Vilabu vya ligi kuu mnaitangaza Vodacom hata pasipostahili

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Posts
23,372
Reaction score
54,943
Habarini wana michezo...


Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa sasa imesimama kupisha kwa muda mashindano ya FA/ASFC (AZAM SPORTS FEDERATION CUP)

Sasa kuna makosa ambao vilabu vya ligi kuu vinapaswa kujua kuwa vinafanya au kwa kujua ama kutokujua, mdhamini wa mashindano haya naamini ni Azam ila ni ajabu mashindano haya kuchezwa huku timu zimevaa jezi zenye nembo ya Vodacom ambayo haina uhusiano wowote na mashindano husika bali ligi kuu tu.

Viongozi wa timu za ligi kuu hebu jaribuni kuwa na mikakati ya kuwa na jezi za ligi na za mashindano mengine tofauti na ligi, Vodacom kwao ni kicheko kuona jezi zenye nembo zao kuvaliwa kwenye mashindano ambayo hawayadhamini.

Kitu kingine, kama Azam ndio wadhamini wa mashindano ya FA wanashindwa nini kuzitaka timu ziwe na jezi zenye nembo yenu nyie kama wadhamini au nanyi mnaona ni suala la kawaida na kulipa nafasi ya kutokea?

Tuchukulie mfano EPL huwa tunaona timu zikicheza mashindano mengine mbali na ligi kuu ya Uingereza basi huwa na jezi zenye kuendea na mashindano husika na siyo tena EPL.

TFF, na nyie hili mnapaswa kulifanyia kazi, leo Yanga anacheza na Tanzania Prisons wote wanatumia jezi zenye nembo ya mdhamini wa ligi kuu kweli!! Hata kama nchi ni masikini timu hazishindwi kupata jezi za ziada.

Nishasema sasa.
 
Hili kosa linafanywa na timu hata Simba na Yanga ,nashangaa kwenye hizo timu kuna watu wa marketing kweli ? Wanajua maana ya hy mikataba na mashindano

Mapinduzi cup pia walivaa nembo ya vodacom

MTC | 101| [emoji769]
Sioni kama wanajua ujinga wanaofanya sikubahatika kushuhudia mitanange ya Mapinduzi ila kama ilitokea basi ni wapuuzi (wanisamehe kutumia lugha hii).

Jana Simba pia walivaa jezi zenye nembo ya Vodacom ile hali wanacheza FA.
 
Kingine mkuu ukiangalia jezi za simba wanazovaa kagere, kahata na wawa nyuma mgongoni maandishi ya madhamini yanayosomeka "Mo Sabuni ya Unga Halisi" yamefutika sasa sijui mdhamini anajitangaza vipi ikiwa anachokitangaza hakionekani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sioni kama wanajua ujinga wanaofanya sikubahatika kushuhudia mitanange ya Mapinduzi ila kama ilitokea basi ni wapuuzi (wanisamehe kutumia lugha hii).

Jana Simba pia walivaa jezi zenye nembo ya Vodacom ile hali wanacheza FA.
Hahahaha, na hapo ndio Timu kubwa zenye watu makini lkn hawaoni kitu km hicho

MTC | 101| [emoji769]
 
Asante kuona hilo. Hivi unaweza kusema GSM walibahatisha kutengeneza jezi za Yanga!! Kwanini nasema hivyo.

Wachezaji wote waliosajiliwa dirisha dogo la usajili jezi zao nyuma zina ufito mrefu ambao umepita hadi karibu na shingo kwa nyuma, namba za jezi huandikwa mgongoni mwa jezi sasa kituko ni pale unapokutana na namba ya jezi ambao haionekani vyema maana namba huandikwa kwa rangi ya kufanana na ya ule ufito nyuma ya jezi.

Jezi za wachezaji wengine waliosajiliwa kwenye dirisha kubwa ziko sawa na namba mgongoni zinaonekana vyema tu kwa sababu ufuto ni mfupi na huishia juu kidogo ya kiuno cha mchezaji.

Sasa huwa najiuliza huwenda GSM walibahatisha kutengeneza jezi hizi kama wanashindwa kutambua kasoro namna hii.
 
Mbao za Mawe, Jezi za wachezaji waliosajiliwa dirisha dogo zimechukuliwa mtaani tuu hizi tunazovaa sisi zenye mstari mmoja mrefu kutoka chini mpaka juu sasa sijui wameshindwa kuufuta ule mstari ili waweke namba matokeo yake sasa wameweka namba juu ya ule mstari namba hazisomeki vizuri ......... ligi ya bongo vituko haviishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hivi.
 
Hili kosa linafanywa na timu hata Simba na Yanga ,nashangaa kwenye hizo timu kuna watu wa marketing kweli ? Wanajua maana ya hy mikataba na mashindano

Mapinduzi cup pia walivaa nembo ya vodacom

MTC | 101| [emoji769]
Mechi ya mtibwa ya kwanza kabisaa kuna kipa wa timu pinzani alivaa Jersey ya Liverpool nilijisikia ovyo sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…