Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tuombe MunguUkisikiliza pande zote mbili utagundua kuna kitu nyuma ya pazia,
Japo itakawia ila tutafika
Kweli na uteuzi wa huyo mama wengi hasakuupokea vizuri, kingine Barbra nae hawezi pressure ya soka la bongo nasikia hata simu akipigiwa na waandishi wa habari hapokeiNataka kujua na hii simba Holding in ya nani??
Dah haya mambo haya. Ila kale kamama kaCEO kalikuja ghafla sana inatia shaka
Ila pia kwa upande wa mfanyabiashara namuelewa No huwez kuweka hela za usajili mishahara bila kuweka mtu unayemuamini
Umeongea point kubwa sana mkuu, daima mtu msomi anaejua business haezi fanya kitu kwa hasara, hata kama mo dewji anaipenda simba kiasi gani!! Watu wanashindwa kutambua huwezi anza kuezeka nyumba bila kutengeneza msingi imara, . kiufupi simba ilikuwa hovyo sana, anachofanya Mo ni kutengeneza mazingira mazuri ya uendeshaji wa club ili hata akiweka pesa faida ionekane kwake na kwa club pamoja na wanahisa wengine!! Pesa sio nyanya kuwa unaweza mwaga tu bila watu waokote, Plan, plan !! Rangi nyeusi ni tatizo kubwa sana, na hawa ndio watu wa kwanza kumpinga magufuli bila kujua plan yake ipo vipi, yaani watu wanawaza kiufupi bila kufikiria mbali zaidi!!
Kebehi zinazotolewa na waandishi uchwara, wapinzani pamoja na baadhi ya wanasimba sidhani kama kulitakia heri soka letu la Tanzania, !!
Ningeona watanzania tuna busara kama tungekosoa positively na kutengeneza njia nzuri itakayompa dira mwekezaji kutopata woga wa kuwekeza!!
Waandishi wa habari juzi tu tunacheza na Tunisia wamebaki kumwomba Mungu aisaidie Taifa stars ushindi wakati wanajua kabsa tatizo lipo wapi, Mungu anakusaidia vipi kama wewe ni mpumbavu ulobobea!!
Kwanini wawekezaji wasiungwe mkono ili tupate Timu bora ya Taifa na yenye nguvu, !!
Watanzania wengi wanashabikia timu za nje bila kujua misingi ya zile timu, hivi nani katuroga tuwe wapumbavu hivi, shetani gani anasumbua vichwa vyetu?
Duuh kwa akili zetu watanzania tutaendelea kuwa wapumbavu na kichwa cha mwendawazimu hadi basi
ni tatu, sheria inataka kuwe na wawekezaji wasiopungua watatu( ingawa nina uhakika, zote ni company za MO)Hapo ktk hy barua ya FCC naona kuna Simba company km NNE zote za Mo ?
Inawezekana alikuwa Mo peke yake sababu alishatengenezewa mazingira.Wengi wawapi?
Alikuwa MO peke yake,
TAARIFA YA MCHAKATO WA SIMBA KWENDA KWENYEMABADILIKO.
- Tume ya Ushindani (FCC) haihusiki na ucheleweshwaji wa mchakato wa Mabadiliko ndani ya Klabu ya Simba SC kama ilivyoelezwa na viongozi wa Klabu hiyo Siku chache zilizopita.
-Tume ya ushindani Tanzania (FCC) imeuuliza Uongozi wa klabu ya Simba,kulikuwa na uharaka gani wa kuteua Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wakati mchakato wa Mabadiliko haujakamilika..!??
- Katika Taarifa ya Tume (Maelezo Zaidi pichani) imeutaarifu umma kuwa ucheleweshwaji wa mchakato (transformation) wa kubadili mfumo wa uendeshaji wa Klabu ya Simba unatokana na mwitikio hafifu wa kampuni ya Simba Sports Club Company Limited wa kuwasilisha taarifa kamilifu na kwa wakati mbele ya Tume katika kufanikisha uchunguzi Kama ulivyoainishwa Katika Taarifa hiyo.
View attachment 1630397
View attachment 1630398
Nami nimehisi hivyo au zingine za wale akina Hans pope nnni tatu, sheria inataka kuwe na wawekezaji wasiopungua watatu( ingawa nina uhakika, zote ni company za MO)
Nadhani Simba wengi tunaamini mafanikio ni kwa Mo ,hili ngumu kutuondoa kichwaniMo ameifanya Simba imtegemee badala ya Simba kujitegemea. Nia ya kugeuza mfumo ilikuwa kuifanya Simba ijitegemee na kuendeshwa kibiashara, sasa hivi mtu yoyote akihoji mambo ya msingi kuhusu uwekezaji wa Simba wataibuka watu na kuhoji je mo akiondoka utasajili wewe wachezaji au utalipa wewe mishahara ya wachezaji.
