Jamii inaongozwa na ujumla wa mifumo na taratibu zinazoathiriwa na belief systems ( imani za kidini, mila, desturi, haki na uhuru wa kujieleza au kudai haki etc).
Nchi nyingi hasa za Kiafrika zimeshikilia sana imani ( za kidini au kimila) kama nguzo za jamii zao na kuwa na kiwango kidogo cha uhuru wa mawazo au hata kudai haki mbalimbali..nchi hizi nyingi hujikuta zina maendeleo hafifu. Nchi kama Sweden au Uholanzi ambazo hutoa uhuru mwingi kwa wananchi wake..kuna haki za watoto na wanawake za kiwango cha kutisha - zimepiga hatua kubwa kimaendeleo.....
Kwa maneno mengine... kadiri jamii inavyoshikilia mila ( traditions) ndivyo kiwango cha maendeleo kinavyokuwa chini..
Je, ina maana mila, desturi au hata imani za kidini hudumaza maendeleo?
Swali lako zuri dada yangu lina majibu ya ndiyo mengi na ya hapana mengi kutegemea mjibuji ana ufahamu gani
Si kweli kuwa mila na desturi zinadumaza maendeleo. Mila na desturi zinatokana hsa na hali ya watu wa mahali hapo, mazingira n.k , mtu anayeishi Dodoma, ni likely akawa na utamaduni tofauti na anayeishi pwani. Mila na desturi uathiriwa pia sana na hali ya hewa,, majanga n.k
Kwa mfano mila zetu wengi tulizoea kulima kwa umoja kuishi kwa umoja na kucheza ngoma vipindi vya mavuno , kutunza mazao na kuyatarisha mashamba kwa ajili ya kilimo kijacho na vizazi vijavyo.
Watu wanaoishi kwenye hali mbaya kabisa za hewa kijiografia let say, nchi za ulaya, asia na america, tabia na tamaduni zao zinaendana sana na kukabili hali hizo na kwa sababu ni ngumu mafanikio ya kukabili hizo hali yanapitia hatua nyingi sana.
Dini pia ina mchango wake wa kuleta maendeleo au kudumaza kulingana na ilivyopokelwa; here is my view in a nutshell
Geographical position
Wanaoshi kwenye tropical, where they can experience all four seasons without any problems and threats, wengi hufurahia hali hii. MAANA ndiyo hasa unakuwa kama unaishi duniani!! study zinasema watu wanaoshi kweny tropical wana furaha sana and peace of mind kulingana na watu wanishi nchi za baridi sana, jangwani au sehemu za matetemeko n.k
Na usipoufanyisha mazoezi ubongo kawaida unadumaa, we can not innovate anything kwa sababu hatuna shida ya kufanya hivyo! (hapa nasema as if hakuna influence ya mataifa ya nje)
Nchi za ulaya wana onekana wana akili kwa sababu hali ya mazingira ya nchi zao imewapelekea kuwa hivyo, taabu na dhiki walizopitia sisi kamwe hatutakuja kuzipitia
Tamaduni
Tamaduni zina nguvu sana, mila zina nguvu mno, ukaribu, ujima, au tulivyokuwa tunaishi kama waafrika, ilileta na inaleta uhusiano wa nguvu sana kati ya mtu na jamii anayoishi. Kwetu sisi mtoto ni wa jamii au jumuiya, kwa hiyo kila afanyacho mtu kina reflect jinsi gani alivyofundishwa na jamii yake; Ubora wa mtu au ubovu ulitokana na jamaa ndugu zake unless atokee mtoto unique kama Okonkwo (Things fall part) ambaye alisema anataka kutokuwa mvivu kama baba yake.
Ndiyo maana kama kabila fulani ni wavivu basi asilimia kubwa ni wote , genes zimeshaingia damuni, so kama kabila lako lilikuwa na utamaduni mbaya usioleta maendeleo basi mtakuwa hivyo hivyo. Tamaduni zinaweza kuvunjwa kutokana na externa force kama maingiliano na jamii zingine, dini , elimu n.k
Dini
Dini hazina ubaya dini kama dini; Ila mapokeo mabaya ya dini ndiyo yanaleta matatizo, dini zetu kubwa mbili zina matatizo makubwa:
waislamu-Tabia ya kuwapeleka watoto madrasa na kuhakikisha mtot anafuata uislamu
Ukristo -tabia za kupeleka watoto makanisani, kuwabatiza wakiwa watoto na kuhakikisha wanafata dini za wazazi.
Tabia hizo zote hapo juu ya dini hizi mbili ni mbaya kama zitaendelezwa vibaya! mtu akizaliwa anakuwa mtu tofauti kabisa na wewe hakuna ubaya kumpeleka mtoto msikitini au makanisani, ubaya unakuja pale tunapolazimisha, kuaminisha na kuwamezesha dini hawa watu tangu wakiwa watoto. Refer point yangu ya utamaduni, ubongo unaathiriwa zaidi na jinsi unavyolelewa , ubongo nao unakuwa kulingana na unavyopata challenge.
