Viongozi ambao ni wafugaji wawekeze kwenye viwanda vya mazao ya mifugo

Viongozi ambao ni wafugaji wawekeze kwenye viwanda vya mazao ya mifugo

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
2,956
Reaction score
1,114
Jamani mimi huwa nawashangaa viongozi wafugaji hasa wa kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa. Enzi za mwalimu kulikuwa na viwanda vya nyama, viwanda vya maziwa na viwanda vya ngozi na viwanda vya viatu ambavyo vilikuwa vya umma. Vyote vimeuzwa au kufilisika na kubaki magofu lakini mifugo tunayo tena mingi na inaharibu mazingira. Kwa nini akina Lowasa, OLe Sendeka, Lekule Laizer na wengineo ambao ni wafugaji wasiwekeze kwa kuanzisha viwanda vyao kwa kupunguza idadi ya mifugo ni kuigeuza mitaji badala kutafuta wawekezaji kutoka nje ya nchi?

Nakumbuka hata wakati wa ukoloni kulikuwa na mkakati wa kupunguza mifugo kwa amri ya serikali (de-stocking).

Wakifanya hivyo mazingira yetu yatanufaika na migogoro na na wakulima na hifadhi zetu itapungua au kwisha kabisa. Pia vijana wetu watapata ajira.!

Mheshimiwa Saning'o ole Telele naibu waziri wa mifugo na uvuvi kazi kwako!
 
Wakiwekeza wataambiwa ni mafisadi, wamepata wapi hela. Hivyo wanaona tu bora wafiche hela kwenye viroba wawe wanakula taratibu taratibu.
 
Hawawezi kuitwa mafisadi kwani tayari wanayo mifugo mingi na kwa taarifa yako kati ya hao niliowataja hakuna ambaye ana ngombe, mbuzi, kondoo, punda n.k. chini ya 2000 kila mmoja. wanatakiwa kuuza na kubaki na wachache ili wapate fedha za kununua mitambo. kwa hiyo tayari wanayo mitaji na wanahitaji tu wataalamu wa kuingia nao ubia!
 
Back
Top Bottom