Vinywaji feki vya Highlife maeneo ya Moshi vyatishia kampuni ya Derick Global Trading

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
Kuna wimbi kubwa la usambazwaji na uuzwaji wa vinywaji feki vya Highlife katika maeneo mbalimbali ya mji wa moshi unaofanywa na wafanyabiashara wasiowaaminifu.

Hatua hiyo inatishia uzalishaji na uuzwaji wa Highlife halisi inayozalishwa na kampuni ya mwekezaji mzawa, Willy Lucas Tarimo mkurugenzi wa Kampuni ya Derick Global Trading Co.Ltd.

Kinachofanywa na watu hao ni kuajili vijana wengi ambao jukumu lao ni kuzunguka kwenye maeneo kunakouzwa bidhaa hiyo na kukusanya chupa za kampuni hiyo na kuzipeleka kwa wahusika ambako huzitumia kuweka pombe zosizokuwa na ubora na kuziweka kwenue chupa hizo.

Tayari kampuni hiyo kwa kushirikiana na vyombo vya Dola wameanza msako wa kuwakamata baadhi ya watuhumiwa hii na Kwa mujibu wa uongozi wa kampuni hiyo.

Kampuni hiyo imetoa rai kwa wateja wake kuwa macho na vinywaji hivyo feki na kuomba kutoa ushirikiano wa kuwafichua wale wote wanafanya hujuma hizo.

Kina nani wanahusika na wako wapi ni hapo baadae.
 
maeneo yanayoongoza kwa hivi viwanda bubu vya kuchakachua ni Njoro.
 
Konyagi na Valuer waliwahi kupata hiyo changamoto ila wakaiwahi kwa kuongeza ulinzi na kubadili vingi kwenye vifungashio
 
Hivi vinywaji vywa plastic namaanisha pombe za plastic zinawamaliza vijana kwakweli
 
Kuna wimbi kubwa la usambazwaji na uuzwaji wa vinywaji feki vya Highlife katika maeneo mbalimbali ya mji wa moshi unaofanywa na wafanyabiashara wasiowaaminifu.

Hatua hiyo inatishia uzalishaji na uuzwaji wa Highlife halisi inayozalishwa na kampuni ya mwekezaji mzawa, Willy Lucas Tarimo mkurugenzi wa Kampuni ya Derick Global Trading Co.Ltd.

Kinachofanywa na watu hao ni kuajili vijana wengi ambao jukumu lao ni kuzunguka kwenye maeneo kunakouzwa bidhaa hiyo na kukusanya chupa za kampuni hiyo na kuzipeleka kwa wahusika ambako huzitumia kuweka pombe zosizokuwa na ubora na kuziweka kwenue chupa hizo.

Tayari kampuni hiyo kwa kushirikiana na vyombo vya Dola wameanza msako wa kuwakamata baadhi ya watuhumiwa hii na Kwa mujibu wa uongozi wa kampuni hiyo.

Kampuni hiyo imetoa rai kwa wateja wake kuwa macho na vinywaji hivyo feki na kuomba kutoa ushirikiano wa kuwafichua wale wote wanafanya hujuma hizo.

Kina nani wanahusika na wako wapi ni hapo baadae.
Kuna wakati Willy aliiba tiper mpya ya baba yake,akaiuza Zambia! Ni willy huyu au ni mwingine?
 
Back
Top Bottom