Vijana zaidi ya 500 wamekutwa wamehifadhiwa sehemu mbalimbali Mkoa wa Kilimanjaro wakifanya mafunzo yasiyojulikana

Vijana zaidi ya 500 wamekutwa wamehifadhiwa sehemu mbalimbali Mkoa wa Kilimanjaro wakifanya mafunzo yasiyojulikana

Nchi hii si ya majimbo. Kila mtu ana haki ya kuishi na kutafuta kipato mahali popote. Unapowaambia hao vijana waondoke Kilimanjaro mara moja, si kinyume cha katiba kweli? Je, hakuna vijana wakazi wa Kilimanjaro wasio na kazi?

Na kwa nini serikali inajiondolea lawama kwa sababu wao ndiyo waliwapa hao watu vibali na leseni za kufanya kazi zao, leo wanajifanya kama hawawajui vile.
 
kuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kagaigai, ametoa siku saba kwa vijana zaidi ya 500, wanaodaiwa kutapeliwa ajira na kampuni ya Alliance Motion in Global, mjini Moshi, kurudi makwao.

Kagaigai ametoa agizo hilo leo Jumatano, Septemba 15, 2021 wakati akizungumza na vijana hao ambapo amesema watakaokiuka agizo hilo na kuendelea kuwepo mkoani Kilimanjaro baada ya siku saba, watahesabika ni wahalifu na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu huyo pia alimuagiza Kamanda wa Polisi Kilimanjaro, kufuatilia mtandao wote uliohusika na utapeli huo kwa kuwahoji viongozi halali wa kampuni hiyo na watuhumiwa wafikishwe mahakamani haraka.

Vijana hao kutoka mikoa ya Mara, Tabora, Singida, Mbeya,Shinyanga, Kigoma na Tanga, wanadaiwa kutapeliwa ajira walizoahidiwa katika kampuni ya Alliance Motion in Global na mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Joseph.
Vijana hao wanadai kutozwa Sh200,000 hadi Sh900,000, na kuahidiwa kupewa ajira, kwa sasa wamepangishiwa vyumba katika kata ya Majengo na Njoro mjini Moshi na chumba kimoja wanakaa watu wanne huku wakidai kuishi mazingira magumu na hawana chakula.

Kigaigai amesema tukio hilo ni hatari kwa usalama na kumuagiza kamanda wa polisi kuwasiliana na makamanda wa polisi mikoa mingine ili kufuatilia mtandao huo unaojihusisha na utapeli huo hapa nchini."Ninyi mlikuwa mnashughulika na wezi na mmetapeliwa, poleni sana vijana, hakuna utaratibu wa mtu kuomba kazi na kuambiwa atume fedha kwanza na mimi ninachoelekeza rudini makwenu mlipotokea" amesema Kagaigai. "Wote mlioitwa na kampuni hii walioko Kilimanjaro, ndani ya siku saba, muwe mmeondoka Kilimanjaro mrudi makwenu, mnaweza kuharibikiwa maisha na nisingependa hilo litokee, rudini nyumbani mkafanye kazi halali"
"Kwa kijana ambaye hataondoka, tutamchukulia ni mzururaji na sheria ya uzururaji itafanya kazi yake, lakini niombe wakuu wa mikoa wenzangu hili wimbi ni baya, yawezekana pia lipo mikoa mingine, tushirikiane kulidhibiti hili" amesema.
Amewataka Wenyeviti wa mitaa na watendaji wa Serikali za mitaa kurejea utaratibu wa zamani wa kuwahoji wageni wanaoonekana katika maeneo yao, ili kudhibiti matatizo kabla ya madhara.
"Wenyeviti wa mitaa na watendaji, naaomba tuanze ule utaratibu wa zamani, ambapo alikuwa akionejana mtu hafahamiki, alikuwa akihojiwa na taarifa kutolewa kwa uongozi wa juu, sasa Kilimanjaro ni lazima turudi huko, tukiona wageni tuwahoji na tukipata shaka tuende zaidi hadi polisi". Akizungumza mmoja wa vijana hao, anatokea Mkoa wa Mara, Stephano Chacha, amesema wanaishi mazingira magumu na kwa sasa hawana chakula.

"Wakati tunakuja niliambiwa nije na Sh250,000 na baadae nilipofika walimpigia baba yangu simu kumwambia kuwa nimefaulu vizuri, atume Sh600,000 kwa ajili ya kutumiwa vifaa mbalimbali na kompyuta na hela ile ikatumwa," amesema. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amesema wanaendelea kuwashikilia watu sita na msako unaendelea kumtafuta mmiliki wa kampuni hiyo. "Yapo madai kuwa watu hawa baada ya kubanwa Kilimanjaro, wamekimbilia mikoa mingine, na kwa mujibu wa taarifa wamekimbilia Singida, Mbeya na mikoa mingine, niombe makamanda wenzangu, tusaidiane na kupeana taarifa za kundi hili linalotapeli watu kwa mgongo wa kuwapa ajira" amesema.

Source:Mwananchi
Huyu Mkuu wa Mkoa ndiyo aliyekataa kutoa fedha za matibabu ya Lissu akiwa katibu wa Bunge ???

