Viongozi kama Waziri Mwigulu hawahusiki kabisa na tozo zote, tunalipa sisi walalahoi

Viongozi kama Waziri Mwigulu hawahusiki kabisa na tozo zote, tunalipa sisi walalahoi

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Ninatoa mfano wa Dr Mwigulu akiwawakilisha Mawaziri na Viongozi wote wa Serikali, hasa wale wateule wa Rais.
Pakikucha Dr. Mwigulu anakuta nje gari la Ofisi limepaki anachukuliwa na dreva - gari limejazwa mafuta na Ofisi, so kwa kuwa hatumii gari lake basi tozo ya mafuta haipo tena. Hili linagusa watoto wake pia ambao ama wanabebwa na gari la ofisi au wapo Boarding. Gari hili pia hutuimka hata kwa safari za binafsi anapokuwa anaenda kijijijini kwao kule Makunda Iramba au pale kwenye nyumba yake Ulemo.

Mshahara wa Dr. Mwigulu na maruprupu mengine yanaingia moja kwa moja kwenye akaunti yake. Hivyo akienda Benki anaenda moja kwa moja kaunta ya bulk cash anahudumiwa hapo au mara chache anatoa fedha kwenye ATM. Ni nadra sana Dr. Mwigulu, mawaziri na hata wabunge kuwaona wanafanya transactions kwenye mobile money shops. Akitaka kuwatumia ndugu zake ama ataingia moja kwa moja kwenye akaunti ya benki na kurusha huko huko au atamtuma dreva au msaidizi wake akawatumie. Ndugu zake waliopo kijijini labda ndiyo wataguswa na tozo hizo kwa sababu yeye alywas atakuwa ni mtu wa kuweka tu na wala sio wa kutoa. Hata anapolipwa posho zingine na Taasisi za chini yake hazitumwi kwenye simu - sana sana anapewa cash kupitia wasaidizi wake au anatumiwa kwenye akaunti yake.

Kuhusu kodi ya ardhi - ukweli hiyo wala sio kodi ya nyumba bali ni kodi ya mpangaji au "household tax". Ni ngumu Mwigulu kuishi nyumba ya kupanga - sana sana anaishi nyumba ya Serikali au amejenga yeye. Vyotevyote kumbuka kuwa Waziri na Viongozi wengine wote wanalipwa posho ya "utility" yaani umeme na maji kila mwezi. So wao wakinunua umeme wanatumia mihela ya Serikali ambazo ni kodi zetu. Wakubwa wengi ni nadra sana kushi nyumba za kupanga - wanaishi nyumba zao na zingine wanapangisha kwa walipa kodi ya pango.

Kwa cycle hiyo watu kama akina Dr Mwigulu hawawezi kamwe kuona machungu ya walalahoi kama sisi kwa kodi wanazotupangia. Kodi zote hizo zinalipwa na watu wa chini - wanunuzi wa mafuta ya magari ni wale watu wa kawaida tu may be na wafanyabiasahara, na sio viongozi. Ukija miamala ya kwenye simu inafanywa na watu wa chini amabao majority ni wafanyakazi wa chini na wakulima - viongozi wao mihela yao ni kwenye akaunti za benki na kulipwa cash kupitia kwa wasaidizi wao. Kodi ya ardhi - inalipwa na wapangaji ambao wengi ni wafanyakazi wa chini wasiliolipwa allowanace ya utility na wala hawana nyumba zao binafsi.

WaTanzania tumelela sana - ndiyo maana Mbunge mmoja katoa wazo la wao kukatwa kodi ameitwa kwenda kuadabishwa! Kazi kweli kweli!
 
Aliyemteua huyu jamaa kwenye hiyo nafasi, alipuyanga kweli kweli! Maana mpaka atakapo ondoka kwenye hiyo Wizara, atakua ametuvuruga siyo kidogo!
 
Aliyemteua huyu jamaa kwenye hiyo nafasi, alipuyanga kweli kweli! Maana mpaka atakapo ondoka kwenye hiyo Wizara, atakua ametuvuruga siyo kidogo!
DR MPANGO NDO ALIKUWA WAZIR WA MAANA KUTOKEA, WENGINE VILZA TU
 
DR MPANGO NDO ALIKUWA WAZIR WA MAANA KUTOKEA, WENGINE VILZA TU
Mpango ndiye aliyeandaa bajeti hii yenye tozo. Kwasabb mchakato wa kuandaa bajeti ulianza kabla Mwigulu hajateuliwa.
 
Mpango ndiye aliyeandaa bajeti hii yenye tozo. Kwasabb mchakato wa kuandaa bajeti ulianza kabla Mwigulu hajateuliwa.
Hizi tozo ni za Mwigulu! Tena ni baada ya kudesa mawazo ya Zungu na ya baadhi ya Wana JF humu jukwaani, na pasipo kuyafanyia utafiti wa kina. Mpango asingekuja na Bajeti ya hovyo kama hii!

Ushahidi ni miaka yote aliyo hudumu kama Waziri wa Fedha na Mipango, bajeti yake mara zote iliuma na kupulizia! Ila hii bajeti ya Mwigulu Nchemba, kuanzia mwanzo mpaka mwisho inauma tu!
 
kwa sababu wananchi wametaka wenyewe. uoga.. unafki tamaa.. hiv ndivyo vina define jamii yetu
Alafu unashangaa WANYONGE wanalialia kwa tozo kidogo hivi,mbona walisema wapinzani walituchelewesha Sana kupata maendeleo,Sasa tuna Bunge la kijani linatuletea maendeleo kwa kasi.
 
Alafu unashangaa WANYONGE wanalialia kwa tozo kidogo hivi,mbona walisema wapinzani walituchelewesha Sana kupata maendeleo,Sasa tuna Bunge la kijani linatuletea maendeleo kwa kasi.
Umaskin wetu una relate na tabia za jamii yetu. tume inherit UWOGA kias kwamba tumeubadilisha jina tunauita utii. ndio hapo ccm wanajipenyeza..
na hiii haitoisha mpaka jamii iamke
 
Umaskin wetu una relate na tabia za jamii yetu. tume inherit UWOGA kias kwamba tumeubadilisha jina tunauita utii. ndio hapo ccm wanajipenyeza..
na hiii haitoisha mpaka jamii iamke
Hata wale wapinzani ambao walikuwa tegemeo kipindi cha JPM wamenunuliwa ili kuwanyonya wengine.
 
Nhh.... Sasa tufanyeje Mkuu...
Tuelimishe jamii yetu ijitambue! Sivyo tuache kulalamika pale tunapohongwa wakati wa Uchaguzi halafu tunarudisha hongo hiyo baada ya Uchaguzi!
 
Back
Top Bottom