Kumbuka sisiemi tusiwapelke watotot maknisani au misikitini, ni vizuri kabisa , ila wakienda na wakafika umri wa kuwa huru kujifunza wajifunze, waulize, wasiambiowe kuuliza maswali ni dhambi au Mungu hapendi! kuuliza maswali ni kufuru! sasa huyu mtot nyumbani hawezi kuuliza, msikitini au makanisani hawezi kuuliza, eventually akienda shuleni hawezi kumuuliza mwalimu, ndiyo tunaambiwa confident yetu ipo chini!
Naamini mtu akizaliwa ni mtu huru kabisa na mwenye mawazo na malengo yake , parents should only guide them in good way, unaposema mtu hawezi kiuwa na tabia njema pasipo kuwa mwislamu na mkristo ni kuvunja haki za binadamu! unapomwambia mtoto unaweza kuwa na tabia nzuri na dini ni kichocheo ni vizuri pia, mzazi mlevi , jirani mzinzi na wote wana dini na watoto wanajua, likely kesho naye anafuata huko huko, MLISHAPATA KUULIZA HIVI VIONGOZI WANAOAPA KWA KUTUMIA vitabu vya dini watailinda katiba are they serious? dini leo zimegeuka ni vichaka vya kuficha wezi wote!!
Ukishaanza kumbana mtoto na kumwelekeza njia za dini kwa nguvu, basi unaharibu system nzima ya kumuwezesha ubongo wake kuuliza, kufikiri, kutawala mazingira, huyu mtu anakuwa na ubongo tegemezi kwa sababu ameshaanzishiwa kunyoshewa njia ya kuishi.We can learn this from animals, hata watoto wadogo wakinyonysa sana maziwa huwa wavivu kula chakula !!!!!
Ndio unakuta dini zote hizi watu wakiwa wakubwa huwa wengi hawazifuati, kama kuzifuata zinafuatwa kwa woga wa jamii lakini siyo kuwa watu wamezipenda kutoka moyoni. Hatujaweza kushawishi kwa SABABU na nguvu ya concepts zilizomo ndani ya hivyo vitabu.
TULICHOWEZA ni kulazimisha kutokana na nguvu zetu za uzazi. Ndiyo maana wazazi wakiona watoto wao wanataka kubadili dini wanakasirika sana kuliko mtoto akisema anataka kuwa shoga!!
Udikteta huu wa fikra za dini, julisha utamaduni tuliokuwa nao, jumlisha sehemu tuliyopo basi ndiyo unaona matatizo mengi sana ya kijamii tunayo. Na dini waliozileta walizileta kwa vipindi vibaya -waarabu walileta na kuchukuwa watumwa kwa nguvu, hivyo swala la kuwa mwislamu aidha ni kwa nguvu au kujikomba kwa waarabu,. wamisionari walileta dini juu ya mgongo wa ukoloni, japo hawakulazimisha, lakini walitumia saikolojia kulazimisha, kuwapa zawadi watu, kuwatengenganisha watu, na wengine wakakubali kuwa wakristo kwa kujikomba au kutaka zawadi, achilia mbali mabavu, wazungu waliopigana vita na mababu zetu na kuleta dini baadaye bado ni yale yale sawa na waarabu tu!
Akili huru za vijana au jamii husika uleta maendeleao huru, akili huru inatayarishwa inajengwa, japo leo hii wenzetu wana watu wachache makanisani, uhuru wao umesiaid akujua pumba na mchele, wanaoenda kanisani wanaenda kweli kweli na wanafuata dini mno, wanaoenda kwenye tabia mbaya wanazifanya kweli kweli, yaani kila mmoja yuko huru na anchokisema. Nguvu za ushawishi no bora sana kwa kuenenza dini kuliko ubabe wa aidha mzazi au utawala. Sasa kama akili haiko huru kuwaza, itakuwa tegemezi na mbaya tunarithi kutoka kizazi kimoja mpaka kingine!
Hivi watoto wa Chenge, Lowassa, Karamagi, RA kitu gani kitawazuia kuwa mafisadi? na wazazi wao still wanaenda makanisani na misikitini nako wanapokelewa vizuri kabisa!
Unaona kabisa jamii yetu haikutegemewa kuwa katika hali ya leo hii, kila mtu anawaza gari, nyumba, simu, PC kwa gharama zozote zile hata kuiba, baadaye ajionyeshe na jamii imtambue! unaona wazi kuwa mind yetu imetawaliwa zaidi na jamii na siyo mtu individually! we even not think of next generation! hakuna mipango ya miaka 100 ijayo!
Dada WoS leo tunahitaji kiongozi anayejua tabia zetu, na ambaye amekombolewa na hali hii, tumeona uvivu tunao umetokana na mazingira, pamoja na tamaduni zingine we as Tanzanian we are in a better position to rule the world! we have everything,
In principles ilitakiwa nchi tajiri kuliko zote duniani iwe Afrika!, we have everything kuanzia hali ya hewa, mali asili watu wenye manguvu, ngozi imara, miili imara n.k, ila sababu za kisaiolojia zimetufanya tuwe nyuma sana.
Hivi ndivyo ninavyofikiri