Jeshi la kongo na Ethiopia yote yapo top 10 ya majeshi yenye nguvu.
Lakini kama unavo jua Technologia huwa haimsamehe mtu.
Anaeendana nae mara zote huwa na faida kubwa kwene vita. Jeshi la Waasi wa tigray waliku na support ya Western technologically.
Hapa n pamoja na kuwavujishia satellite na...
Mpatanishi wa Umoja wa Afrika katika mzozo wa Tigray, #OlusegunObasanjo, ameliambia jarida la Financial Times (FT) kuwa idadi hiyo imetokea ndani ya miaka miwili ya mapigano.
Mzozo ulianza Novemba 2020, baada ya Waziri Mkuu #AbiyAhmed kuamuru mashambulizi dhidi ya vikosi vya Tigray kwa maelezo...
Ripoti Mpya iliyochapishwa na Shirika la Top10VPN inasema kukosekana Mtandao huko Tigray, Ethiopia Mwaka 2022 kumezigharimu Biashara Nchini humo Dola za Marekani Milioni 145.8
Kuzuia Intaneti pamoja na kuweka vikwazo katika Upatikanaji wake huwaathiri Wananchi Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa...
Wanajeshi wa Eritrea wamefanya mashambulizi makubwa katika eneo la Tigray nchini Ethiopia, msemaji wa kundi la waasi la Tigrayan, TPLF, amesema. Mjumbe wa Marekani alisema kuwa Marekani inafahamu kuhusu wanajeshi wa Eritrea kuvuka kuingia Tigray, na akalaani kitendo hicho.
Serikali ya Eritrea...
Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wanasema wanaamini kuwa Serikali ya #Ethiopia inahusika na uhalifu dhidi ya binadamu unaoendelea katika eneo la #Tigray, Kaskazini Mwa Nchi hiyo
Katika Ripoti hiyo, Tume ya Wataalamu wa Haki za Kibinadamu iliangazia kile ilichokiita taarifa za kuaminika za mauaji...
Msemaji wa chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF),alikaririwa na vyombo vya habari akidai Aprili 25, 2022 majeshi yao yaliondoka Mkoani Afar, akiongeza kuwa anatumai kwamba msaada wa chakula unaohitajika sana unaweza kuwasili Tigray.
Vikosi hivyo vimekuwa vikishikilia Mkoa wa Afar...
Shirika la afya ulimwenguni WHO limepata kibali cha kusambaza vifaa vya matibabu katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia, ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya miezi sita, lakini uhaba wa mafuta bado unakwamisha zoezi hilo.
Mkurugenzi wa shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza kwamba...
Kumekuwa na kilio cha muda mrefu cha kuzorota kwa hali ya kibinadamu huko Tigray, Kaskazini mwa Ethiopia.
Hali ya vita inasemekana kusababisha vifo, njaa na hata miundombinu msingi kama umeme, barabara na majengo.
Kwa hali inayoripotiwa na viongozi wa Tigray, Jamii ya Kimataifa haijachukua...
Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu hali mbaya ya Njaa Kaskazini mwa Nchi hiyo ikielezwa zaidi ya 80% ya Familia hazina uhakika wa chakula, hali inayopelekea Watoto chini ya miaka mitano kuwa na Utapiamlo.
Mashirika ya Misaada yamekuwa yakipata changamoto kufikisha mahitaji Mkoa wa Tigray ambapo...
Serikali imeridhia kuondolewa Hali ya Dharura ya miezi sita iliyowekwa Novemba 2021 baada ya Vikosi kutoka Tigray kusema vilikuwa vinaelekea Mji Mkuu wa Nchi hiyo, Addis Ababa
Mwezi Desemba, Mamlaka zilisema Jeshi lilikuwa linaondoa Vikosi vya Tigray katika Mikoa ya Amhara na Afar. Waziri Mkuu...
Serikali ya Ethiopia imetangaza kuidhibiti tena miji miwili ya kimkakati ya Dessie na Kombolcha, mwezi mmoja baada ya kushikiliwa na wapiganaji wa Tigray
Hatua hiyo ni ya hivi karibuni katika mfululizo wa ushindi wa haraka katika uwanja wa vita unaotangazwa na vikosi tiifu vya waziri mkuu Abiy...
Umoja wa Mataifa (UN) umesema takriban watu 1,000 (wengi kutoka Tigray) wanashikiliwa katika Miji mbalimbali Nchini humo tangu Hali ya Dharura ilipotangazwa Novemba 02, 2021
Maelfu wamefariki dunia na zaidi ya watu milioni mbili wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na mzozo kati ya Mamlaka...
Jeshi la Nchi hiyo limewataka Wanajeshi wa zamani kujiunga nao wakati linapambana na Waasi. Wito huo unakuja baada ya Vikosi vinavyoongozwa na TPLF kuendeleza nia ya kwenda Mji Mkuu, Addis Ababa
Hali inayoendelea Ethiopia imepelekea Marekani kutoa tahadhari kwa Raia wake kuondoka mapema...
Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres Jumatano ameitaka serikali ya Ethiopia kuruhusu utoaji wa haraka wa misaada ya kibinadamu kwa mamilioni ya watu kaskazini mwa nchi bila pingamizi.
Hayo yanajiri wakati maafisa wa Umoja wa mataifa wakiripoti vifo kutokana na njaa.
Wakati wa...
Marekani yasema itaiwekea vikwazo Ethiopia baada ya serikali ya nchi hiyo kuwafukuza maafisa saba wa mashirika ya kutoa misaada ya Umoja wa Mataifa ambao wanadaiwa kujihusisha na maswala ya ndani ya nchi hiyo.
Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia imewapa maafisa saba wa Umoja wa Mataifa muda...
Miezi kumi tangu kuanza kwa vita vya Tigray, Umoja wa Mataifa umeonya hali ya kibinadamu katika mkoa huo wa kaskazini mwa Ethiopia inaelekea kuwa mbaya zaidi, ukilaumu kile ulichokiita mzingiro wa misaada kwa hali hiyo.
Mapigano yalizuka Novemba 2020 kati ya vikosi vya serikali ya shirikisho na...
Vikosi vya waasi kutoka mkoa uliokumbwa na vita kaskazini mwa Ethiopia wa Tigray, vimeushutumu Umoja wa Afrika kwa upendeleo, siku chache baada ya Jumuiya hiyo kumteua rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, kuwa mpatanishi katika mzozo huo.
Msemaji katika chama cha ukombozi wa watu wa...
Wakati Ethiopia ikiwalaumu Waasi kwa hali inayoendelea Tigray, Waasi hao wamesema vizuizi vilivyowekwa na Serikali ndiyo sababu ya hali mbaya ya eneo hilo wakisisitiza Jamii za Kimataifa kukwama kuchukulia hatua dhidi ya Waziri Mkuu kumeongeza tatizo
Wamesema Mfumo wa Huduma za Afya umeharibiwa...
Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) limeonya hatari ya kuisha kwa chakula cha misaada kuanzia wiki hii katika eneo la mapigano la Tigray nchini Ethiopia.
Zaidi ya watu 900,000 wapo katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa ikiwa ni kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.