Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,773
- 1,174
Timu ya vijana wa Kitanzania kutoka jamii ya Watanzania wa Diaspora waliozaliwa nchini Somalia kwa wazazi wa asili ya Kitanzania na Kisomali, imeibuka mabingwa wa Ligi ya Vijana mjini Mogadishu.
Ushindi huo umeonesha uwezo mkubwa wa vijana hao ambao licha ya wengi wao kutowahi kufika Tanzania, wameendelea kubeba na kuendeleza vipaji hali inayosababisha Wasomali wengi kuamini kuwa Tanzania ina Vipaji maalum katika Urithi wake wa kuchanganya damu.
Wakiwa na umahiri mkubwa katika mbinu na kazi za miguu (footwork), vijana hao wamejipatia sifa kubwa kutoka kwa jamii ya Wasomali ambao huwataja kama “Machotara wenye vipaji maalum”.
Aidha, Serikali ya Tanzania kupitia Ubalozi wake nchini Kenya, kwa kushirikiana na Ubalozi wa Somalia nchini Tanzania na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, imeandaa mwaliko kwa timu hiyo kutembelea Tanzania.