Viongozi mahiri wa kike kuwahi kutokea Tanzania

Viongozi mahiri wa kike kuwahi kutokea Tanzania

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,412
Reaction score
3,043
Leo tuwakumbuke viongozi mahiri na shupavu kuwahi kutokea Tanzania.

Naanza na Bibi Titi Mohamed, huyu kwangu mimi anabakia kuwa “Iron Lady” mwanamama mahiri zaidi katika ardhi ya Tanzania.

Huyu ni miongoni mwa waliojitoa haswa katika harakati za Uhuru enzi ya TANU. Alikuwa na misimamo haswa.

Huyu aliwahi kula njama za kumpindua Nyerere mwaka 1969 akabainika akafungwa jela maisha na baadae kusamehewa na Rais Mwinyi na kurudi tena katika harakati za siasa mpaka alipofariki dunia mwaka 2001 nadhani.

wewe unamkubali yupi?
 
Hakuna Mwana Mama Na mwanamke Imara kuwahi kutokea katika ardhi na Bara la Afrika wa kufananishwa na Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Huyu mama ni chuma kwelikweli.Ni mtu na Nusu .sina uhakika kama ardhi ya Tanzania na barani Afrika atatokea Mwanamke mwingine jasiri, Shupavu, madhubuti,imara ,hodari na mwenye uwezo mkubwa wa kiuongozi na aliyekamilika kila idara kama alivyo Rais Samia .

Nampa saluti Rais Samia.🙏
 
Umeajiriwa op gani? Afande
 
Back
Top Bottom