Vikwazo vyaathiri uchumi wa Urusi

Vikwazo vyaathiri uchumi wa Urusi

Mrengwa wa kulia

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2022
Posts
1,091
Reaction score
3,695
Kupanda mchongoma Kushuka ndio Ngoma. Wachinjaji walienda Machinjioni kuchinja Ngombe walipo fika wakakuta Ngombe wameshika Visu na Kuwasubiri wachinjaji.

Watafiti katika Chuo Kikuu cha YALE nchini Marekani wanasema uchumi wa Urusi unakabiliwa na uharibu mkubwa kutokana na vikwazo vya nchi za Magharibi, licha ya Moscow kupuuzia athari hizo.

Waandishi wa ripoti hiyo wanadai kuwa kazi yao inatilia mashaka madai ya Moscow kuwa uchumi wake bado uko imara na kuwa nchi za Magharibi zinaumia Zaidi kupitia kile kinatajiwa kuwa ni "vita vya kuzorota uchumi.”

Utafiti huo wasemaje?

Timu ya watalaamu wa Yale ilitumia data ya watumiaji bidhaa na takwimu kutoka washirika wa kimataifa wa kibiashara na usafirishaji bidhaa wa Urusi, kupima shughuli za kiuchumi miezi mitano baada ya Moscow kuanzisha uvamizi wake nchini UKRAINE [emoji1255]

Waligundua kuwa msimamo wa Urusi kama muuzaji wa bidhaa ng'ambo umeyeyushwa kabisa, baada ya kulazimika kugeuka kutoka kwa masoko yake makuu barani Ulaya kuelekea Asia..

Utafiti huo unasema uingizaji wa bidhaa nchini Urusi umeporomoka tangu vita vilipoanza, na nchi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa za kununua pembejeo, vipuri na teknolojia.

Timu hiyo iligundua kuwa uzalishaji wa ndani wa Urusi umekwama kabisa na haina uwezo wa kujaza nafasi za biashara zilizoanguka. Watayarishaji wa ripoti hiyo wanasema hali hiyo imesababisha kupanda kwa bei za bidhaa na hasira ya watumiaji.

Nchi zaMagharibi zimeiwekea Urusi vikwazo. Huku kukiwa na karibu kampuni 1,000 za kimataifa zilizofunga milango yao nchini humo, Urusi imepoteza kampuni ambazo zinawakilisha karibu asilimia 40 ya patojumla la ndani kwa mujibu wa utafiti huo.

Ripoti hiyo imesema Putin anaingilia kati kwa kutumia njia isiyo endelevu ya kifedha ili kuficha mapungufu ya muundo wa kiuchumi.

Iliongeza kuwa bajeti ya serikali ya Urusi imetumbukia katika nakisi kwa mara ya kwanza na fedha za Kremlin zipo katika hali ngumu mno kuliko inavyoeleweka kawaida.

Wakati huo huo, watafiti hao wamesema masoko ya kifedha ya Urusi – wakiweka jicho kwa utabiri wa usoni – ndio yanayofanya vibaya Zaidi ulimwenguni, hali inayopunguza uwezo wa kuvutia uwekezaji mpya wa kuufufua uchumi.

"Tangu uvamizi huo, takwimu za kiuchumi za Kremil zimekuwa za kuchaguliwa, kwa kutoa maeneo ambayo hayaonekana kuwa mazuri kwao na kuchapisha tu yanayowafaa” unasema utafiti huo.

Urusi imewekewa vikwazo vya mafuta
Takwimu mpya za uzalishaji wa viwanda wa Urusi kwa mwezi Juni zinaonyesha kuwa iliathirika pakubwa katika sekta nyingi ikilinganishwa na mwaka jana. Kwa magari, uzalishaji ulipungua kwa asilimia 89 wakati kwa nyaya za mawasiliano ulishuka kwa karibu asilimia 80. Nini kinachofuata kwa uchumi wa Urusi?

Waandishi wa utafiti wa Yale walisema Urusi haina mbinu ya kujiondoa katika janga hilo la kiuchumi kama washirika wa Magharibi wataendelea kuungana kuhusu vikwazo.

Utafiti tofauti wa Taasisi ya Ujerumani ya Masuala ya Kimataifa na Usalama uliochapishwa Juni pia unaashiria kuwa uchumi wa Urusi upo kwenye misukosuko mingi, licha ya kustahimili siki za mwanzo za kutangazwa vikwazo.
"Athari za vikwazo ndio zimeanza tu kushuhudiwa: matatizo ya uzalishaji na usambazaji yanaongezeka na mahitaji yanapungua kwa kasi.” "katika kipindi kirefu, uchumi wa Urusi utadorora Zaidi wakati kwa kiasi fulani ukiachana na biashara ya kimataifa.” Ilisema ripoti hiyo.

