VIOJA Bungeni No.1

VIOJA Bungeni No.1

Nadhani hii nchi inahitaji mtawala dictator kama Joseph Stalin ili awachinje mataahira wote. Wananchi wengine wanaobaki wanolewe kwa uzalendo na maadili. Tofauti na hapo ni upunguani mtupu!

Joseph Stalin hayupo duniani. Na wewe n tahaira unayetakiwa kuchinjwa?
Tahaira n mtu wa aina gani?
Stalin alikuwa Juha kuwachinja matahaira.
 
inasikitisha sana au ndo staili ya kuongeza siku maana wanatumia muda mwingi kuchambana
 
mkuu hii nani aliitapika!

Hii ilitoka mdomoni mwa mwanaume mmoja ambaye alijitambulisha kwamba ni sheikh. Ni maoni ambayo hayakuhitajika kabisa maana alistahili kujiuliza miaka yote ya uhuru, akina mama huapishwa namna gani. Ajabu kabisa alishangiliwa sana! Na nadhani kwa kutozoea kushangiliwa akaongeza manjonjo!
 
Mkuu Mchunguzi hiyo ya mwisho ni siriaz au unatania?ni kijana gani huyo?

Siriasi!! Tena hii ilitoka kwa kijana mmoja nadhani akiwakilisha makundi maalumu. Mkongwe mmoja akajibu kwamba hata yeye kijana angeweza kutangulia na kuwaacha wazee wakiwa hai!
 
ama! kwa kweli hawa magamba wamechoka kufikiri, au ndio wanafikiri kwa kutumia ma**lio?
 
Umesahau hii...'mwenyekiti ahirisha tuondoka'. Wako mle kula mshiko na sio vinginevyo.
 
Jana nilikuwa nasikiliza bunge maalum la katiba kwa mara ya kwanza ilikuwa jioni TBC inaonyesha mie moyo unanienda mbio naangalia uku naona aibu, matusi yataporomoshwa sasa hivi mara naangalia kidogo mara narudisha mambo yalivyokuwa kwani vipaza sauti vya wajumbe wote viko on kila mbunge anaongea story yake wengine habari za mnadani ilivyokuwa, wengine anasifia watoto wake uku vinaingiliana kwenye speak hadi huku kwenye tv tunasikia ilikuwa kama kilabuni walevi wakilewa hawana discipline kubwa zaidi ya yote kuna mbaba mmoja alikuwa anachangia mara mama moja bila ya aibu akanyanyua kipaza uko aliko akawa anasema tumekuchoka !!!! mara kwa mara sauti inajirudia yaani vituko mara ii mmeshachokana !!!! 2 weeks.Yaan wako kama wehu, sura zao zimekosa aibu, unaweza ukawa hauna uzalendo mungu akakupa aibu, vyote hawana, kwani kule bungeni kunamitambo sijui ya kuwakata watu fluzi, mbona wengi wamevurugwa nashindwa kupata jibu.Ninyamaze nisije kupata ban
 
Haya ndo baadhi ya maoni ya baadhi ya hawa wabunge wa Bunge maalumu la katiba. Michango ni mibovu na mingine haina umuhimu kabisa, lugha mbaya na wakati mwingine bila staha, lakini wao wanasema wana kazi muhimu sana!

"...Mheshimiwa mwenyekiti, nchi zote hizo zilizotolewa mfano kwamba ni za kidemokrasia zinaruhsu ushoga na usagaji, hatutakubali kuiga watuwanofanya mambo kama hayo ruksa!!"

"…Mheshimiwa mwenyekiti kuruhusu kura ya siri ni sawa na mtu anayeingia kichakani kujisaidia, macho anageuzia barabarani kwenye watu, ------ anayageuzia porini kwenye simba!!!"

"...Mheshimiwa mwenyekiti huyu Sendeka hajui Kiingereza…. Arudi akajifunze upya."

"...Mheshimiwa mwenyekiti, wanawake wa kiislam wakiwa kwenye zile siku zao mbaya dini inawakataza kushika msahafu, hivyo tunaomba basi iwekwe namna ya kuwaapisha bila kushika msahafu!!... na wanaume wa kiislamu lazima wawe na udhu …"

"...Mheshimiwa mwenyekiti .... na tuendelee kudai ongezeko la posho mpaka kieleweke ...."

"...Mheshimiwa mwenyekiti sisi vijana lazima tusimame imara na kwa uwazi kwa kupiga kura ya wazi kwa sababu katiba inayotengenezwa ni yetu sisi vijana, nyie mazee wote mtakuwa mmeshakufa!!"
MchunguZI ...asante sana kwa kutuonyesha ni wajumbe wa aina gani tulionao katika hili bunge maalumu la katiba. Ingekuwa vizuri zaidi kama ungetuwekea na majina ya hao waheshimiwa katika hizo nukuu!
 
Last edited by a moderator:
Mtikila aliyasema mapemaaa..
"hili bunge ni la kihunihuni bcoz limechaguliwa kihuni" sasa ukweli umedhihirika. Aibu ye2 waTZ.
 
Kinachosikitisha ni hawa wabunge wazoefu ambao wameonekana kuongoza kwa kutoa matusi kuliko hawa wengine walioingia kwa makundi yao.

Naona kama hawa jamaa wanajifanya ni wenyeji ktk jengo hilo na wanajua kuwasha na kuzima mic., kwao hilo laonekana ni elimu kubwa! Lugha mbaya, hakuna umakini ktk uchaguzi wa manneo ya kutumia.
 
Back
Top Bottom