Vijana zaidi ya 500 wamekutwa wamehifadhiwa sehemu mbalimbali Mkoa wa Kilimanjaro wakifanya mafunzo yasiyojulikana

Nchi hii si ya majimbo. Kila mtu ana haki ya kuishi na kutafuta kipato mahali popote. Unapowaambia hao vijana waondoke Kilimanjaro mara moja, si kinyume cha katiba kweli? Je, hakuna vijana wakazi wa Kilimanjaro wasio na kazi?

Na kwa nini serikali inajiondolea lawama kwa sababu wao ndiyo waliwapa hao watu vibali na leseni za kufanya kazi zao, leo wanajifanya kama hawawajui vile.
 
Huyu Mkuu wa Mkoa ndiyo aliyekataa kutoa fedha za matibabu ya Lissu akiwa katibu wa Bunge ???

No wonder anataka vijana waondoke mkoani kwake ndani ya siku saba sasa sijui watapaa kwa ungo.!!!!!!.

[emoji706][emoji706][emoji706]
 
Bado wanapika ile kesi ya Freeman ili ionekane vijana hao wanapatiwa mafunzo mkoani kwa akina Freeman

Unatumia kiungo gani kufikiri mkuu. Hivi Mbowe alikuwa na sifa yeyote ya kuwa Rais wa Tz. Unampa ukubwa ambao hana. Maisha yanaendelea huko mtaani. Mbowe is nothing.
 
Hii taarifa ilivyotolewa ni mkakati wa 'kuathiri akili za watu wengi' ili waanze kufikiria kuwa hao watu walikuwa wanapatiwa mafunzo ya uhalifu, tena ugaidi kabisa. Kumbuka hao vijana wamekamatwa Moshi, na Mbowe ambaye leo alikuwa mahakamani anatokea Moshi, na akina Kingai 'walikamata magaidi' Moshi. Tatizo la hawa vijana ni tatizo la serikali ambayo inajivua na kujiweka kando. Inashindwa kutengeneza miundombinu rafiki kwa vijana kujiajiri, hapo TRA sasa hivi kupata Taxi Clearance kwa mtu anayetaka kujiajri ni balaa, mara anaambiwa ajaze vitu gani sijui kwa e-filling wanakulamba mihela kibao...hii nchi ni hovyo kabisa!
 
Huyu Mkuu wa mkoa hana utu kabisa na hafai kuongoza jamii yeyote hao ni watoto wa Wawatanzania sio wakimbizi alitakiwa kutotumia Lugha ya waondoke siku saba su tano...hawa viongozi sijui wanatolewa wapi
 
Huyu Mkuu wa mkoa hana utu kabisa na hafai kuongoza jamii yeyote hao ni watoto wa Wawatanzania sio wakimbizi alitakiwa kutotumia Lugha ya waondoke siku saba su tano...hawa viongozi sijui wanatolewa wapi
Kama aliweza kunyima fedha mgonjwa aliyepigwa marisasi unategemea utu gani kutoka kwake ?
 
...Hio Laki Tisa angeweza hata kuhangaika nayo mwenyewe na mkono ukaenda kinywani!
Hivi Matapeli hao walipokuwa wanatoa matangazo ya Ajira kuwarubuni Vijana, Serikali haikushituka na kuchukua hatua ili vijana wetu wasitapeliwa?....na badala yake solution inayoona ya tatizo hili ni kuwatimua tu Vijana warejee walitoka??
 
Kumbe inawezekana kuwafukuza watu wasio na kazi mkoa wako,sasa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam afuate mfano huu maana mkoa umejaa wazurulaji kutoka mikoani.Watu wasio na kazi maalumu warudi mikoani walipotoka hii itapunguza wizi,utapeli,omba omba na kujazana kwenye mabasi.
 
CCM nchi iliwashinda tangu enzi ya nyerere. Alipong'atuka Nyerere na CCM ilitakiwa ing'atuke
 
Kwa nini Kilimanjaro?
Kama ni kweli ni vyema kuchukua hatua za busara sio Jambo zuri kuonesha kua mkoa mmoja wa Tanzania kua ni wakihalifu na watu wake ni wahalifu mbegu hiyo ikikua huo mkoa na watu wake wakatambua kua wanafahamika kua ni wahalifu
Taifa litaanza kumomonyoka na watu hao watajijua kua hawatakiwi Nini kitatokea
 
Kutokana na sera mbovu za CCM ajira imekuwa ngumu sana kupatikana Matapeli nao wanatumia mwanya huo kuwatapeli na kuwaibia Vijana wetu wa Kitanzania

CCM ni nuksi.
 
Yule Mkuu wa wilaya ( au mkoa) aliyeliwasilisha kwa public ya Tanzania na Dunia amelishusha hadhi para lake mwenyewe na kuwafanya wazee wa vipara wasipewe ile 90% yao yatarajiwayo kutoka kinywani mwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…