nadhani muandaaji wa hii kitu alibase kwenye mafanikio binafsi ya wahusika zaidi sio mchango kwa jamii..ndio unamuona hata mtu kama mnyika hapo,kwani maechangia nini kwa jamii?[/QUOTE]
Nahisi humjui Mnyika vizuri au labda unamaanisha Mnyika mwingine na si huyu John John Mnyika mbunge wa jimbo la ubungo kwa tiketi ya CHADEMA! Mnyika(mb) ninaemjua mimi amechangia kwa kiasi kikubwa kwa jamii licha ya kuwa na muda mfupi bungeni, amekuwa ni mtoa hoja mzuri, mkosoaji/mrekebishaji mzuri wa miswada ya serikali na mara nyingi hoja zake zimekubaliwa na kama umekuwa ni mfuatiliaji mzuri wa bunge kumbuka wakati wa mjadala wa sera ya manunuzi ya umma jinsi alivyosimama kidete katika kujenga hoja zilizopelekea kubadilishwa kwa vipengere kadhaa vya muswada huo kwa kubana mianya ya rushwa au kutoa adhabu kali, je huo si mchango kwa jamii? au kwa fikra zako unadhani mchango kwa jamii mpaka utoe fedha au bidhaa fulani!? kama unadhani hivyo pole sana na sina jinsi ya kukusaidia.
,