Vikombe vyenye nembo ya timu ya mpira au picha unayoipenda

Mimi natafuta kiki kwa pikipiki nataka nifanye mass order ya vikombe 500 vyenye picha tofauti za JPM. Nataka nivigawe bure barabarani maeneo ya Kawe. Utanifanyia bei gani?
500 zinawezekana lakini si unajua picha ya mkuu , lazima kuombea kibali, njoo pm tuzungumze kuhusu bei

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo "Clip" ya "Magic Cup" ni ya kwenu ama umeitoa mtandaoni kuonesha jinsi kinavyokuwa? Maana nataka kumtumia kikombe kimoja Polepole, ili akiweka chai tu inatokea Nembo ya CHADEMA.
Clip ni kama reference Tu, lakini kikombe kinatoka kama hicho kilivyo, unaweza kumtumia hakuna neno, atafurahi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utumwa huu wa kuthamini cha wasiokujua kuliko chako unawatesa sana wa Africa, Tanzania hapa hakuna mwananchi asiye na timu iwe simba au yanga, nafikiri ungeweka tu picha ya simba au yanga au mlima kilimanjaro ungepata order nyingi ila ubunifu ndio tatizo la vijana wengi Tanzania
 
Hii ni biashara kama watu wanapenda hivyo hana budi kuendana nao
 
Sio lazima mtu achukue vikombe vya timu nilizoweka, ni timu yoyote inawezekana ,kama ni kuweka mlimani Kilimanjaro au kuweka wanyama unadhani nani angekuwa yuko interested. Kwenye biashara unatakiwa kuweka kitu cha kuvutia ili watu wakujue kisha wateja wenyewe wanaweza kujiongeza. Na nilishasema kwenye Uzi hapo juu ni picha yoyote au ujumbe wowote inawezekana kuchapisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…