Vilabu visikwepe wajibu wao wa kujenga viwanja

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Makala hii ilichapishwa katika Mwananchi la 19 Mei 2014

 
ni ukweli mtupu lakn CCM watakula wapi>? au hujui ni kwa nn Yanga wanawekewa zengwe?
 
Sawa.

Ila na wapenzi wasikwepe wajibu wao wa kuingia viwanjani, na wajibu wao wa kulipa viingilio halali.

Na wakaa milangoni wasikwepe wajibu wao wa kupitisha milangoni wenye tiketi halali tu, na wajibu wao wa kuziwasilisha hela hizo bila ya kuzidokoa.

Na waamuzi wasikwepe wajibu wao wa kuchezesha mechi kwa haki, na wajibu wao wa kutochezesha kwa mujibu wa jinsi walivyowezeshwa. Na TFF wasikwepe wajibu wao wa kuendesha ligi kwa haki. Na wa kuhakikisha kwamba timu zinashinda na kishindwa kwa mujibu wa uwezo wao, sio kwa mujibu wanavyotaka wao.

Na kamati za rufaa zisikwepe wajibu wao wa kuamua kwa haki, sio kwa kutizama warufaa usoni. Na wadhamini wasikwepe wajibu wao wa kudhamini timu na/au ligi kikwelikweli na sio kisanii.

Na wanahabari wasikwepe wajibu wao wa kutangazia mashindano ya mpira wa miguu kwa mujibu wa maadili ya taaluma yao, sio kwa ushabiki wa timu au kiongozi fulani.

Na makocha wasikwepe wajibu wao wa kufundisha kwa kadri ya uwezo wao, badala ya kuganga njaa huku wakitumiwa na timu pinzani.

Na wachezaji wasikwepe wajibu wao wa kucheza kwa moyo badala ya kujifurahisha wao au kukubali kurubuniwa na timu pinzani. Na taasisi za fedha nzo zisikwepe wajibu wao wa kutoa mikopo ya ujenzi wa miundombinu kwa asasi husika vikiwamo vilabu, badala ya kuwakomoa masikini wanaokwenda kukopa kwa ajili ya kusomesha watoto wao au shida zao nyingine za msingi.

Na waanzisha mada nao wasikwepe wajibu wao wa kuwazindua wadau wote hawa na wengineo badala ya kuvisakama vilabu pekee.
 
ni ukweli mtupu lakn CCM watakula wapi>? au hujui ni kwa nn Yanga wanawekewa zengwe?

Kwani Yanga wanacheza uwanja wa CCM? Uwanja wa Taifa ni mali ya Serikali chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, ule wa zamani wa Uhuru ni mali ya jeshi.
 

Ahsante kwa mwitikio wako chanya kaka.

Nitasema kuhusu hoja chache tu ambazo zinalenga mada yetu moja kwa moja.

Kuhusu wajibu wa washabiki kuja viwanjanai na kulipa viingilo halali. Washabiki wa hapa nyumbani hili wanajitahidi kulitimiza kwa kiasi kikubwa, kufeli kwa kunasababishwa na wadau wa juu wa tiketi na mechi, mathalani unatoa tiketi leo siku ya mechi, mshabiki atajuaje kama hii ni halali na ile ni haramu ilhali zote zinapatikana katika kituo kimoja? Kuhusu kuhudhuria, kitakwimu tuko juu kuliko majirani zetu Kenya na Uganda ambao kwao Ligi ya Uingereza ina mashiko kuliko ligi ya nyumbani.
https://www.jamiiforums.com/sports/657407-kushabikia-soka-la-ulaya-hakutusaidii.html#post9519138

Kuhusu mashirika na taasisi za fedha kukwepa wajibu wao wa kusaidia ujenzi. Si kweli kwamba mashirika na taasisi hizi wanakwepa kushirikiana na vilabu katika miradi ya maendeleo, lakini kila mtu hupenda kufanya kazi na mshirika aliye makini ili pande zote mbili zinufaike na ubia husika. Kufanya kazi na klabu ambazo zinzfanya vioja ambavyo tunavishuhudia katika ligi yetu ni kutaka hasara ya lazima na kusumbuana, timu imeshindwa kujenga choo katika jengo lake, leo uipe uwanja wa kuingiza mashabiki 40,000 na utarajie hele yako irudi, si ndoto za mchana hizi?

