Vilabu 15 NBC havijapata mgawo wowote miezi 3

GSM uhuni hajaanza leo...ashuruku anayemlinda otherwise JPM angemsagia kunguni.ule uchafu wake wa bandarini ulikuwa kufuru..hizi pesa analeta kwenye mpira Ni kuzisafisha tu..Timu zimeitangaza kampuni miezi kumbe hazijapata kitu..Hawa lengo lao Ni kuharibu soka tu..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
➪ Wameelezea Kwa mapana zaidi lakini suala kubwa ni Klabu ya Simba na viongozi wake kushindwa kuvaa logo za GSM,

➪ Logo ya GSM kutowekwa kwenye mechi za Simba

➪ Banners za GSM kutokuepo kwenye mikutano ya maandalizi ya mechi/mikutano ya wanahabari kwenye mechi za Simba

➪ Lakini pia Na viongozi wa Tff kutoeshimu logo zao.
 
Je, vigezo vili fuatwa kama walivyo kubaliana kimkatabaa ??? kama hapana basi bodi ya ligi na Tff wna makosa na kama vilifuatwa Gsm ata fidia hyo miezi aliotangazwa na vilabu [emoji848]
Mkuu ule mkataba ulivyofichika kulikuwa na kitu baina ya GSM na TFF,huwezi kusign mkataba halafu useme usijadiliwe
 
Sasa vilabu vingepata vipi mgao wakati kulikuwa na mgogoro wa kimkataba?

Simba hakuwa tayari, hadi hapo GSM asingeweza kuendelea na mkataba na TFF...
Popoma Utadhani Watakuelewa Mkuu.
 
Mkuu ule mkataba ulivyofichika kulikuwa na kitu baina ya GSM na TFF,huwezi kusign mkataba halafu useme usijadiliwe

Hayo ndio makubaliano ya GSM na TFF na wameshindwa Kuyatimiza, hata kama ni wewe mdhamini hauwezi hauwezi kutekeleza udhamini wako kama makubaliano ya kimkataba hayajatimizwa
 
Waliilenga SSC. Simba nao wajanja, wakagomea logo ya mchongo
 
GSM Kama ana mapenzi mema na ligi zetu basi akadhamini championship haina longolongo
Mkuu, GSM ni kampuni ya kibiashara na wenyewe wanahitaji faida kwa kila wanachokifanya

Championship haionekani kwenye TV, Timu zilizopo kule hazifatiliwi na hazina wapenzi wengi

Je, wanaweza kuwa na return ya kutosha kwenye biashara yao na wala sio kampuni ya misaada
 
Shida ilianza pale TFF iliposema mkataba Ni wao na GSM, haruhusiwi mtu mwingine kuujadili. Hapo ndipo shida ilipoanza.
Mikataba mingapi TFF inaingia na wadau mbalimbali bila timu zote kujua wala kuhoji ila kilichomponza GSM ni Uyanga wake
 
Niimejiridhisha pasi na shaka kuwa, wengi waliokuwa wanapinga udhamini wa (GSM) kwenye ligi na wote wanaosherehekea kujitoa kwake, wamegawanyika katika makundi makubwa mawili.

1. Hawajui katiba ya (TFF) hasa kuhusu suala la mkataba wenyewe unaotajwa kuwa ni wamagumashi.

2. Wanajua katiba ya (TFF), ila wanaendeshwa na hisia za ushabiki maandazi wa Usimba na Uyanga.

Kwanza kabisa hakuna sehemu yoyote ambayo (GSM) anamakosa kuhusu suala la udhamini mwenza kwa sababu yeye kama Muwekezaji alifuatwa na (TFF) akiombwa kuidhamini ligi kuu Tanzania bara na sio kwamba yeye alilazimisha kuja kuidhamini ligi.

- Jambo hilo lilithibitishwa na Rais wa (TFF) Wallace Karia ambaye alikiri kwamba wao kama (TFF) ndio walimuomba (GSM) aidhamini ligi kuu.

Baada ya (GSM) kuhakikishiwa na (TFF) + Bodi ya ligi kwamba logo yao itavaliwa na vilabu vyote (16) vya ligi kuu upande wa kushoto wa mkono wa jezi, na mabango yao yatawekwa kwenye viwanja vyote, (GSM) akakubali kuidhamini ligi....

... GSM kama kampuni wakakaa na (TFF) na bodi ya ligi wakafikia makubaliano ya kimkataba kuwa (GSM) watatoa Tsh 2.1 Billion kwa misimu (2) kwa awamu tofauti kulingana na makubaliano ya mkataba.

Kwa nini vilabu havikushirikishwa au vilishirikishwa? Hilo sio jukumu la (GSM). Kwa mujibu wa katiba ya (TFF) wenye jukumu la kuingia Mikataba yote inayohusu Udhamini wa ligi, haki za matangazo ya Tv na radio nk ni (TFF)...

(TFF) Wao ndio wanapaswa kusimamia vilabu ikiwemo kuwashirikisha na kuwajuza nini makubaliano ya Mikataba waliyoingia, japo katiba haiwalazimishi kufanya hivyo pia.

- Katiba ya (TFF) ndiyo iliyotoa LOOPHOLE ya baadhi ya vilabu kupinga Udhamini na sio (GSM)... Kwa kuwa (GSM) ni muungwana yeye ameamua kujitoa kwa sababu (TFF) imeshindwa kutekeleza makubaliano ya kimkataba waliyokubaliana.....

GSM angeamua hata kuishitaki (TFF) kwa kumchafua au kwa kutotekeleza mkataba ambao uko kisheria. Lakini yeye akachagua kujiweka kando tu.

- GSM hapa anatumika kama kichaka cha kujifichia, lakini ukweli wa mambo ni kuwa Uyanga wake ndio unamponza kwa sababu kuna Mikataba mingi tu inayoingiwa hapo (TFF) bila kuvishirikisha vilabu kwa kutumia katiba hiyohiyo iliyopo lakini hakuna klabu hata moja ambayo ilishawahi kuhoji au kulalamika kuwa haikushirikishwa.

- Mimi naamini, kama huu huu mkataba wa Udhamini mwenza ungekuwa umeingiwa na kampuni nyingine tofauti na (GSM) kusingekuwa na hoja zoote hizo zilizoibuliwa kuupinga.

- TBC wameingia mkataba wa miaka (3) kwa Tsh 300 Milioni pekee, lakini hakuna klabu inayoyapinga mabango ya TBC kwenye viwanja kwa kusingizia kuwa pesa ni ndogo,, Lakini kwa GSM aliyetoa 2.1 Billion mabango yake uwanjani yalipigwa vita sana kwa madai pesa ni ndogo !!!!
 
Tangu mkataba usainiwe Kati ya GSM na TFF na kushirikisha vilabu 15 ,vilabu havijapata mgawo ndani ya miezi yote mitatu...
Taahira kazini, hizo pesa zinatolewa kienyeji kienyeji Kama kugawa peremende eti? Unatoaje pesa wakati terms za mkataba azijatekelezwa? Waulizeni tff kwanini awajawekewa pesa watawapa majibu yenu kuliko mnavyobweka hapa na amjui chochote kwenye masuala ya mikataba kisheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…