Wakuu
======
Katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu, kunashuhudiwa ongezeko kubwa la vikundi vinavyozuka na kujitambulisha kama "wafuasi wa mgombea fulani". kwa mfano Vinyozi wa mama,Samia for us, wachekeshaji wa mama,Mbunge Cup, Diwani Cup na vingine vingi, vinaibuka ghafla mitaani na vijijini vikifanya shughuli mbalimbali — kugawa zawadi, kufadhili mashindano ya michezo, au kusaidia kwenye shughuli za kijamii.
Kwa nje, vitendo hivi huweza kuonekana kama upendo kwa jamii au harakati za maendeleo. Lakini kwa mtazamo wa kisiasa na kisheria, maswali ya msingi huibuka: Je, vikundi hivi havitumiki kama chombo cha kisasa cha rushwa ya uchaguzi? Je, ni halali kutoa zawadi kwa wananchi kwa jina la ufuasi wa kisiasa?
Sasa kuna hawa Samia Golden Girls, Wameanza ziara ya mtaa kwa mtaa Nchi nzima kuhamasisha wanawake na mabinti kushiriki vema kwenye uchaguzi mkuu
Chanzo: Lemutuz tz