Viongozi kutopokea simu, nini kifanyike?

Viongozi kutopokea simu, nini kifanyike?

tanzibar

Member
Joined
Aug 27, 2021
Posts
43
Reaction score
71
Kumekuwa na wimbi la viongozi wa umma kutopokea simu zao. Simu za mezani nyingi hazipokelewi na kiganjani pia. Je, Ili kuwepo mawasiliano rahisi kati ya Umma na Viongozi hao, nini kifanyike?
 
Kumekuwa na wimbi la viongozi wa umma kutopokea simu zao. Simu za mezani nyingi hazipokelewi na kiganjani pia. Je, Ili kuwepo mawasiliano rahisi kati ya Umma na Viongozi hao, nini kifanyike?
Nikuwaptezea tu
 
Cha kufanya ni kuwashtaki kwa chakubanga tu maana enzi zile akiwa mwenezi alikua anawapigia cm kwenye tV program yake inaitwaje sijui...nshaisahau ila walikua wanapokea..😎😎
 
Nikuwaptezea tu
mfano: una shida taasisi fulani, halmashauri ama wizara yeyote ile. unaeleza shida yako na kujibiwa kuwa njoo baada ya siku tatu, au wiki. Lakini kwa urahisi wa mawasiliano unaomba namba ya ofisi hiyo husika ili kabla ya kuja ujue wamefikia wapi. unapewa. unarudi mfano km50 au 100 ulizotoka. siku uliyoahidiwa inafika na unapiga simu kwa namba hiyo na haipokelewi!!! kesho yake unafunga safari unaenda tena kwenye ofisi hiyo, ukifika kwanza hata kukusahau wamekusahahu!! pili unaanza kueleza tatizo upya!! tatu unaambiwa njoo tena baada ya wiki!!!!! Kama simu zingefanya kazi ipasavyo zingerahisisha kuondoa usumbufu!!! (NB: huu ni moja ya mifano ya mingi iliyopo ya usumbufu unajiotokeza kwa kutokuwepo kwa urahisi wa mawasiliano)
 
Back
Top Bottom