Kuhusu wadau kaka sisi (watoa mada) kusakama vilabu pekee. Kwa kweli tunajitahidi kuleta usawa katika kutupa lawama, maoni, ushauri na hata pongezi kwa ulinganifu kwa wadau wote, na hii utaiona kama utajaribu kusoma mada tofauti kwa wakati tofauti. Kama nikisema niguse kila upande unaohusika katika makala moja, itakuwa ni katabu na sio makala (kumbuka safu moja huwa na ukubwa usiozidi nusu ukurasa katika gazeti moja na pasingetosha kuweka maoni yote yanayogusa washika dau wote wa viwanja vya michezo.

Ahsante sana kwa mawazo yako endelevu mwangalingimungu.
 
Last edited by a moderator:
Nakuunga mkono mkuu.

Tena hili jambo halikutakiwa kuvaliwa njuga na serikali ila kila kilabu kilitakiwa kiwe na malengo haya.

Vilabu vya bongo vinaongozwa na wazee wa klabu wasiokuwa na maono ya miaka 100 ijayo kazi kufikiria kufanya ndumba na fitna tu.

Bado naamini vijana kama sisi kuna kitu tunaiona ila hakipo na hakitakuwepo
 

Waingereza husema 'I can't agree with you more'.

Ila mimi natofautiana na wengi wanaodhani kwamba vilabu vyetu, hasa Simba na Yanga, ndio wahusika wakuu wa kudumaza maendeleo ya soka nchini kwa sababu tu wanagombana, kwa sababu tu timu zao hazijatwaa makombe ya Afrika kama Al Ahly, kwa sababu tu hazijajenga viwanja vyao kama Arsenal, kwa sababu tu hazina academy kama La Masia.

Lakini tunasahau kwamba hizo timu zenye Allanze Arena, Emirates Stadium au Nou Camp, zenyewe na ligi zao zina uhai wa zaidi ya karne. Wadau wao, zikiwamo taasisi zao za fedha zilikuwa (kwa maana zote 'to be' na 'to grow') pamoja nao. Kama Azam Group of Companies ilivyokuwa pamoja na Azam Fc.

Nani anaamini kwamba fedha za kuendeshea Azam FC zinatokana na faida ya timu hiyo kuuza wachezaji na watazamaji kuangalia mechi zao? Ni swala la mdau kuwa pamoja na timu. Kama mifuko ya huduma za jamii inawekeza kwenye miradi isiyorejesha fedha kwa haraka kama Daraja la Kigamboni, itashindwaje kuwekeza kwa kushirikiana na vilabu miradi inayorejesha haraka kama viwanja vya michezo?

Kama Emirates wamewajengea Arsenal kwa masharti ya kukiita kiwanja hicho jina la mjenzi huyo ndani ya miaka kadhaa, makampuni ya kwetu yanashindwaje kuvijengea vilabu vyenye mwelekeo (Majimaji, Mwadui, Pilsner wakati huo) huku makampuni hayo yakiendesha viwanja hivyo mpaka fedha zao zitaporejea? Hatuoni kwamba Mwadui, Mseto, Tukuyu Stars, Pamba ya Mwanza zingeendelea kuwapo licha ya kushuka kwao madaraja, iwapo zingekuwa na miundombinu kama viwanja?

Yanga na Simba zinahusikaje na hilo? Hatuoni kama Yanga na Simba kupiga hatua tunazowataka wapige kutaziua timu nyingine ambazo hatuzishinikizi kutumia huu tunaouita uoza wa Simba na Yanga kuziba pengo la tofauti nazo?

Nionavyo, Simba na Yanga ni mfano wa kuigwa juu ya jinsi timu za mitaani zinavyoweza kudumu. Ndani ya ukanda huu ndio timu zilizochukua mara nyingi zaidi kombe linazohusisha vilabu, ndizo pekee ambazo hazijashuka daraja tangu ligi ianze, ndizo pekee zilizochukua makombe ya kitaifa mara nyingi zaidi, ndizo pekee zenye washabiki wengi zaidi hadi nje ya mipaka yao. Hatuoni ajabu kwamba hayo yote yamefikiwa licha ya hiyo migogoro tunayozilaumia?

Migogro ni yao weyewe lakini sifa hizi si mali wala hatimiliki ya vilabu hivyo pekee. Hata hao wanaovilaumu wana nama yakunufaika nazo. Tunapovinyooshea kidole kimoja, vitatu vinatuelekea sisi wenyewe.
 

Mashirika ya umma yana matatizo katika utekelezaji wa ajenda zake, uwekezaji ukiwemo. HAtuwezi kuyapa jukumu lote la kushikana na vilabu, hoja ya msingi inakuwa ni namna gani ambavyo vilabu vimejaribu kushikana na taasisi zenye uwezo. Huwezi kudai kuungwa mkono wakati mwenyewe hujaanzisha mwendo, kuna kipindi Adidas walijaribu kushikana na klabu ya Simba kwa kuwapa udhamini wa vifaa vya michezo, lakini walikwamishwa na ubabaishaji, kama suala dogo kama hili limekwama, sembuse mradi wa uwanja ambao utagharibu bilioni kadhaa?

