Vikwazo Vinavyozuia Ukuaji wa Kilimo Tanzania

Vikwazo Vinavyozuia Ukuaji wa Kilimo Tanzania

Vikwazo vingine ni Ardhi

Tatizo la ardhi ni kubwa sana.

unakuta mashamba yenye rutuba wanagaiwa wawekezaji halafu wazawa wanakuwa vibarua. kwani nini mzawa asitumie nguvu kazi yake kujiajiri katika ardhi yake kama heka 5 au 10?

unakuta viongozi wa serikali wanahodhi ardhi heka 500 au elfu - pengine unakuta mwekezaji anapewa ardhi hekari 5000 mpaka 100000.

Watanzania hatuna haki ya kugawiwa ardhi.

Hapana! Ardhi siyo tatizo kwa Mtanzania. Tuna ardhi kubwa sana inayofaa kwa kilimo lakini haitumiwi ipasavyo. tatizo lililopo kwa wakulima wetu ni uwezeshwaji mdogo yaani anzia katika mitaji ya kupanua kilimo. Kilimo chetu kinategenmea jembe la mkono hivyo kunakuwa na ufanisi mdogo sana katika uzalishaji, badala ya kulima ekari labda 10 watu wanaishia kulima ekari 1 au 2 kwa familia ya watu 10 hapo unategemea nini? Hapa tunaweza kusema kwamba teknolojia inayotumika katika kilimo chetu ni duni sana (mbegu zinazotumika, madawa n.k).

Angalia pia uwezeshaji kwa wataalam wa kilimo, hawatumii utaalam wao ipasavyo katika kuwasaidia wakulima wetu ili waweze kuboresha kilimo chao. Pia shida iko kwa watafiti wetu, mara wanapokamilisha utafiti wao hawarudishi matokeo ya utafiti huo kwa wakulima ili uwasaidie kuboresha kilimo chao mara mtafiti anapokamilisha lengo la utafiti wake na kupata hicho alichokuwa anakitafuta anaachana nao. Hivyo katika kilimo kuna vikwazo vingi sana.
 
Back
Top Bottom