Nliwahi kumsikia mtu akiitwa mwanafalsafa wa imani za kijamaa na kikoministi, Karl Max, katika maandiko yake anasema "...religion is opium of the people",kwamba kwa imani za watu kama hata kama unaonewa na mabwanyenye,hutakiwi kurudisha "..just turn the other cheek.."
Ila nitofautine kidogo na mtoa maada,kwa heshima kabisa,si kuwa imani,mila na desturi ndizo zinazoduma maendeleo ya Waafrika,nataka hapa niungane na Marehemu Dr.Walter Rhodney, ambaye aliweka wazi kuwa kwa tamaduni za kiafrika zilivyokuwa karne ya 15 na 16, ziliwawezesha Waafrika kupiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa wakati huo kuliko hata nchi za Ulaya. Kumbuka hata mapinduzi ya viwanda yalikuwa bado Uingereza,tayari waafrika walikuwa na system nzuri za utawala...mfano tawala kama za Ghana, Mali, Timbuktu... Mwanamutapa, Congo, Zulu...Maghreb, zilishakuwa na hata mifumo ya taaluma na sayansi na hisabati ambazo wazungu walipokuja walizikuta mfano kama Algebra zilikuwa maarufu Afrika Magharibi kabla ya kuja wazungu.
Tamaduni za waafrika zilishika katika kazi na kujenga jamii miji na ustawi wa watu...kabila kama za Fulani,Tuareg...tamaduni za watu kama Nok zilishastawi katika teknolojia ya chuma na zana za chuma mbali sana kabla ya wazungu kutia mguu Afrika.
Si kweli kuwa tamaduni au mila hizi ndizo zilizorudisha nyuma maendeleo ya Waafrika, ni wakati wa vugu mechi ya wazungu kuingia Afrika na kuharibu kila asili ya jambo la kimaendeleo la Waafrika,kuanzia mifumo ya utawala,imani,mila na hata mazingira..vyote vilihamishwa na kupewa muonekano na mtazomo wa kizungu usisaidia kupiga hatua yoyte ya uvumbuzi na ujenzi wa jamii ya kiafrika.
Angalia wasomi wa shahada za juu tuliouwa nao sasa,wote walitokana na mifumo ya elimu za kikoloni ambzo haziwawezeshi wasomi hawa kuvumbua hata sindano,zaidi ya kupiga makelele tu, elimu ya kiafrika ilimwezesha mwafrika kuweza si tu kujitegemea mwenyewe bali hata kutegemewa na jamii yake, kwani ilimjenga kuwa mbunifu na mtendaji wa mambo ya faida na maendeleo kwake na kwa watu wake,tokea akiwa mdogo naye hurithisha kwa watoto wake na watoto kurithisha kwa watoto wao kwa namna mpya inayoendana na wakati huo,jamii ziliendelea na mabaki ya historia ya kazi hizo mengine mpaka leo yapo.
Haya yote yameharibiwa na wazungu,kama nilivyosema kwa kupandikizo system mbovu zenye madhara mpaka leo kwa waafrika,tokea biashara ya utumwa, ukoloni,ubeberu,ukoloni mambo leo,utandawazi...hatua zote hizi zimechangia kufuta kabisa mila na tamaduni za kiafrika zenye faida kwa mazingira ya kiafrika.
Sikatai kuwa kuna sehemu ya lawama kwa waafrika wenyewe kushindwa kutumia fursa ya kujitawala,walau kupunguza hizi legacy..kama alivyosema Prof.A.A. Mazrui "...pasingekua tatizo wakati nchi zetu zinapata uhuru viongozi wakakaa na kufikiria mifumo sahihi ya uwongozi kwa mujibu wa mazingira ya kiafirka,kama wangekaa wakafikiria tu tuwe na baraza la mji kama la mfalme wa Buganda, Wolof,Calabar, Ghana n.k...bdala yake tumekwenda mbali kutaka vyombo vyetu vya kimaamuzi viwe kama bunge la Cananada au WestminsterAbbey model.."