Vimelea sugu vya malaria vyagunduliwa!

md4doctor2000

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2012
Posts
736
Reaction score
315
Watafiti nchini Cambodia (magharibi) wamegundua vimelea sugu vya malaria. Vimelea hivi vina uwezo wa kuhimili:
  • Dawa za malaria za artemisinin (dawa hizi ndizo dawa zinazotumika kutibu malaria hivi sasa duniani), ALu (mseto) ikiwa ni moja ya dawa hizo!
  • Hofu iliyopo ni kusambaa kwa vimelea hivi sugu katika maeneo mengine ya dunia, Afrika ikiwemo kama ilivyokuwa kwa vimelea sugu vilivyokuwa vinatibika kwa dawa kama Chloroquine na SP katika miaka ya nyuma.
Ikumbukwe kuwa watu zaidi ya milioni 219 waliugua malaria katika mwaka 2010 duniani kote, kati ya hao watu 660,000 walifariki na asilimia 90 ya vifo hivyo vilitokea katika nchi za Afrika.

Link: http://www.nature.com/ng/journal/vaop/ncurrent/full/ng.2624.html
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…