HAKI KWA WOTE
JF-Expert Member
- Nov 30, 2022
- 1,108
- 1,132
Habarini,
Mimi bado siamini ktk biblia na msahafu hasa katika kuijenga AFRIKA. Kumekuwa na taratibu za viongozi wa Afrika kuapishwa kwa kushika biblia na msahafu lakini wakawa wezi,mafisadi na wahujumu uchumi pasipo kudhurika wala kuogopa.
Nimekuwa nikiona baadhi ya jamii za kiafrika wakiapishana kwa mila zao za Kiafrika na kuwa watiifu na waaminifu kuliko hawa wanaoapa kwa vitabu vya kuja na ikitokea kuna tatizo wazee walifunga na kuomba ktk mila zao kupitia mizimu na wale wote walioshiriki kutenda makosa wakaadhibiwa na mizimu kitu ambacho kilijenga heshima na uaminifu kwa viongozi na hata wanajamii husika i.e:-kuvunja chungu kwa Wachaga.
Sasa kwanini viongozi wa Afrika tusianze kuwaapisha kwa MILA ZETU ZA KAFRIKA kupitia wazee ili atakayeiba au kulisaliti Taifa adhulike na ikibidi afe kwani hivi vitabu biblia na msahafu vinawafuga viongozi majizi.
Hata wakiapishwa na vitabu vyao basi pia waapishwe na wazee kwa kuruka chungu tuone atakayeiba au hulihujumu taifa.
Mwl Nyerere wakati anatafuta UHURU wazee walifunga na kumuombea ili wabaya wote wasimkaribie na kumdhuru sasa kwanini hya yasifanyike kwa viongozi ili kuwafunga.
Tutafakari!!!