Vijana zaidi ya 500 wamekutwa wamehifadhiwa sehemu mbalimbali Mkoa wa Kilimanjaro wakifanya mafunzo yasiyojulikana

Vijana zaidi ya 500 wamekutwa wamehifadhiwa sehemu mbalimbali Mkoa wa Kilimanjaro wakifanya mafunzo yasiyojulikana

Pesa walizotapeliwa wanarudishiwaje? Je nauli za kurudi walikotoka wanazo? Wakisharudi makwao mmliki wa global alliance atashtakiwa kwa KOSA gani?
Mafunzo gani waliyokuwa wakipewa mbona kama Kuna kificho labda kama ni sababu za kiusalama zisitajwe.
 
Hawa vijana wana umri
kati ya miaka 18 na miaka 20.
Mkuu wa Mkoa amewaagiza,amewaamuru warudi mikoa walikotoka.
Swali langu ni kwamba,kwa nini
Radia One wakubali kutangaza habari za namna hii,kwa nini wakubali kutangaza habari kwa staili hii. Mafunzo yasiyojikana ndio mafunzo gani?

-----
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kagaigai, ametoa siku saba kwa vijana zaidi ya 500, wanaodaiwa kutapeliwa ajira na kampuni ya Alliance Motion in Global, mjini Moshi, kurudi makwao.

Kagaigai ametoa agizo hilo leo Jumatano, Septemba 15, 2021 wakati akizungumza na vijana hao ambapo amesema watakaokiuka agizo hilo na kuendelea kuwepo mkoani Kilimanjaro baada ya siku saba, watahesabika ni wahalifu na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu huyo pia alimuagiza Kamanda wa Polisi Kilimanjaro, kufuatilia mtandao wote uliohusika na utapeli huo kwa kuwahoji viongozi halali wa kampuni hiyo na watuhumiwa wafikishwe mahakamani haraka.

Vijana hao kutoka mikoa ya Mara, Tabora, Singida, Mbeya,Shinyanga, Kigoma na Tanga, wanadaiwa kutapeliwa ajira walizoahidiwa katika kampuni ya Alliance Motion in Global na mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Joseph.

Vijana hao wanadai kutozwa Sh200,000 hadi Sh900,000, na kuahidiwa kupewa ajira, kwa sasa wamepangishiwa vyumba katika kata ya Majengo na Njoro mjini Moshi na chumba kimoja wanakaa watu wanne huku wakidai kuishi mazingira magumu na hawana chakula.

Kigaigai amesema tukio hilo ni hatari kwa usalama na kumuagiza kamanda wa polisi kuwasiliana na makamanda wa polisi mikoa mingine ili kufuatilia mtandao huo unaojihusisha na utapeli huo hapa nchini.

"Ninyi mlikuwa mnashughulika na wezi na mmetapeliwa, poleni sana vijana, hakuna utaratibu wa mtu kuomba kazi na kuambiwa atume fedha kwanza na mimi ninachoelekeza rudini makwenu mlipotokea" amesema Kagaigai.

"Wote mlioitwa na kampuni hii walioko Kilimanjaro, ndani ya siku saba, muwe mmeondoka Kilimanjaro mrudi makwenu, mnaweza kuharibikiwa maisha na nisingependa hilo litokee, rudini nyumbani mkafanye kazi halali"

"Kwa kijana ambaye hataondoka, tutamchukulia ni mzururaji na sheria ya uzururaji itafanya kazi yake, lakini niombe wakuu wa mikoa wenzangu hili wimbi ni baya, yawezekana pia lipo mikoa mingine, tushirikiane kulidhibiti hili" amesema

Amewataka Wenyeviti wa mitaa na watendaji wa Serikali za mitaa kurejea utaratibu wa zamani wa kuwahoji wageni wanaoonekana katika maeneo yao, ili kudhibiti matatizo kabla ya madhara.

