Villarreal yanyakua Kombe la Ligi ya EUROPA. Yaifunga Man. Utd kwa penati 11-10

bartenderznz

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2016
Posts
398
Reaction score
195

Klabu ya Villarreal imechukua Ubingwa wa Ligi ya Europa baada ya kuifunga Klabu ya Manchester United kwa penati 11-10

Timu hizo zilifungana goli 1-1 katika dakika 120 hatua iliyofanya mchezo kuamuliwa kwa mikwaju ya penati.

Villarreal ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli katika dakika ya 29 kupitia kwa Gerard Moreno, lakini Manchester iliweza kusawazisha kupitia kwa Edinson Cavani katika dakika ya 55.

Katika upogaji Matuta, Kipa wa Villarreal, Geronimo Rulli aliweza kuokoa penati na kipa mwenzake David De Gea na kuipa timu yake Ubingwa huo.

Kocha wa Villarreal Unai Emery ameweka rekodi ya kuwa Kocha wa kwanza kushinda mataji ya UEFA Cup/Europa League kwa mara nne (2013-14, 2014-15, 2015-16 & 2020-21).
 
Ni fainali ya EUROPA, Manchester United ikichuana na Villareal kwenye kiwanja cha Stadion Energa Gnask, Gnask, nchini Poland [emoji1200] mnano saa Nne kamili muda wa afrika mashariki.
Ni battle ya Unai Emery na Ole Gunnar Solskjaer​

 
Kwa wanaotumia antena za star times, inawezekana kulipia bundle la siku 1 (masaa 24?) ni sh ngap?
 
Kvp mkuu imefikia stage shabiki wa united unasema utaishangaza dunia zidi ya Villarreal kweli!!
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]... Fainali ni fainali usimshangae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…