Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
VILABU VYA MPIRA MITAANI VIMEKWENDA WAPI?
Dar es Salaam tuliyokulia sisi katika 1960s hakuna ambae alikuwa hachezi mpira.
Kutoka Upanga hadi kufika Kidongo Chekundu kulikuwa na viwanja zaidi ya 10.
Tukifanya mazoezi kila siku mwaka mzima.
Jangwani kulikuwa na viwanja hata idadi yake sijui kama kuna mtu anajua.
Yanga na Sunderland (Simba) na Cosmopolitan pamoja na club ndogo za mitaani kama Young Boys, New Port, Young Kenya kwa kutaja chache walikuwa na viwanja vyao Jangwani.
Leo hakuna kiwanja hata kimoja.
Moyo wangu unavuja damu ninapoona watoto wanacheza mpira wa makaratasi barabarani miguu chini.
Kucheza mpira mzuri kulikuwa kunanyanyua heshima yako.
Angalia picha yangu hapo chini tukivaa viatu na ''shin guards.''
Nini kimetokea?