SoC04 Vijana Wetu Wasomi

SoC04 Vijana Wetu Wasomi

Tanzania Tuitakayo competition threads

black abdu

Senior Member
Joined
Dec 2, 2022
Posts
156
Reaction score
212
Mazungumzo na mwanangu:
Jioni moja kwenye mazungumzo na mwanangu nikamtajia wazo langu kuwa, ingekuwa vema angeingia kwenye siasa, kwa vile nafikiri hapo baadae angeweza kupata nafasi ya uongozi na kufanya mema kwa nchi yetu. Jibu lake lilikuwa fupi na la kisomi kuwa “Siasa is not my thing”. Tukafungua mjadala mrefu kiasi uliomalizika kwa makubaliano kuwa angefanya utafiti na kujifunza zaidi namna siasa zinavyoenda.

Nukta tulizojadili hadi kufikia muafaka ni kuwa:

Halihalisi; kumekuwa na matukio mengi yanayohusishwa na siasa na kusababisha woga kwa vijana wengi kuingia au kujihusisha na siasa, hasa kwa vijana wenye uwezo na fikra ya kufanya mema kwa taifa lao. Hawahofia kuingia kwenye siasa kwa sababu wanatambua kuwa kwenda kinyume na mfumo ni kujifungulia mlango wa matatizo. Ndipo vijana wanaamua kujiweka mbali na mambo ya siasa, na kutumia usemi wa “fanya yako”, ikisisitiza kujihusisha zaidi na shughuli binafsi na kuachana na kujihusisha na siasa kama njia ya kuwa salama.

Tafsiri ya hii ni kuwa vijana wamekubali kushindwa na hivyo kutoa ruhusa kwa mfumo kufanya unavyotaka bila kupingwa hata ikiwa ni mikakati ambayo itakuwa mzigo kwa wananchi, ili tu kufanikisha malengo yake.

Tunachokiona ni kuwa kunakuwa na malalamiko mengi ya kutokuridhishwa na mambo mengi lakini yote yanabaki kuwa manung’uniko ya kimya kimya, kila mtu anaogopa kusimama na kupaza sauti. Ndio, kuna wale wapinzani rasmi wa mfumo wanaotumia nafasi zao kueleza maoungufu ya mfumo lakini hata wao wanakosa kuungwa mkono na wananchi wengi, hasa vijana, ambao hukaa kimya kutazama nini kitakachotokea.

Kifupi ni kusema kuwa vijana walio wengi hawaridhishwi na mengi ya mfumo, wanatamani mabadiliko lakini hofu yao inawanyima nguvu ya kusemea mabadiliko hayo, na hivyo kusubiri wengine ndio wawapiganie na kuwasemea. Kitu ambacho kiuhalisia hakiwezekani au kitachukua dahari kuona mabadiliko.

Mtindo wa mbuni kuficha kichwa mchangani akiamini ndio amejinusuru kutoka kwa adui, ndivyo vijana wanavyojidanganya kuwa watakuwa wamejinusuru na mfumo kama wataangalia mambo yao, yaani kama mtu ana chanzo cha kumpatia mkate wake wa siku na paa la kujisitiri basi aachane na hayo mengine ili asiiletee familia yake matatizo au akaacha yatima wanaoteseka. Ndio tunaona vijana wengi wengi sasa wako bizi na shughuli zao binafsi, mbali na siasa wakiamini wamenusurika.

Utajua tunajidanganya pale unapoona hao wenye vipato wakilalamika kuhusu kupanda bei ya mafuta au ongezeko la nauli, kulalamikia kukosekana kwa huduma za umeme na maji kwa vipindi virefu, tozo na makusanyo mbalimbali yanayopewa majina tofauti na kadhalika, ndipo unaelewa kuwa si kuwa tunaridhia yanayoendelea ila tu tunavumilia kwa sababu ya hofu yetu kwa mfumo. Labda kuvumilia huku ni jambo jema kwa vile tunaepusha machafuko, swali ni, je, tunapaswa kuvumilia hadi lini?

Tunarudi kwenye swali la msingi; kwa nini kupaza sauti kudai yaliyo ya msingi kunaitwa kuleta taharuki? Ni nani anayesababisha hiyo taharuki kama maoni ya watu yatasikilizwa na kufanyiwa kazi? Tunahitaji kuliweka hilo sawa vichwani mwetu ili tusijibebeshe hatia isiyotuhusu.

