Vikosi vya Majeshi ya Tigray vyaondoka Mkoani Afar

Vikosi vya Majeshi ya Tigray vyaondoka Mkoani Afar

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Msemaji wa chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF),alikaririwa na vyombo vya habari akidai Aprili 25, 2022 majeshi yao yaliondoka Mkoani Afar, akiongeza kuwa anatumai kwamba msaada wa chakula unaohitajika sana unaweza kuwasili Tigray.

Vikosi hivyo vimekuwa vikishikilia Mkoa wa Afar tokea Juni 29, 2021,hata hivyo, Kamishna wa polisi huko Afar, Ahmed Harif, alisema viliondoka katika Wilaya ya Abala lakini bado viko katika wilaya tatu za mkoa huo na walikuwa wakidhibiti barabara kuu kati ya Abala na mji mkuu wa Tigray Mekelle.

Imeelezwa kuwa kujiondoa kwa waasi Afar kutakuwa "hatua muhimu" katika ufikishaji wa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo lililoathiriwa na mzozo wa Tigray

Chanzo: Aljazeera
 
Back
Top Bottom