Vioja gani ulifanya kipindi umeanza starehe ya pombe

Vioja gani ulifanya kipindi umeanza starehe ya pombe

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
Habari za mwisho wa weekend wanajamii.

Naamini kila kila mtu ana aina yake ya starehe,lakini hapa nimejikita zaidi kwenye starehe yenye kuhusisha Pombe.

Je,kwa Mara ya kwanza ulivyotumia ilikuwaje/ ulifanya kioja gani?

Kwangu
1. Mwaka Mpya Arusha 2018,
Mimi na jamaa yangu tukaenda kupata mlo nyumba kwa mshkaji wetu,tulikutana watu kama 15 hivi.

Nyama Choma kama zote, kwenye vinywaji ni,Kvant, Jägermeister, Jack Daniel's na Whisky ya kirusi (sikumbuki jina).

Nkasema ngoja nijaribu, nlipiga Jägermeister+apple punch glass 4 yakanizidia. Nikaanza mlilia mjamaa tuondoke, nilimsumbua mpaka akakubali. Ndiyo kwanza saa 11 jioni

Sasa ile kuinuka tu na kuanza kutembea, nilipiga hatua za nne za faster kwenda kushoto na kulia kama nakamata panzi, mara pu chini.

Mjamaa akanisaidia mpaka kwenye gari, akafungua mlango wa nyuma Mimi nikajitupa kwa kulala, mjamaa akafunga mlango na kurudi kula gambe.

Baadaye nikaskia mlango kama kufunguliwa baadaye kumuuliza kama tumefika, akasema alikuwa anajaza mafuta, nikalala tena. Saa 6 usiku.

Kufika home: Nikajitupa tu, kuamka asubuhi, Nimelala sakafuni sebreni.
 
2.Dar 2017,
Inamhusu mjamaa wangu C
Tulikutana washkaji pale kwenye pub ya Coco Beach...ndyo kwanza tumetoka maliza vyuo.
Imeagizwa Koka(for me )+ soda water + Konyagi bapa mbili ,
Wanawashaanza kunywa gambe mi nipo na koka.
Mchizi P ndiyo wa mwisho kufika,,bwana akaona apige Konyagi ili asionekane mshamba.

Sasa C akawa anagigida Nyagi kavu, halafu mwana mmoja akawa anampa bichwa eti "Nyie familia yenu hamnaga vichwa vya kulewa"

Mjamaa alikata nusu mzinga,,vioja vikaanza
  • Kila akiongea lazima aweke tusi la kiingereza
  • Anafoka bila sababu
  • Analia
Wana wakasema wabdili kijiwe na kwenda Sinza.
  • Yeye ile kuinuka mtihani
  • Itabidi nichukue boda kumpeleka kwao,ile kufika Msasani magunia
  • Mwamba kaanguka chini, Kiatu kuvuka
  • Kuinuka mtihani
  • Kuvaa kiatu nusu nzima anahangaika mpaka kakichana
  • Umati unatuangalia sie
  • Kumfikisha kwai,kesho yake napigiwa simu naambiwa mtu karudisha chenchi kama yote.
 
3.Dar,2017
Ina mhusu mchizi K
Weekend tupo Bar flan maeneo ya Sinza,Washkaji kama watano
  • Mchizi K ana stress za kutemwa na manzi yake
  • Gambe zilipokolea,mchizi K akaanza kulia kisa kutemwa,tena analia kwa kizungu,,oh "why you left me"
  • Ikafika saa 7 tukasema tuondoke,mana na mchizi akaanza na fujo.
  • Tupo getini mchizi K akataka kugombana na Baunsa,akambwa kofi 2,kanyamaza kimya,tukaondoka
 
Habari za mwisho wa weekend wanajamii.

Naamini kila kila mtu ana aina yake ya starehe,lakini hapa nimejikita zaidi kwenye starehe yenye kuhusisha Pombe.

Je,kwa Mara ya kwanza ulivyotumia ilikuwaje/ ulifanya kioja gani?

Kwangu
1. Mwaka Mpya Arusha 2018,
Mimi na jamaa yangu tukaenda kupata mlo nyumba kwa mshkaji wetu,tulikutana watu kama 15 hivi.

Nyama Choma kama zote, kwenye vinywaji ni,Kvant, Jägermeister, Jack Daniel's na Whisky ya kirusi (sikumbuki jina).

Nkasema ngoja nijaribu, nlipiga Jägermeister+apple punch glass 4 yakanizidia. Nikaanza mlilia mjamaa tuondoke, nilimsumbua mpaka akakubali. Ndiyo kwanza saa 11 jioni

Sasa ile kuinuka tu na kuanza kutembea, nilipiga hatua za nne za faster kwenda kushoto na kulia kama nakamata panzi, mara pu chini.

Mjamaa akanisaidia mpaka kwenye gari, akafungua mlango wa nyuma Mimi nikajitupa kwa kulala, mjamaa akafunga mlango na kurudi kula gambe.

Baadaye nikaskia mlango kama kufunguliwa baadaye kumuuliza kama tumefika, akasema alikuwa anajaza mafuta, nikalala tena. Saa 6 usiku.

Kufika home: Nikajitupa tu, kuamka asubuhi, Nimelala sakafuni sebreni.
Mkuu ulijikagua vizuri huko nyuma?
 
Back
Top Bottom