Ingekuwa kuna huo upuuzi wa damu ya lulu basi tungesikia watoto wa Mandiba wanashika nchi. Wake zake, Winnie na Graca, ni wanamapinduzi waliokuwa mstari wa mbele wakati wa mapambano ndio maana wanaenziwa. Maria alikuwa mke wa nyumbani na hakuwa mstari wa mbele katika mapambano ya aina yeyote. Thabo Mbeki, mtoto wa Govan Mbeki, hakurithishwa kwa vile alikuwa na damu ya lulu. La hasha, alikuwa mpambanaji mwenzao lakini wenzake walipoona anapoteza dira hawakuchelea kumtema! Sasa nyinyi leo mnataka kumfananisha Makongoro na Julius? Kwa kitu gani alichofanya Makongoro! Kama mnataka kuwaenzi, watawazeni uchifu kama wanavyofanya wanyakyusa na hakuna atakayewaingilia. Lakini hili la kutaka kutufanya wote wajinga kwa vile mnataka kujibalaghua kwa jamaa zenu hatutakubali.
Msivyo na haya mnataka kutuambia kuwa Mrema alivuruga NCCR Mageuzi kwa kumuogopa Makongoro! Makongoro huyu tunayemjua? Yeye mwenyewe atawashangaa sana akiwasikia kuwa mnamfananisha na baba yake labda awe amebadilika siku hizi. Watu kama nyie ndiyo mliofanya wapuuzi wengine kwenye huo ukoo, kuudhalilisha kwa kudai kuwa wametelekezwa! Narudia tena, hapa si Korea ya Kaskazini. Tunathamini vitendo kuliko jina.
Amandla.......