Vimbwanga vya ex beki tatu wenu ambavyo hautavisahau kamwe!

Dola Iddy Wa Chelsea

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2014
Posts
2,125
Reaction score
1,526
Habari za muda huu wana jamii forums!
Sio kwa kusudi la kuwashusha heshima wala kuwadhihaki ila ni kwa vituko vyao walivyovifanya ambavyo mpaka leo ukikumbuka unacheka au unathamini sana.
MEJA=>huyu yeye nakumbuka mwaka 2002 ndio wakati alioanza kazi yeye alikuwa hajui kusoma wala kuandika,
Sasa siku moja tukamjaribu tukamwambia baba kasema nenda kasage na kukoboa mahindi tukampa 500 tukamwambia baba amesema urudishe chenchi 9000 , Tukaona mwenzetu kachukulia siriaz huyoo mashineni kaenda kusaga!,
Hahahahahaha seleka likaja kaondoka kwenda kusaga saa 10 mpaka saa 12 hajarudi ,
Ndipo tukaamua kwenda kumfuatilia tukakuta analia sana mashineni kuwa anataka chenchi yake!,
Hahahahaha aiseee tulicheka nusu kuzirai,

Vipi beki tatu wenu unamkumbuka kwa lipi?
 
Mi namkumbuka alikua ananiremba kama mwanamke siku moja kaninyoa nyusi zote akanipaka wanja na akanikata eye lid kanipaka make up uso unameremeta meremeta kwenye macho nako wanja tena sasa jioni upepo kupuliza nikawa nafunga macho sasa mama aliporudi hiyo tifu hapo nyumbani ilikua si ndogo
 
Hahahaha mkuu ulikuwa na umri gani ?
 
Uko salama Mkuu? Isije ikawa alikuharibu mpaka ukawa si ridhiki. Beki tatu nomaaa!
 
Nimegundua wewe wa juzi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…