Vilabu Ligi Kuu viendeshwe kwa hisa.

Vilabu Ligi Kuu viendeshwe kwa hisa.

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Wakati wa fukuto la vilabu vya Simba na Yanga kugeuzwa kuwa Kampuni ama kumilikiwa na mtu mmoja, Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja, alisema kwamba serikali haitaruhusu vilabu hivyo vimilikiwe na watu binafsi kwa kuwa vitatumiwa na watu hao kwa manufaa ya kisiasa.

Lakini pia kuna wanachama wengi sana wa vilabu hivyo wanaoamini kwamba vilabu hivyo vikimilikiwa na watu binafsi kwa kufuata mfumo wa hisa, basi wao watanyang'anywa umiliki wa asili wa vilabu hivyo. Wengine walijenga majengo ya vilabu hivyo wengine walikuwa ni wachezaji wa zamani na wengine vizazi vyao ndivyo wanachama wa kwanza waanzilishi wa Simba na Yanga.

Lakini mpira wa kisasa ni fedha na fedha za "ufadhili" katika zama hizi zinaweza kutafsiriwa kama ni usafishaji wa fedha haramu. Kwa nini usiwekwe utaratibu mzuri kwa wanachama wa vilabu hivyo kuuziwa hisa halafu wenye uwezo wa kununua hisa nyingi ndiyo waingie kwenye bodi za kuviendesha vilabu hivyo.

Ni vyema sasa vilabu vilivyoko kwenye ligu kuu viendeshwe kwa kufuata mfumo wa hisa badala ya kutegemea hela za "ufadhili" ambao husababisha wafadhili kuabudiwa na Klabu kutetereka wafadhili hao wanapokaa pembeni.
 
Mkuu umetoa wazo zuri lakini si rahisi kwa wazo kama hili kupokelewa kwa mikono miwili na watu kama Mzee Akilimali na mwenzake Mzee Kilomoni.

Aidha, ni watu wachache tunaoamini kuwa mafanikio huanzia kwenye hesabu kisha kwenye uhalisia. Kwa sababu hiyo, hata huu uzi wako unaweza usipate wachangiaji wengi wa mawazo.

Hebu piga hesabu ya chini kabisa kwamba Yanga au Simba ina wanachama na wapenzi Milioni 10 ambao wako tayari kuchukua hisa kulingana na vipato vyao.

Assume:
Watu 2 Milioni kila mmoja achukue hisa za TZS 100,000 = 200 Bilioni
Watu 2 Milioni kila mmoja achukue hisa za TZS 10,000 = 20 Bilioni
Watu 6 Milioni kila mmoja achukue hisa za TZS 1,000 = 6 Bilioni
JUMLA ni TZS 226 Bilioni

Kwa huo mkwanja klabu inaweza kumnunua mchezaji yeyote bila kumtegemea mtu mweupe.

Kwa hesabu hiyo, sasa linganisha na uharo wa MO anayetaka kuinunua Simba kwa 20 Bilioni!
 
Jiulize pia hao wanachama ml 10 wapo,?

Sent using Jamii Forums mobile app

Shida ni mabadiliko hayakwepeki.

Njia pekee ni kujiwezesha kwenye uelewa wa mambo ya hisa yanfanyikaje, kimsingi. Kama swala la msingi la hisa likieleweka na kukubaliana, terms and conditions yaani makubaliano na masharti yanayoendana na viwango yataafikiwa. Hii sasa ni hatua nyingine ambayo inataka kulielewa somo, na kama haiwezekani, kutumia washauri wenye utaalamu wa masuala hayo. Zaidi ya hapo inatakiwa umahiri kwenye ku negotiate yaani majadiliano kuelekea muafaka. Sasa kila pande zina maslahi yake, hivyo ni yule atakayeshinda ndiye atafaidika. MO hajaleta uharo, suala ni wenye mali: Simba kupitia mkutano wao mkuu, wadau wengine kama Baraza la Wadhamini kina Kilomoni kwa namna inayotakikana wakiongozwa na secretariat yenye uadilifu, watengeneze mihimili ya majadiliano ya kuhusu hisa wakilinda masilahi ya wana Simba wote.

MO akija na spidi zaidi, nao waje na spidi linganishi lakini msaada mkubwa, msaada wa kiufundi, kwani mnunuzi au muuzaji lazima ujue unachouza au kununua. Kwa dalili, akina Kilomoni wanaogopa kuwa kunaweza kuwa na utapeli. Ni woga mzuri lakini wajiongeze na kuja na vifaa vya ubishi wa kisayansi. Kwa upande mwingine, uongozi wa sasa na Friends of Simba, lazima waielewe jamii ya wanachama wanayoiongoza au jamii ya simba kwa ujumla. Hao ndiyo thamani ya kweli ya timu. So, as much as possible they should carry them on board yaani wawahusishe, na warejee visa vya Mpira Pesa. Wakicheza na hawa, maadui au mahasimu wao watatumia mwanya huo.
 
Nimekuelewa sana mkuu hicho ndicho kinachotakiwa kifanyike haswa wakati semina hizi zakuwaelewesha wanachama zinazo endelea nivyema watu kama nyie muhudhurie muweze kutoa mchango wenu wamawazo mazuri mlionayo sio kama hao wengine wanao sema mo ni uharo nikumkosea heshima kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu tumieni lugha nzuri mnapojadiri mambo ya kitaalamu.

Lugha za uharo hazikubaliki.
 
wazo zuri sana hili ila kuna vilabu vyetu viwili hivyoo vina kamati zao zinajiita kamati za wadhamini ndio wapigaji pesa wazuri huku wakijifanya wanaidhamini timu kumbe hamna kitu wapigaji tuu.
pili,wabongo elimu ndogo juu ya hizi mambo,kama kadi tuu wengi hatuna morale ya kununua hisa itakuaje???
 
Huku hadi kule spain kwa akina Real Madrid akina BI HINDU wapo?
 
Back
Top Bottom