"Wenyeviti wa mitaa na watendaji, naaomba tuanze ule utaratibu wa zamani, ambapo alikuwa akionejana mtu hafahamiki, alikuwa akihojiwa na taarifa kutolewa kwa uongozi wa juu, sasa Kilimanjaro ni lazima turudi huko, tukiona wageni tuwahoji na tukipata shaka tuende zaidi hadi polisi"

Akizungumza mmoja wa vijana hao, anatokea Mkoa wa Mara, Stephano Chacha, amesema wanaishi mazingira magumu na kwa sasa hawana chakula.

"Wakati tunakuja niliambiwa nije na Sh250,000 na baadae nilipofika walimpigia baba yangu simu kumwambia kuwa nimefaulu vizuri, atume Sh600,000 kwa ajili ya kutumiwa vifaa mbalimbali na kompyuta na hela ile ikatumwa," amesema

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amesema wanaendelea kuwashikilia watu sita na msako unaendelea kumtafuta mmiliki wa kampuni hiyo.

"Yapo madai kuwa watu hawa baada ya kubanwa Kilimanjaro, wamekimbilia mikoa mingine, na kwa mujibu wa taarifa wamekimbilia Singida, Mbeya na mikoa mingine, niombe makamanda wenzangu, tusaidiane na kupeana taarifa za kundi hili linalotapeli watu kwa mgongo wa kuwapa ajira" amesema.

Chanzo: Mwananchi
Hii iliwahi tokea Kenya ila ni kipindi cha nyuma sana, Hahaaaa
 
Hii taatifa imekua exaggerated mno na media. Hata viongozi walivyoisema ni tofauti na uhalisia, kama kiki vile. Alliance Global Motion hawajaanz kutoa seminar hizo leo. Tuendelee kufuatilia, kesi hii itakosa nguvu, kama ile ya Q-net ilivyokua kule Hai wakati wa Sabaya
Hata mimi nimeshangaa, hizi ni propaganda hatari sana ukizingatia na kesi ya freeboy... viongozi tumieni akili
 
Vijana 500 ambao uwezo wao wa ku_reason unatia wasiwasi[emoji24]...Elimu Elimu Elimu
 
Hili dogo kuna kubwa la watu waliowahi kusomeshwa wakiahidiwa vyuo kuwapatia kazi baada ya kuhitimu,
Pamoja na ada walizolipa hakuna hata mmoja aliyetafutiwa ajira.
Haya yanawakumba vijana baada ya serikali kushindwa kutoa ajira kwa wasomi hasa waliohitimu vyuo vikuu.
Serikali mna moango gani wa ajira kwa wahitimu?
 
How?ccm ndo wamefanya hayo mafunzo mafichoni mkuu?
Yote unayoyasikia na kuyaona ni hujuma za serikali inayoongozwa na ccm ili kuudhoofisha upinzani na hasa chadema kama ilivyo kesi inayomkabili mbowe ya kwamba ni gaidi.
 
kuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kagaigai, ametoa siku saba kwa vijana zaidi ya 500, wanaodaiwa kutapeliwa ajira na kampuni ya Alliance Motion in Global, mjini Moshi, kurudi makwao.

Kagaigai ametoa agizo hilo leo Jumatano, Septemba 15, 2021 wakati akizungumza na vijana hao ambapo amesema watakaokiuka agizo hilo na kuendelea kuwepo mkoani Kilimanjaro baada ya siku saba, watahesabika ni wahalifu na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu huyo pia alimuagiza Kamanda wa Polisi Kilimanjaro, kufuatilia mtandao wote uliohusika na utapeli huo kwa kuwahoji viongozi halali wa kampuni hiyo na watuhumiwa wafikishwe mahakamani haraka.

Vijana hao kutoka mikoa ya Mara, Tabora, Singida, Mbeya,Shinyanga, Kigoma na Tanga, wanadaiwa kutapeliwa ajira walizoahidiwa katika kampuni ya Alliance Motion in Global na mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Joseph.
Vijana hao wanadai kutozwa Sh200,000 hadi Sh900,000, na kuahidiwa kupewa ajira, kwa sasa wamepangishiwa vyumba katika kata ya Majengo na Njoro mjini Moshi na chumba kimoja wanakaa watu wanne huku wakidai kuishi mazingira magumu na hawana chakula.