Wazungumzia uchanga wa ligi, lakini zipo ligi ambazo ni changa kuliko zetu lakini zina mafanikio makubwa, mfano Ligi ya Afrika Kusini. Ligi ya Taifa ya Brazil ilianza mwaka 1959, miaka michache tu kabla ya kuanza sisi lakini wamepiga hatua kubwa sana.
Umenena vyema kuhusu kampuni ya Azam Group kushikana na timu, ni kweli tunahitaji ushirika zaidi wa aina hiyo kwa maendeleo ya Soka letu. Na hao Azam wameweza hili katika miaka minane tu ya kuwepo katika Soka la bongo, seuze timu ambazo zina karibu miaka 80 ya uwepo, hakika kuna uzembe mahali.

Umwewasifia ambingwa mara nyingi katika ukanda huu ambao ni Simba na Yanga, ukasahau kuwa katika mazingira fulani ubingwa unakuwa ni wa magumashi na kununua, rejea sakata la Prisons na Moro United kukosa ubingwa wa Bara miaka ya 2000. Visababu kama hivi ndivyo vinafanya hata ufanisi katika mashindano ya kimataifa uwe wa kusua sua, huwezi linganisha bingwa wa kweli na bingwa wa magumashi, lazima pumba na mchele vitajitenga tu.

Timu hizi zina mchango mkubwa katika Soka letu, lakini huo usiwe upenyo wa kukwepa lawama kwa hatua duni tuliyonayo hadi sasa. Wao ndio wamekuwa vinara, timu za mfano, na ndoto ya wachezaji wengi, kufeli kwao katika mambo ya msingi ndiko kumefelisha pia timu zingine.
 
Naomba nitofautiane na mtoa mada
Kwa sasa sidhani kama ni muhimu kwa vilabu vyetu kujenga viwanja,Azam pamoja na kujenga uwanja wa kisasa lakini sidhani kama wanaingiza chochote kutoka kwenye uwanja wao ,na wakicheza na timu kubwa wanalazimishwa kuja kuchezea uwanja wa Taifa .Kwa sasa ni bora kuimarisha mifumo ambayo itazisaidia hizo klabu kuongeza mapato ukiiacha viingilio vya kwenye mechi.Mfano

1.Kuongeza idadi ya wanachama na kuweka mfumo mzuri wa kukusanya ada za wanachama.

2.Kuuza bidhaa za klabu kama jezi,skafu,key holders,kalenda,picha na bidhaa nyingine za timu.Kuna wajanja wanaingiza mamilioni kutengeneza jezi feki vilabu vimekaa kimya

3.Kuimarisha timu za vijana na kuhakikisha kila msimu at least vijana 2 wanapandishwa kikosi cha kwanza,hii itapunguza upotezaji ya mamilioni yanayopotea kila mwaka wakati wa usajili
 
Naogopa tusije kuwa mimi na wewe ndio wateka nyara wa uzi huu. Kwa kiasi fulani tunakerwa na tatizo moja, na maoni yetu ni mamoja.

Tunachotofautiana, kama nikikitafsiri kwa lugha nyengine ni : nani alaumiwe kwa timu zetu kushindwa kuwa na miundombinu yao wenyewe, vikiwamo viwanja?

Tangu mwazoni, mawazo yangu mimi ni : walaumiwe wadau wote. Hoja inakuja: baina ya vilabu na wadau wengine, nani alaimiwe zaidi kwa hilo? Mawazo yangu mimi ni: wadau wengine. Kwa sababu:

1. Umetaja Ligi zilizoanzishwa baada sana ya yetu na zinafanya vizuri. Lakini hizo na kama hizo zinaendeshwa kwa mfumo unaofanana na wa Ulaya, ambako vilabu haviko juu ya FA husika. Nani alaimiwe kwa kuziweka Simba na Yanga juu ya TFF?

2. Bila ya miongozo inayofanya Ligi ichezwe kitaalamu na kulipa kibiashara, hakuna mwekezaji atayejitolea kusaidia klabu kiujima. Nchi nyingi za Ulaya, mathalan, timu kushindwa kulipa mishahara ya wachezaji inakuwa imeshuka daraja. Hilo linazifanya timu zichakarike kutafuta mapato. Ujerumani, mathalan, timu hazipaswi kumilikiwa na makampuni. Hilo linaondoa ushindani wa kibiashara za makampuni hayo kupitia mpira.

