ng'adi lawi
JF-Expert Member
- Sep 27, 2014
- 2,956
- 1,114
Jamani mimi huwa nawashangaa viongozi wafugaji hasa wa kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa. Enzi za mwalimu kulikuwa na viwanda vya nyama, viwanda vya maziwa na viwanda vya ngozi na viwanda vya viatu ambavyo vilikuwa vya umma. Vyote vimeuzwa au kufilisika na kubaki magofu lakini mifugo tunayo tena mingi na inaharibu mazingira. Kwa nini akina Lowasa, OLe Sendeka, Lekule Laizer na wengineo ambao ni wafugaji wasiwekeze kwa kuanzisha viwanda vyao kwa kupunguza idadi ya mifugo ni kuigeuza mitaji badala kutafuta wawekezaji kutoka nje ya nchi?
Nakumbuka hata wakati wa ukoloni kulikuwa na mkakati wa kupunguza mifugo kwa amri ya serikali (de-stocking).
Wakifanya hivyo mazingira yetu yatanufaika na migogoro na na wakulima na hifadhi zetu itapungua au kwisha kabisa. Pia vijana wetu watapata ajira.!
Mheshimiwa Saning'o ole Telele naibu waziri wa mifugo na uvuvi kazi kwako!