Source DW. Aljazeera

=========

NB: Russia kuomba msaaada wa kijeshi IRAN ni ishara tosha.

by the way tutauamini huu utafiti hadi tutakapo pata utafiti mbadala toka russia [emoji635]
 
Wanajitekenya na kicheka wenyewe,ukweli duniani kote unafahamika kuwa Urusi amesababisha mdororo wa kiuchumi duniani note.Nchi zilizoathirika zaidi ni EU na USA kuliko hata Urusi yenyewe,mfano USA inflation rate imefika 9.1% kiwango ambacho hakijawahi kutokea toka miaka 40 iloyopita.

Huko Uingereza na Germany inflation zimetoka 1.2% hadi 8%,kiwango ambacho hakijawai kufikiwa kwa miaka mingi.koifupi Urusi amewashika korodani.
 
Urusi
Kwa vikwazo alivyowekewa urusi hawezi kufanya vizuri kiuchumi asilani , kabla ya vikwazo russia alikuwa anapitwa na nchi kama india . Uchumi wa urusi uko hoi long time kitambo na ni sababu mojawapo iliyopelekea ussr kuvunjika na ashukuru Mungu kaijaalia gesi na mafuta vinginevyo ingekuwa tunaongea mengine na ndiyo maana urusi haina ushawishi wa maana kwa wenzake wa ulaya mashariki maana haina hela. Hata russians wenyewe hutaman waende west.

Angalia hata waliosoma russia wengi lazima utakuta wa mahangaiko fulani hivi kwenye maisha sasa angalia waliosema western wengi hawana hayo mahangaiko e.g. rip Dr. Mengi vs rip Dr. Shika. Putin kaenda omba msaada wa drones iran na kupata uzoef wa kuuza bidhaa na huduma kimagendo kukwepa vikwazo vya western sasa ka nchi imefikia hatua hii kwa nini kiuchumi wasiwe hoi bin taaban?
 
Hili liko wazi sana, hata kama bahadhi ya members humu kila siku wanatuletea riport ndefundefu kila siku kuonnyesha kuwa urusi mambo yako shwari.., huwezi ukatengwa na mataifa makubwa yenye nguvu kiuchumi alafu eti usipate madhara yoyote,Hilo haliwezekani hata ikitokea washirika wa marekani wakaungana kwa dhati bila kujari madhara yatakoyowapata,na wakaamua kumtenga marekani, usitegemee kumuona Amerika akiendelea kuwa super pawer
Ninachokiona hapa ni serikali ya urusi kuendelea kupika takwimu huku ikifunga mlango kwa yeyote mwenye mawazo tofauti na klemlin!
 
Marekani ni mpotoshaji nambari uno dunia nzima. Hakuna siku marekani ataandika habari ya kusifia au kuliongelea taifa lingine vizuri.

Ndio maana miaka hii tokea mataifa mengine yamemstukia katika mbinu yake hiyo ya propaganda ambayo huitumia kucheza na akili za watu imekuwa ni rahisi sana kum'mudu.

Marekani ana amini kuwa yeye ndie mtengeneza njia kwa wengine hata asipohitajika analazimisha iwe hivyo.

So hizi ulizoandika hapa mleta mada ni porojo tu za marekani kama kawaida maana anatumia media kujifarangua as if hakuna watu wenye utimamu wa kuona hali halisi.

Russia ni taifa la kisocialist anaanzaje kudhurika vibaya na mchafuko wa soko?!

Marekani ambaye ni bepari ndie anakiona cha mtema kuni zama hizi. Na ngoja BRICS na front nyingine zikae imara atafurahi na roho yake.

Atatulizwa kama kitenesi.
 
IMG_4665.jpg
 
Russian ruble is the worst performing currency of the emerging economies against USD. Imeshuka 16% mwezi huu baada ya kupanda ghafla mwezi May. Ruble ina fluctuations kali na haiko stable, haitabiriki kabisa.

Utengenezaji wa magari nchini Russia umepungua capacity zaidi ya nusu, components muhimu from European countries hazipatikani
 
Pole sana biden anaumwa covid k

Cha ajabu covid ya Biden ina fanana sana na homa ya vipindi - yaani on and off: leo kapona kesho inamrudia tena. Bottom line jamaa huyu katiri sana na mpenda kulipiza visasi na mpenda vita akiwa na lengo la kunufahisha viwanda vya silaha vya nchini mwake, na yeye anapewa mshiko baada ya silaha kuuzika - yeye na mwanae wa kiume wanaji-involve kwenye dubious deals tangu yuko makamu wa Rais,hivyo vita hii ya Ukraine ni windfall kwake na familia yake kupiga hela ndefu,ndio maana anashabikia sana vita hii ya Ukraine.
 
"katika kipindi kirefu, uchumi wa Urusi utadorora Zaidi wakati kwa kiasi fulani ukiachana na biashara ya kimataifa.”

Kipindi kirefu ni muda gani? Inahitajika specific estimates kwa ajili ya kupima usahihi.
 
Back
Top Bottom