Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Napenda kuomba radhi mwanzoni kitu nilichokuwa nimedhamiria hakikuweza kuwafikia kama nilivyotaka badala yake yalitokea maandishi mafupi tu, yasiyo na tafakuri yeyote. Hata hivyo hii hapa chini ndio tafakuri yangu na linki ya audio kutoka Youtube ipo hapo.
Kumekuwepo na mjadala mpana sana kuhusu ni nini Afrika wanahitaji kati ya viongozi imara na taasisi imara. Mjadala huu umekuja haswa mara tu ya aliyekuwa raisi wa marekani kuongea yakuwa:: Kwamba afrika haihitaji strong leaders bali strong institutions ili iendelee. Kwa siku za hivi karibuni mjadala huu umechagizwa zaidi na aliyekuwa Mkaguzi muu wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kusema neno kama hilo akimnukuu tajiri mmoja wa kimarekani aitwaye Buffet.
Napenda kutofautiana kidogo na watu wanaosema afrika haihitaji strong leaders bali strong institution. Vitu hivi viwili vinahusiano wa karibu sana. Huwezi kuwa na taasisi imara kama huna viongozi imara. Tunamahitaji makubwa mno ya viongozi imara. Na sio viongozi imara pekee, bali viongozi wenye maono, hekima na busara kuweza kujenga na kusimamia taasisi hizi. Tunapozungumza viongozi imara hatuzungumzii viongozi wabinafsi, madikteta na wanao kandamiza na kuonea watu. Bali viongozi ambao wako pale kwaajili ya kuhudumia watu na sio tyrants. Kwakuwa tyrants wakishika nchi wanatenda kwaaajili ya manufaa yao na sio kwa manufaa ya taifa. Kwahiyo ninapozungumzia strong leader sizungumzii tyrant bali yule ambaye yuko kwa maslahi ya wananchi na ambaye anayalinda na kuyatetea kwa nguvu zake zote.
Na wale tusujidanganye taifa likiwa na viongozi weak na wasio na maarifa na busara ya kutosha nchi na taasisi zitakuwa hivyo hivyo. Kwahiyo tunahitaji kiongozi ambaye ata elevate na kuwaempower watu na kuwa raise their consciousness kwa utaifa na uwajibikaji. Kwahiyo kiongozi imara hatotaka watu wake wawe dhaifu, atataka wawe kama yeye alivyo ili wa serve nchi yao vyema.
Na wala sizungumzii kiongozi ambaye anataka kuonekana yeye tu, bal ikiongozi ambaye atajenga mfumo imara na kujenga pia watu wake kuwa bora ili waendeshe taasisi hizo pia ziwe bora na ziishi kwa muda mrefu. Kwakuwa taasisi nazo zinakufaga na zinategemea ubora wa watu walionao ili zi serve watu vyema, Na watu wanapokuwa corrupt na taasisi pia zinakuwa corrupt. Taasisi zinategemea watu moja kwa moja. Ubora wa watu ndio ubora wa taasisi. Kwahiyo kiongozi imara lazima awekeze kwa watu na anafahamu huwezi kubadilisha nchi pasipo kuwekeza kwa watu na kuwafanya watu kuwa bora. Kwahiyo anajua nguvu yake na ya taifa lake inategemea ubora wa watu wake. Ni tyrant pekee anataka watu wake wawe weak na yeye awe Strong ili aendelee kuwanyonya. Na tryant sio lazima awe mtu kinaweza kuwa chama. Lakini a strong leader Nguvu yake iko kwa wananchi na mipaka ya nguvu yake haishii kwenye nchi yake pekee husambaa kwasababu nguvu yake hategemei jeshi lake pekee bali pia umma.
Tabia za wananchi katika nchi husika huonyesha dira ya taifa hilo ikoje. Na hiki ndicho kiongozi imara anatakiwa ajenge na taasisi za nchi hutegemea sana kuhusu hilo. Miongoni mwa tabia hizo bora ni nidhamu na kupenda kufanya kazi. Kunapopungikiwa na nidhamu katika nchi maendeleo huwa shida na kunakuwepo hakuna kusikilizana na hata uongozi unakuwa shida na hivyo taifa hukosa dira. KIla mtu atakuwa mkuu, kila mtu mjuzi, watu wataongea bila kufikiri na wala kujali impact ya maneno yao na order katika nchi huwa ndogo.
Barack obama anasahau kwamba waliojenga Marekani hawakuwa watu dhaifu naongelea their founding fathers. Walikuwa ni watu wenye busara na nguvu. Vitu viwili muhimu kwa kiongozi. Kwasababu nguvu lazima iwe regulate by wisdom ile iwe efficiency. Tujue kwamba taasisi haziwezi kujiendesha zenyewe lazima ziendeshwe na watu na inategemea sana watu hao wana maarifa na busara kiasi gani ili taasisi hizo ziendelee kudumu and if they are fool hata watengeneze sheria nzuri kiasi gani na taratibu haziwezi kuwasaidia. Kwahiyo kama tuna problem katika Afrika problem ni sisi wenyewe let us eveluate ourselves. Ni ujinga kusema tunahitaji taasisi imara kama vile zitajiendesha zenyewe na sisi tutasimama kufikiri huku taasisi zikifikiri kwa niaba yetu. Taasisi zinatutegemea sisi kuziendesha zitakuwa bota kama sisi ni bora. Zinahitaji busara na hekima zetu ili ziendelee. Sisi ndio wenye matatizo na cha ajabu hatutaki kujichunguza sisi watu tukibadilika tutabadilisha kila kitu.

Last edited: