The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Miaka 3 iliyopita serikali ya Marekani iliiwekea vikwazo vya kiuchumi kampuni ya vifaa vya mawasiliano ya China, Huawei kwa sababu za kiusalama.
Vikwazo vilianza kung'ata mwaka jana Huawei ikaamua kuuza kampuni yake tanzu ya Honor ili na yenyewe isije kufa kwa vikwazo vya Marekani.
Sasa takwimu zinasema Huawei imepoteza karibu 24%ya umiliki wa soko, market share kwenye soko la ndani, China. Hadi December 2019 Huawei ilikua inamiliki 41% ya soko, sasa iko 16% hadi kufikia December 2020 sawa na Apple.
Kampuni ya Oppo, Vivo zimeipiku Huawei na kuwa kampuni maarufu kwa sasa kwa China zikimiliki 22% na 20% kwa Vivo.
Wachambuzi wanasema inawezekana kufikia mwaka 2023 Huawei ikawa haipo kwenye soko ama ina nafasi ndogo sana ya soko iwapo utawala wa Biden hautaondoa vikwazo vilivyowekwa na Trump.
Kwa sasa timu ya washawishi ya Huawei imeweka kambi Washington kujaribu kushawishi utawala wa Biden wawalegezee vikwazo vinginevyo Huawei itasahaulika Duniani.
Sasa naamini kuwa Marekani bado ana nguvu ya kuiondoa kampuni yoyote ile Duniani kwenye soko. Sikutegemea Huawei itakua hivi.
Huawei's smartphone struggles are hitting it hard in China Huawei's smartphone struggles are hitting it hard in China