Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Wakati wa fukuto la vilabu vya Simba na Yanga kugeuzwa kuwa Kampuni ama kumilikiwa na mtu mmoja, Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja, alisema kwamba serikali haitaruhusu vilabu hivyo vimilikiwe na watu binafsi kwa kuwa vitatumiwa na watu hao kwa manufaa ya kisiasa.
Lakini pia kuna wanachama wengi sana wa vilabu hivyo wanaoamini kwamba vilabu hivyo vikimilikiwa na watu binafsi kwa kufuata mfumo wa hisa, basi wao watanyang'anywa umiliki wa asili wa vilabu hivyo. Wengine walijenga majengo ya vilabu hivyo wengine walikuwa ni wachezaji wa zamani na wengine vizazi vyao ndivyo wanachama wa kwanza waanzilishi wa Simba na Yanga.
Lakini mpira wa kisasa ni fedha na fedha za "ufadhili" katika zama hizi zinaweza kutafsiriwa kama ni usafishaji wa fedha haramu. Kwa nini usiwekwe utaratibu mzuri kwa wanachama wa vilabu hivyo kuuziwa hisa halafu wenye uwezo wa kununua hisa nyingi ndiyo waingie kwenye bodi za kuviendesha vilabu hivyo.
Ni vyema sasa vilabu vilivyoko kwenye ligu kuu viendeshwe kwa kufuata mfumo wa hisa badala ya kutegemea hela za "ufadhili" ambao husababisha wafadhili kuabudiwa na Klabu kutetereka wafadhili hao wanapokaa pembeni.