mangiTz
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 1,820
- 3,062
Habari wana JF
Moja ya vitu vinaturudisha nyuma ni uwajibikaji wa viongozi katika nafasi zao , waziri mkuu ametembelea miradi ya maendeleo kigoma alivyojionea kama si sheria unatamani umpige mtu lakini hapana huwezi kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa kauli iliyosikika ya PM ni kuwa halimashauri imepokea hela toka 2021 lakini mpaka leo hospitali bado imewekwa msingi tu hakuna kinachoendelea hela zipo kwenye account . Aina ya wasimamizi wa eneo hilo ni dhahiri hawatufai na wanatengeneza sifa mbaya kwa viongozi wa juu kusiko na ulazima kwakuwa miradi ikiwa haiendi wananchi ni kawaida kupeleka lawama ngazi za juu.
Viongozi mlipewa dhamani tekelezeni majukumu yenu wala msitie ugumu katika miradi ya maendeleo huku ni kudhulumu haki za watu. Wengine huzuia pesa au kwa kutumia mamlaka waliyo nayo kukwamisha miradi huo haifai. Unajisikiaje mama mjamzito anafia njiani kwa kukosa huduma ya afya kwakuwa wewe ulikwamisha huduma kupatikana? Hamjisikii hata vibaya kwa watu wanavyopata shida.
Source: ITV
View: https://fb.watch/ncmsWmcjRB/?mibextid=Nif5oz