Mbao za Mawe
JF-Expert Member
- May 11, 2015
- 23,372
- 54,943
Habarini wana michezo...
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa sasa imesimama kupisha kwa muda mashindano ya FA/ASFC (AZAM SPORTS FEDERATION CUP)
Sasa kuna makosa ambao vilabu vya ligi kuu vinapaswa kujua kuwa vinafanya au kwa kujua ama kutokujua, mdhamini wa mashindano haya naamini ni Azam ila ni ajabu mashindano haya kuchezwa huku timu zimevaa jezi zenye nembo ya Vodacom ambayo haina uhusiano wowote na mashindano husika bali ligi kuu tu.
Viongozi wa timu za ligi kuu hebu jaribuni kuwa na mikakati ya kuwa na jezi za ligi na za mashindano mengine tofauti na ligi, Vodacom kwao ni kicheko kuona jezi zenye nembo zao kuvaliwa kwenye mashindano ambayo hawayadhamini.
Kitu kingine, kama Azam ndio wadhamini wa mashindano ya FA wanashindwa nini kuzitaka timu ziwe na jezi zenye nembo yenu nyie kama wadhamini au nanyi mnaona ni suala la kawaida na kulipa nafasi ya kutokea?
Tuchukulie mfano EPL huwa tunaona timu zikicheza mashindano mengine mbali na ligi kuu ya Uingereza basi huwa na jezi zenye kuendea na mashindano husika na siyo tena EPL.
TFF, na nyie hili mnapaswa kulifanyia kazi, leo Yanga anacheza na Tanzania Prisons wote wanatumia jezi zenye nembo ya mdhamini wa ligi kuu kweli!! Hata kama nchi ni masikini timu hazishindwi kupata jezi za ziada.
Nishasema sasa.