TFF ina kanuni na masharti gani kwa vilabu, yanayovifanya kulazimika kujitegemea, kuwa na viwanja vyao, n.k. Necessity is the mother of invention. Kukiwa na masharti kama hayo, timu zitalazimika kuyafuata. Kama yangekuwapo ya timu kuwa na viwaja vyao, mathalan, Mwadui wangekuwa nacho, Pilsner, Sigara, Pamba, CDA n.k. Bila ya shaka Simba na Yanga nazo zingelazimika kutafuta namna, hata kama Ni kuchangia uwanja mmoja kama ilivyo kwa San Siro/Giusappe Meazze unaomilikiwa kwa ubia na mahasimu FC Milan na Inter Milan. Na hata kama zingeshindwa na kutoweka, bado tungebaki na timu nzuri na ligi nzuri kwa sababu zilizosalia zingebaki na miundombinu stahiki.

Kwa ufupi, ubunifu wa timu za ligi zilizoendelea hadi kufikia tunapoziona umeanza na ubunifu wa wadau wengine wa soka nchini humo. Hapa kwetu, ubunifu wa timu zetu unaanza na timu zenyewe. Labda tuwalaumu Wakoloni Waingereza kwa kutohamishia mfumo wa Ligi yao kwetu wakati wakitutawala!
 

Nakubaliana na kutofautiana kwako, lakini nitapingana na mawazo kuwa ujenzi wa uwanja (ambao ni muundombinu wa msingi katika Soka) si kipaumbele kwa vilabu vyetu. Azam bado ni timu changa na haina idadi kubwa ya mashabiki kindakindaki ambao wanaweza kuujaza uwanja wao, sasa hivi wanao uwanja wasionufaika nao, lakini nadhani ni heri kuliko kutokuwa kabisa na uwanja halafu ukalazimika kuhama viwanja wakati inapotokea dharura (rejea kipindi cha Simba na Yanga kwenda Arusha, Tanga na Mwanza kisa Uwanja wa Uhuru kufungwa kwa matengenezo).

Mara kadhaa tumesikia malalamiko kuhusu makato mengi katika viwanja ambavyo si mali ya timu, sidhani kama Azam na Mtibwa wanapata matatizo makubwa sana katika hilo kama timu zingine ambazo zinadandia viwanja vya Serikali au CCM.

Mara kadhaa uwanja wa Azam umetumika kufanyia mechi zingine ambazo hazihusishi Azam na bila shaka wahusika wanaukodisha kwa fedha, mapato hayo.

Kuwa na uwanja kutakuepusha gharama za kukodi uwanja wa mazoezi kwa kila timu uliyonayo na washabiki wanaweza pia kulipa kiingilio nafuu kuja kuona mazoezi ya timu.

Azam, Mtibwa, Ashant, Ruvu JKT na Shooting kulazimishwa kuhama viwanja katika mechi za Simba na Yanga ni ulimbukeni na tamaaa ya fedha ya wezi wa mapato ya mlangoni. Huwa tunaona Ulaya timu ina uwanja wa kuingiza washabiki 15'000 na bado itacheza katika uwanja wake bila kujali inacheza na nani.
 
Still siamini kama hata wakijenga viwanja vitaweza kupunguza sana matumizi yao cha msingi ni klabu ziwe na viwanja vya kufanyia mazoezi kama ulivyosikia hata klabu kubwa AC Milan/Inter hawana viwanja wanakodisha but wana viwanja vya mazoezi.Ligi yetu kwanza ina timu chache na kutunza viwanja kuna gharama kubwa sana na ukizingatia soka letu bado linaonekana ni kama la ridhaa,naamini kuna mambo mengi ya kufanya ambayo yatazisaidia klabu kuongeza mapato yao
 

Belo!

Gharama za kujenga Uwanja huko mamtoni sio sawa na hapa. Uwanja wa Emirati kwa mfano ulijengwa kwa pauni 470 Milioni wakati Karai letu hapo Taifa lilijengwa kwa makadirio ya pauni 36 Milioni + eneo la bure la Jeshi.

Vilabu vyetu havina uwezo mkubwa sana, lakini hawashindwi kuanzisha mwendo wa kiwanja cha watu japo elfu 30 tu, Ulaya zipo timu kama Valencia ambazo zilifilisika baada ya kuingia kichwakichwa kwenye mradi wa uwanja ambao ni ghali sana kwa kule.

Tumeweza kusogea japo kidogo, taratibu tunaachana na falsafa ya 'uridhaa'. Tunaweza...
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…