Vikwazo vinavyowekwa dhidi ya Klabu ya Chelsea vitaifutilia mbali

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Hii klabu ilianza mwaka 1905 na mkongwe tokea kuanzishwa kwake.
ila vikwazo ambavo vimekuja kuathiri kutokana mgogoro wa urusi na ukrain kwa kuwa mzamini wake abromovich kuwa karibu na putin ! au pesa alizowekeza kuwa tishio kwa nchi ya wingereza.

Kuzuiliwa kuuza na wazamini kujitoa na pili kufreez account zote ni kitendo cha kuimaliza hii club na kuitoa kwenye ramani.

kama hivi vikwazo vikifika hata miaka kumi basi chelsea itakuwa ishafia mbali kwa haya
 
Abromovich alidhamini Chelsea Kwa fedha za Damu.

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Abromovich alidhamini Chelsea Kwa fedha za Damu.

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
Bila ushahidi kuwekwa hapa ni sawa na zile hadithi za Juma na Uledi kwamba Baba yale Juma ana ngoma kuuuubwa Watu wanacheza mpira juu na chini ya uvungu wa hiyo ngoma magari yanapita, Baba yake Uledi ana pesa ambazo zikipangwa juu ya reli noti za elfu kumi kumi zinaweza kuanzia Dar mpaka Dodoma
 
Hii timu haiwezi kufa nafikiri hivi ni vikwazo vya mda tu.. lengo lao wanataka kumfilisi jamaa tu..timu iwe chini ya serikali then wao waiuze..

Kuchanganya football + politics ni upimbi wa kiwango cha lami
 
Wameionea sana hiyo club, huyo mwamba club si aliikuta na ataiacha pia sasa ni kipi kinafanya waiminye namna hiyo!?

Na hata mchizi alisema club ikiuzwa ye hataki kitu japo anaidai.
 
Nilivoons umeandika neno kama WINGEREZA,WAZAMINI.Nikajua kabsa kichwani hamna kitu
 
Vita ya kiuchumi ni mbaya sana ndugu zangu au nasema uongo ndugu zangu cheltako.
 
Lengo wanataka wamdhulumu full stop , Yani auze alaf hela wampige Pini , mana walishtukia chenga yake ya mwili ya kuuza timu ili akasaidie wahanga kule Ukraine , wakamgundua
 
yule aliwekeza Chelsea kimkakati yule na mfadhiri mkuu wa majasusi wote kutokea urusi namambo mengine ya serikali ya urusi nchini petu uingereza
 
Utamu wa soka la ushindani unapunguzwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…