No wonder anataka vijana waondoke mkoani kwake ndani ya siku saba sasa sijui watapaa kwa ungo.!!!!!!.

[emoji706][emoji706][emoji706]
 
Bado wanapika ile kesi ya Freeman ili ionekane vijana hao wanapatiwa mafunzo mkoani kwa akina Freeman

Unatumia kiungo gani kufikiri mkuu. Hivi Mbowe alikuwa na sifa yeyote ya kuwa Rais wa Tz. Unampa ukubwa ambao hana. Maisha yanaendelea huko mtaani. Mbowe is nothing.
 
Hapa naona mchanganyiko maalum.Wanasema wengine walikuwa wanapata mafunzo maalum yasiyojulikana,mara wanasema wameitwa kwa ajili ya kupewa ajira bila ajira kuwepo yaani wametapeliwa.Sasa kipi ni kipi,mnazidi kuwapa watanzania wasiwasi.

Toeni taarifa zisizo za kubabaisha na kugongana.Hawa hawana haki ya kutafuta ajira Kilimanjaro? au ni wakimbizi.Sioni ni kwa nini wanafukuzwa kana kwamba wao sio Watzd.
Hii taarifa ilivyotolewa ni mkakati wa 'kuathiri akili za watu wengi' ili waanze kufikiria kuwa hao watu walikuwa wanapatiwa mafunzo ya uhalifu, tena ugaidi kabisa. Kumbuka hao vijana wamekamatwa Moshi, na Mbowe ambaye leo alikuwa mahakamani anatokea Moshi, na akina Kingai 'walikamata magaidi' Moshi. Tatizo la hawa vijana ni tatizo la serikali ambayo inajivua na kujiweka kando. Inashindwa kutengeneza miundombinu rafiki kwa vijana kujiajiri, hapo TRA sasa hivi kupata Taxi Clearance kwa mtu anayetaka kujiajri ni balaa, mara anaambiwa ajaze vitu gani sijui kwa e-filling wanakulamba mihela kibao...hii nchi ni hovyo kabisa!
 
Huyu Mkuu wa mkoa hana utu kabisa na hafai kuongoza jamii yeyote hao ni watoto wa Wawatanzania sio wakimbizi alitakiwa kutotumia Lugha ya waondoke siku saba su tano...hawa viongozi sijui wanatolewa wapi
 
Huyu Mkuu wa mkoa hana utu kabisa na hafai kuongoza jamii yeyote hao ni watoto wa Wawatanzania sio wakimbizi alitakiwa kutotumia Lugha ya waondoke siku saba su tano...hawa viongozi sijui wanatolewa wapi
Kama aliweza kunyima fedha mgonjwa aliyepigwa marisasi unategemea utu gani kutoka kwake ?
 
Du kukosekana kwa ajira kunasababisha vijana wanakuwa vulnerable kutapeliwa. Fikiria hiyo laki tisa umekopa sasa hujui utairudisha vipi.

Ma graduate wengine wameamua kujiajiri kwenye umachinga ili mkono uwende kinywani, nao wanaambiwa waondoke barabarani.
...Hio Laki Tisa angeweza hata kuhangaika nayo mwenyewe na mkono ukaenda kinywani!
Hivi Matapeli hao walipokuwa wanatoa matangazo ya Ajira kuwarubuni Vijana, Serikali haikushituka na kuchukua hatua ili vijana wetu wasitapeliwa?....na badala yake solution inayoona ya tatizo hili ni kuwatimua tu Vijana warejee walitoka??
 
Kumbe inawezekana kuwafukuza watu wasio na kazi mkoa wako,sasa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam afuate mfano huu maana mkoa umejaa wazurulaji kutoka mikoani.Watu wasio na kazi maalumu warudi mikoani walipotoka hii itapunguza wizi,utapeli,omba omba na kujazana kwenye mabasi.
 
CCM nchi iliwashinda tangu enzi ya nyerere. Alipong'atuka Nyerere na CCM ilitakiwa ing'atuke
 
Kwa nini Kilimanjaro?
Kama ni kweli ni vyema kuchukua hatua za busara sio Jambo zuri kuonesha kua mkoa mmoja wa Tanzania kua ni wakihalifu na watu wake ni wahalifu mbegu hiyo ikikua huo mkoa na watu wake wakatambua kua wanafahamika kua ni wahalifu
Taifa litaanza kumomonyoka na watu hao watajijua kua hawatakiwi Nini kitatokea
 
Kutokana na sera mbovu za CCM ajira imekuwa ngumu sana kupatikana Matapeli nao wanatumia mwanya huo kuwatapeli na kuwaibia Vijana wetu wa Kitanzania

CCM ni nuksi.
 
Yule Mkuu wa wilaya ( au mkoa) aliyeliwasilisha kwa public ya Tanzania na Dunia amelishusha hadhi para lake mwenyewe na kuwafanya wazee wa vipara wasipewe ile 90% yao yatarajiwayo kutoka kinywani mwao.
 
Back
Top Bottom