Vilabu vya ligi kuu Tanzania bara vinapataje faida kupitia soka

FUTURE HUNTER

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
2,050
Reaction score
2,651
Habari wana soka kindaki ndaki wa jf
Niende kwenye maada maoja kwa moja.Tangu nianze kuona ligi kuu Tanzania bara na kuhudhuria mechi nyingi za ligi hii ghafla nilijikuta najiuliza maswali mengi haswa eneo hili la namna vilabu vinapata pesa na si pesa tu bali ile inayokidhi mahitaji ya kuendesha team
Kwa kuangalia viwanjani bado kwa ligi yetu mahudhurio kwa asilimia kubwa ni hafifu mno na vingilio bei ni chini sana.Je vilabu vinapataje faida haswa katika kuendesha timu maana getini bado waya mkali kwa namna nionavyo.Ni mechi za simba na yanga pekee ndio walau mapato yake yanaletaga hela ya kiume mezani.Je kwa vilabu vingine hivi inakuwaje?
Je kuna gawio toka TFF,CAF na FIFA na kama lipo mgao unakuwaje?.vilabu vyote hupata mgao sawa?
Nimewaza sana timu zinavosafiri kuizunguka nchi wakipiga mechi yaani gharama ni kubwa mno za kujiendesha.
Naomba nimalize kwa kuuliza ni namna gani vilabu vya ligi kuu vinapata pesa ya kutosha kujiendesha maana viingilio bado si hela inayoweza kutosha.
Karibuni wataalam wa football.
 
Labda faida mara moja moja wanapouza wachezaji kwenda team nyingine


Ila kama team ikitaka faida lazima ufanye huge investment ndio uone faida vinginevyo utasubiria sana
 
Team inabidi ishiriki league kubwa kama club bingwa Africa na hata kushiriki world club champion
 
Ukifuatilia sana utagundua vilabu havipati faida, mpaka sasa vyanzo vya mapato vya vilabu vya bongo ni:-
1.azam tv
2.ile benki ya kenya niemsahau jina
3.mapato ya mlangoni
4.kuuza wachezaji
5.ufadhili binafsi
6.ubingwa wa shirikisho na ligi kuu.

Lakini hivyo vyote havikidhi hata gharama za uendeshaji wa timu, wanaofaidika hapo ni wajanja wajanja tu wachache ambao wanapiga mipigo yao kwenye vilabu
 
Naona Luna haja TFF wafanye research us kwa nn ligi inakuwa hvo vinginevyo wachezaji watabaki kuwa masikini
 
Creativity and innovation ndio imekosekana kwenye kuweka mfumo mzuri wa kuendesha team vinginevyo tutasubiri sanaa



Angalia mchezaji anakaa team moja miaka kwenda rudi mpaka anakuwa mzee bila ya kuuza kufanya biashara
 
Hivi hamnaga fungu kutoka CUF na FIFA kwa vilabu?. Maana juzi nimemsikia karia akiongelea mikwanja iliyokuwa inakuja toka fifa ilikuwa ni mirefu.Mabilion yale yanaendaga wapi
 
Na hii sio Tanzania tu Africa kwa ujumla changamoto sana ila kuna baadhi ya nchi kama south Africa kidogo kuna nafuu
 
Hivi hamnaga fungu kutoka CUF na FIFA kwa vilabu?. Maana juzi nimemsikia karia akiongelea mikwanja iliyokuwa inakuja toka fifa ilikuwa ni mirefu.Mabilion yale yanaendaga wapi
Pesa hiyo huwa havipewi vilabu bali ni kwa ajili ya kukuza maendeleo ya soka, zinakuwa chini ya TFF na zinasimamiwa na TFF moja kwa mojawakati vilabu hivi viko chini ya bodi ya ligi, hii bodi ya ligi ndio inatakiwa kuhakikisha ligi kuu na ligi daraja la kwanza vinakuwa na mvuto lakini si kwa kuvipa pesa vilabu bali kwa kutengeneza mazingira mazuri ya vilabu kupata pesa kama vile kuwe na mdhamini mzuri, ila mengi ni majukumu ya vilabu vyenyewe kuona vinapata wadhamini wa kutosha na vinavutia mashabiki wengi kwenye viwanja vyao ili vipate pesa
 
Sawa mkuu nimekuelewa haswaa.
 
badala bodi yaq ligi kufanya hayo unayosema yenyewe ndio inavuna pesa kutoka kwa vilabu
 
vilabu vinatakiwa viwe na viwanja vyao, kuuza brand zao kwa wadhamini na kuuzaq jezi zao Mbeya city ni timu iliyoanza kwa kasi sijui imeishia wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…