Kigaigai amesema tukio hilo ni hatari kwa usalama na kumuagiza kamanda wa polisi kuwasiliana na makamanda wa polisi mikoa mingine ili kufuatilia mtandao huo unaojihusisha na utapeli huo hapa nchini."Ninyi mlikuwa mnashughulika na wezi na mmetapeliwa, poleni sana vijana, hakuna utaratibu wa mtu kuomba kazi na kuambiwa atume fedha kwanza na mimi ninachoelekeza rudini makwenu mlipotokea" amesema Kagaigai. "Wote mlioitwa na kampuni hii walioko Kilimanjaro, ndani ya siku saba, muwe mmeondoka Kilimanjaro mrudi makwenu, mnaweza kuharibikiwa maisha na nisingependa hilo litokee, rudini nyumbani mkafanye kazi halali"
"Kwa kijana ambaye hataondoka, tutamchukulia ni mzururaji na sheria ya uzururaji itafanya kazi yake, lakini niombe wakuu wa mikoa wenzangu hili wimbi ni baya, yawezekana pia lipo mikoa mingine, tushirikiane kulidhibiti hili" amesema.
Amewataka Wenyeviti wa mitaa na watendaji wa Serikali za mitaa kurejea utaratibu wa zamani wa kuwahoji wageni wanaoonekana katika maeneo yao, ili kudhibiti matatizo kabla ya madhara.
"Wenyeviti wa mitaa na watendaji, naaomba tuanze ule utaratibu wa zamani, ambapo alikuwa akionejana mtu hafahamiki, alikuwa akihojiwa na taarifa kutolewa kwa uongozi wa juu, sasa Kilimanjaro ni lazima turudi huko, tukiona wageni tuwahoji na tukipata shaka tuende zaidi hadi polisi". Akizungumza mmoja wa vijana hao, anatokea Mkoa wa Mara, Stephano Chacha, amesema wanaishi mazingira magumu na kwa sasa hawana chakula.

"Wakati tunakuja niliambiwa nije na Sh250,000 na baadae nilipofika walimpigia baba yangu simu kumwambia kuwa nimefaulu vizuri, atume Sh600,000 kwa ajili ya kutumiwa vifaa mbalimbali na kompyuta na hela ile ikatumwa," amesema. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amesema wanaendelea kuwashikilia watu sita na msako unaendelea kumtafuta mmiliki wa kampuni hiyo. "Yapo madai kuwa watu hawa baada ya kubanwa Kilimanjaro, wamekimbilia mikoa mingine, na kwa mujibu wa taarifa wamekimbilia Singida, Mbeya na mikoa mingine, niombe makamanda wenzangu, tusaidiane na kupeana taarifa za kundi hili linalotapeli watu kwa mgongo wa kuwapa ajira" amesema.

Source:Mwananchi
 
Nchi ya ovyo kabisa
hao matapeli yamekuwepo muda mrefu zaidi
Leo ndio wamegundua hilo
 
Du kukosekana kwa ajira kunasababisha vijana wanakuwa vulnerable kutapeliwa. Fikiria hiyo laki tisa umekopa sasa hujui utairudisha vipi.

Ma graduate wengine wameamua kujiajiri kwenye umachinga ili mkono uwende kinywani, nao wanaambiwa waondoke barabarani.
 
Hapa naona mchanganyiko maalum.Wanasema wengine walikuwa wanapata mafunzo maalum yasiyojulikana,mara wanasema wameitwa kwa ajili ya kupewa ajira bila ajira kuwepo yaani wametapeliwa.Sasa kipi ni kipi,mnazidi kuwapa watanzania wasiwasi.

Toeni taarifa zisizo za kubabaisha na kugongana.Hawa hawana haki ya kutafuta ajira Kilimanjaro? au ni wakimbizi.Sioni ni kwa nini wanafukuzwa kana kwamba wao sio Watzd.
 
Back
Top Bottom