Elections 2010 Vincent Nyerere... Leticia Nyerere... Fumbo kwa CHADEMA

Kama hakuna, basi tulia tuwaenzi watoto wa waanzilishi wa Tanzania.

Kwa kujali zaidi asili ya mtu kuliko uwezo wake, naona mpo radhi ata kutawaliwa na mataahira kwa sababu tu wana damu za viongozi wenu wa zamani.
 
Du...Hivi hawa wana uhusiano wa damu na Mwalimu Nyerere? Kifalsafa je?

Kwa kuwa wana damu ya Nyerere, hawa ni wabarikiwa wa nchi hii, hayo mengine yote sio muhimu....; mtazamo wa ajabu sana huu.
 
Ingekuwa kuna huo upuuzi wa damu ya lulu basi tungesikia watoto wa Mandiba wanashika nchi. Wake zake, Winnie na Graca, ni wanamapinduzi waliokuwa mstari wa mbele wakati wa mapambano ndio maana wanaenziwa. Maria alikuwa mke wa nyumbani na hakuwa mstari wa mbele katika mapambano ya aina yeyote. Thabo Mbeki, mtoto wa Govan Mbeki, hakurithishwa kwa vile alikuwa na damu ya lulu. La hasha, alikuwa mpambanaji mwenzao lakini wenzake walipoona anapoteza dira hawakuchelea kumtema! Sasa nyinyi leo mnataka kumfananisha Makongoro na Julius? Kwa kitu gani alichofanya Makongoro! Kama mnataka kuwaenzi, watawazeni uchifu kama wanavyofanya wanyakyusa na hakuna atakayewaingilia. Lakini hili la kutaka kutufanya wote wajinga kwa vile mnataka kujibalaghua kwa jamaa zenu hatutakubali.

Msivyo na haya mnataka kutuambia kuwa Mrema alivuruga NCCR Mageuzi kwa kumuogopa Makongoro! Makongoro huyu tunayemjua? Yeye mwenyewe atawashangaa sana akiwasikia kuwa mnamfananisha na baba yake labda awe amebadilika siku hizi. Watu kama nyie ndiyo mliofanya wapuuzi wengine kwenye huo ukoo, kuudhalilisha kwa kudai kuwa wametelekezwa! Narudia tena, hapa si Korea ya Kaskazini. Tunathamini vitendo kuliko jina.

Amandla.......
 
..jamani tusimuingize Mama Maria kwenye hili sokomoko la siasa za Tanzania.

..binafsi nasikitishwa sana watu wanaojitafutia uhalali wa kisiasa kupitia heshima na nafasi aliyonayo Mama Maria Nyerere.
 
..jamani tusimuingize Mama Maria kwenye hili sokomoko la siasa za Tanzania.

..binafsi nasikitishwa sana watu wanaojitafutia uhalali wa kisiasa kupitia heshima na nafasi aliyonayo Mama Maria Nyerere.

Mimi kwa kusema kuwa alikuwa mke wa nyumbani sina maana kuwa hastahili heshima. La, hasha. Waliooa watatueleza umuhimu wa mke katika mafanikio ya mume. Ninachokataa ni wale ambao wanataka kumfanya sawa na Mwalimu katika mchango kitaifa. Aheshimiwe katika nafasi yake ( ambayo ni kubwa mno) lakini wasitake kumtumia kwa ajili ya ajenda zao za kisiasa. Heshima haiko kwenye siasa peke yake.

Amandla........
 

Jina lako linajieleza nini unaweza kufanya, wewe ni wa kuambia fanya hivi, huwezi kuwaza kwa kujitegemea na umechagua cheo kizuri kinachokufaa, "Fundi Mchundo". Chambua mambo akilini kwako acha kufuata unayoambiwa hata kama ni mabaya.
 

Fundi Mchundo,

..tuko pamoja 100%.

..mama wa watu hakujihusisha na siasa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

..nachukizwa sana na hizi harakati za CCM kujaribu kumtumia kujijengea uhalali mbele ya wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…