Vioja vya majibu ya barua ya posa 'UZARAMONI'

Vioja vya majibu ya barua ya posa 'UZARAMONI'

ila mkuu ujue jamaa lazima atapata waume wenza!wanawake wa kizaramo kugongwa nje ni jadi pia ruhusa za kutoka kila siku
 
kwani gharama zikiwa kubwa ni ujanja?
unaweza oa mke wa mamiliono kumbe kicheche full
na mwingine akaoa kwa elfu kumi tu
na akapata mke wa kweli..

Naungana na wewe mkuu,
Kuwa na tabia mbaya ni hulka ya mtu na sio na haihusiani kivyovyote na Kabila lake, Kwa mfano sisi kwetu Mtwara gharama za kuoa ni za chini sana hasa sehemu kama Masasi ambako wayao ni wengi.

Nakumbuka kaka yangu alitoa alitakiwa kulipa mahari 45,000 lakini alitoa 15,000 na akaondoka na jiko lake kama kawaida na mpaka naandika post hii bado wapo pamoja na wana watoto na ndoa yao ni mfano mmojawapo wa kuigwa katika jamii kwani hawana mitafaruku ya aina yeyote ile.
 
ila mkuu ujue jamaa lazima atapata waume wenza!wanawake wa kizaramo kugongwa nje ni jadi pia ruhusa za kutoka kila siku

Una uhakika???!! Vipi wale wanaokatazwa kuwaingilia wake zao hadi watu wengine wawaingilie pindi wanapowaoa!! Hiyo nayo ni mila nzuri??
 
Ha! Mtwara na Lindi mpaka 50,000 unaweza kupata jiko.

Hhahahahahaahahahaha, mkuu hico kiwango ulichotaja kikubwa sana, me nakumbuka kaka alioa kwa Tsh 15,000 tu na akaondoka na jiko lake. Mpaka leo wapo pamoja na ndoa yao ina furaha sana.

Muda mwingine huwa sioni mantiki ya kutoa mahari nyingi wakati kuna sehemu kama hizi ambazo unaweza kupata jiko kwa bei ya chee kabisa, kwa jinsi inavyoelekea, wazaramo,wayao,wamatumbi, wakwere, wandengereko ndio watakaokuwa wa kwanza kuachana na hii tabia ya kuuza watoto wa kike kwa wanaume.
 
Mwaka 2000, jamaa yangu alitozwa mahari ya Tsh 7000/= akajipatia jiko la binti wa Kizaramo...................


Kuna jamaa alitegeshewa ndoa ya mkeka basi yeye akamwona binti anaingia chumbani kwake na kanga moja akafikiri amepata kumbe alikuwa amepatikana. Hajakaa sawa shehe huyo na Mkeka (Shehe mjomba wa Binti) Basi majadiliano ya hapa na pale ikawa kwamba ama polisi (under 18) ama ndoa jamaa akaona heri ndoa. Basi akahesabiwa kila kitu jumla 70,000/=. Jamaa akaruka kuwa hiyo ni bei kubwa kwa binti kama yule, mzee akatumia busara kuwa wote wawili wana makosa hivyo yeye alipe 35,000/= na binti 35,000/=. Jamaa akadai hata hiyo hana basi akaambiwa una bei gani akasema 20,000/= wakasema leta hiyo 15 elfu deni. Sijui kama alimaliza maana ndoa haikuchukua duru ( Hii ilitokea maeneo ya Kimara Baruti mwaka 1994)
 
Back
Top Bottom