Tuna vijana wengi wasomi wenye uwezo wa kuleta mabadiliko kwenye mfumo na kuongeza fikra za kisasa zitakazoweza kuboresha hali ya maisha ya wananchi nakunyanyua uchumi wa nchi, pekee kinachohitajika ni uthubutu wa vijana kupiga moyo konde na kuingia kwenye mfumo kwa wingi zaidi, ili kuleta mabadliko tunayoyataka. Hakuna njia tofauti.

Hatari iliyopo ni kuwa endapo vijana tutaendele kukaa mbali na mfumo tunatoa nafasi ya mfumo kuendelea na mtindo wake kwa kuwarithisha falsafa zake wanaoandaliwa kushika usukani baadae. Sasa kwa nini tujinyime haki tunayopewa na katiba yetu? Hata sisi tuna haki ya kukaa mjengoni, tukatenegeneza sera na mikakati kwa fikra zetu njema halafu tukarudi kupongezana kwa kugongeana meza.

Mtindo wa virusi; tujifunze kwa jinsi virusi vya UKIMWI vinavyofanya kazi, vinapoingia mwilini havisababishi homa za ghafla kama vijidudu vingine, bali vyenyewe huingia taratibu hadi kujiweka na chembe nyeupe zinazotengeneza kinga ya mwili, na kufanya seli hizo kuzalisha virusi badala ya kutoa kinga za mwili. Mtu akitahamaki virusi vishasambaa mwilini. Ndio vijana tunapaswa kimya kimya kuingia kwenye mfumo na kuingiza fikra zetu zilizo njema na manufaa, fikra hizi zikifanikiwa na kuleta matunda, baadae tutajikuta tumefanikiwa kubadili mfumo mzima.

Tutaweza kuweka mikakati imara zaidi ya uzalishaji wa mapato isiyo kandamizi, tutengeneze fursa zaidi kwa vijana kujinasua kutoka shimo la umasikini, kuwapa wazee wetu ahueni ya maisha na matibabu na kuwajengenea wadogo zetu barabara ya mafanikio ili wawe warithi wema wa viti mjengoni na maofisini.

Tujifunze kuwa panapokuwa na jambo lisilopendeza, shujaa hutumia mkono wake kubadili hali iliyopo, hodari hutumia mdomo wake kusema fikra zake, muoga hubaki akinung’unika bila kufanya chochote na dhaifu hukataza hata akili yake isifikirie nini kinapaswa kufanyika, na hewala, akakubaliana na hali iliyopo.

Kwa sasa wengi wetu ni dhaifu na waoga, tunaona yanayoendelea ila tunabaki kunung’unika vijiweni na kwenye comments za mitandao. Tunahitajika kupanda ngazi na kuwa hodari kujifunza kusema tunayoona si sawa, sauti zikiungana hutengeneza ngurumo inayoweza kuleta mtikisiko.

Wakati wa kuanza ni sasa tukielekea kwenye uchaguzi, tuchague wagombea kulingana na sera na sifa zao, tusikubali kufanywa daraja la wao kupitia. Wanapokuja kututumia kwa bakshishi na zawadi ni kwa sababu wanatambua nguvu tuliyonayo kwenye kufanikisha jambo, basi tuamue awamu hii iwe tofauti na awamu zingine, tunzie hapo kama mkakati wa muda mfupi. Hiyo ni "akili kichwani".

Kikubwa ni kuacha kudharauliana na kusimama pamoja tukitambua sote tupo ndani ya merikebu moja, Ili tufike safari yetu salama ni lazima tumwambie nahodha anapokosea, ajue alipokosea, na kishwa tumpe njia sahihi ya kufuata, na halafu sisi wenyewe tusome vema ramani na tujiweke sawa kupambana na mawimbi na tufani ili kushika vema usukani ikifika zamu yetu ya kuongoza chombo.

Ninachomaanisha ni kuwa hakuna jambo bora mtalifanya kama kusimam imara na kushika uongozi wan chi yetu na hili
 
Upvote 4
Back
Top Bottom