahili pongezi budah
 
Ndiyo sababu wanatafuta kazi ya umario, vijana wa kiume kuolewa na mashuga mami.
 
Kichwa cha habari na habari ni mambo mawili tofauti
Unapopenda kuwa mkulima sio kila mtu atakuwa mkulima, sema ungesema unatueleza umefikia wapi juu ya mkakati wako wakulima na kuwekeza.
MKuu Usifikirie kukomaa sana ndio kufanikiwa
Maisha ni haya haya tu, Ukishindwa kula bata leo usitegemee kesho
Nina Usemi Mmoja tumia hela upate akili ya kutafuta hela nyingine,
Sinaga Upuuzi wa kuweka akiba hata siku moja, Wala siamini katika kuweka akiba,
but always naamini katika investment ila usiwe na akili za kitoto namna hivyo
Nina mashaka na namna unavyoendesha familia yako
 

Najua sana hayo unayosema na nina uzoefu halisi ambao nimeuishi na kuushuhudia. Pia nimetumia muda mwingi sana kutafuta maarifa mengi sana kuhusu kilimo na ufugaji, pia nimetembelea mashamba darasa idadi ya kutosha kabisa kama ni lecture nimepata za kutosha, jumlishia na background yangu mimi nimetokea familia ya wakulima japo kama unavyojua wazazi wetu walikuwa wanalima kienyeji sana. Ni muda wa mimi kufanya kitu tofauti. Sina papara ni muhimu kuwa na malengo, na ufurahi unapoona malengo yanatimia. Kuhusu changamoto ya soko na utunzaji shambani, falsafa yangu ni kuwa Mungu alituweka duniani tuitawale dunia... hata kilimo ni muhimu kutumia akili badala ya nguvu nyingi. Wengi wanalima kwa sababu kahamasishwa na flani au kaona mwenzake anafanya hivyo. Badala yake unatakiwa uwe na target yako wewe kama wewe, tumia akili. Mfano, mwaka jana sikulima mahindi hata punje baada ya kutafakari gharama na usumbufu ambao mkulima anapata, huku akitarajia mvua ndo avune. Sitaki kilimo cha kubahatisha nikasema nitanunua mahindi. Wengine wajinga wakanishangaa kuona nasafisha tu shamba natoa visiki alafu msimu wa mahindi sijapanda. Baadaye walikuja kuona nilitumia busara baada ya wao kujikuta wanauza mahindi gunia Tsh. 25000. Ukicheza katara vizuri utaokoka, ukizubaa utaliwa, lakini pia lazima ukubali wakati mwingine mahesabu yanaweza kugoma, lakini hayawezi kugoma kila siku. Go wisely
 

Siyo kila post lazima uchangie. ishi upendavyo acha wengine tuishi kivingine, ndo raha ya dunia
 
Safi sana ndugu, umejieleza vizuri na kwa kupitia maelezo hayo nimefahamu yakuwa unafahamu na umetafiti vya kutosha kuhusu kilimo. Nakutakia kilimo chema.
 
Na kweli ni mvivu, uvivu namba moja ni kutaka kubanana kwenye ekari 3, hivi ekari 3 ni eneo kweli la kubanana watu wawili wanaotaka kufanya serious investment? Wakati mashamba yamejaa kibao kila pahala.
 

sio kila mtu anaweza KUJIONGEZA
neno HAPANA watu wengi wanaona ugumu sana kulitumia
unapoteza muda kufikiria ambayo tayari umeshafikiria na ukaona HAIFAI hivyo ukijilazimisha kukubali kwa sababu ya urafiki ulionao ni mwanzo mzuri wa KUFELI
Sema HAPANA maana wewe una mipango tofauti ndio maana wakati wewe unaanza yeye hakutaka

sema HAPANA na acha kupeleka mbele maamuzi ambayo unaweza kuyafanya sasa unakaa unafikiria umjibuje mtu wakati jibu ni HAPANA na huna jibu jingine stong kuliko hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…