Tayari amewateka vichwani wanachama na washabiki bila yeye hakuna Simba ila nawapongeza FCC kwa kusimamia taratibu ziende kisheria
UKIONA MFANYABIASHARA AMBAYE SIO MZAZI WAKO WA DAMU...Wengi wanaompinga MO sio kwamba wana uchungu na Simbasc ni watu wanao ona wivu na watengeneza fitna, ni kawaida ya ngozi nyeusi!!! Maana ukiwasikiliza wapingaji wengi hawana mawazo mbadala zaidi ya kejeli na matusi kwa muekezaji!!
Kauli zao ni "Simbasc inaibiwa" muhindi ni mjanja anafaidika sana, hawasemi anafaidika nini na kwa kiwango gani?!!! Akili za wamatumbi "waswahili" ni shida. Kwa akili tu kabla ya kuja kwa bw. MO simbasc ilikuwa kama kikundi cha tu cha watu kisichokuwa na vision wala mission ya kueleweka, uyu muhindi amejaribu angalau kufanya kitu kinachoonekana.
Kama tunaitaji kukosoa ni ruksa tukosoe uku tukionyesha njia sahihi za kupita na sio makelele tu kama tupo kwenye vijiwe vya walevi!! Tumeona simbasc imebadilika inalipa mishahara kwa wakati, inasajili wachezaji wazuri angalau kwa ukanda huu, ina wataalamu wa benchi la ufundi na imetoa ajira kwa vijana wengine kwenye engo tofauti za kiofisi!! Yote hayo uwezi kusikia wakosoaji walau wakipongeza!!
Mimi ninachoona MO Dewji anajaribu kutengeneza taasisi yenye brand ya kueleweka ili baadae aje atengeneze faida ambayo watagawana yeye na wanahisa wenzake ambao watakuwa wanamiliki share!! Kitu ambacho ndio lengo la mfanyabiashara yeyote yule, kitu ambacho sio kibaya hata kidogo, ila kwa sasa mtu akisema anafaidi sijui anapata zaidi ni uongo mkubwa na mtu wa dizaini iyo hajui biashara!! Biashara ya mpira kwenye nchi maskini kama hii ambayo haina miundombinu ya mpira wala mazingira rafiki ya uwekezaji wa mpira ni ngumu kufanikiwa!!! Ndio maana wafadhili wengi wa vilabu vya Simba and Yanga wa zamani waliishia kufilisika tu!! Washabiki wa nchi hii wanajaa mechi moja wakikutana watani!! Hata mapato yanayopatikana hapo ukichunguza asilimia kubwa yanaenda kwenye taasisi za serikali, na timu zinabaki na chini ya asilimia 30 tu. Sasa hapo ni mwehu tu anaweza kusema kuna faida!!
Kuhusu biashara ya jezi nayo ni utata mtupu washabiki wengi wanavaa jezi feki, ambazo mapato yake yanaishia kwa wanjanja wa kikinga hapo kariakoo!! Hakuna udhibiti na serikali ipo kimya!!!
Nafikili kuliko kumkosoa MO kwa kumuita majina mabaya na kumtuhumu ebu tumpe ushirikiano wa mawazo ili walau tuone tutafika wapi!! Maana kiukweli hizi timu kubwa zikisimama vizuri zitainua soka la nchi hii kwa asilimia kubwa.
Tangu simba imeumbwa hakuna mtu amefanya aliyofanya MoInawezekana alikuwa Mo peke yake sababu alishatengenezewa mazingira.
Alishaanza kuwakopesha viongozi pesa za usajili na mishahara.
Kama mnakumbuka baada ya Simba kuingia miataba wa udhamini na sport pesa mo alikuja juu kwanini viongozi wameingia mkataba bila kumshirikisha. Kumbuka haya yote yalifanyika wakati zabuni ya uuzaji hisa haijatangazwa .
Hata bei za hisa zililenga kiasi kilekile ambacho Mo alitangaza kwa maana nyingine hata walioandaa huo mchakato hawakufanya upembuzi yakinifu nini thamani ya Simba.Tunapozungumzia thamani ya timu inaangaliwa na fan base yake. Wataalamu kama watu wa masoko ya hisa hawakushirikishwa badala yake waliokuwa msitari wa mbele ni Mulamu.Ngambi ambaye naye amepewa zawadi ya ujumbe wa bodi. Ukifatilia kauli ya jaji Thomas Mihayo alisema wao upande wao walishamaliza upande uliobaki ni wa viongozi, Ukifatilia kquli ya aliyekuwa mwenyekiti wa Simba Mkwabi alisema Simba isiogope kudai pesa za uwekezaji, ukifatilia mkataba wa uwekezaji mwekezaji alitakiwa kuweka asilimia kumi mwezi wa kwanza na asilimia zilizobaki ndani ya miezi 3. Mo.hakutakiwa kuharakisha kuingia uwekezaji bali alitakiwa kuhakikisha mazingira yamewekwa sawa kabla ya kuongia kwenye mchakato wa kununua hisa lakini kitendo cha yeye kukubali kununua hisa na asilipe kwa kuhoji matatizo anayoyahoji sasa hivi no wazi inaonekana anafanya ubabaishaji.kwa hivyo mchakato ulitengeneza ili mo aweze kuwa mwekezaji pekee.
Mkuu vipi kuhusu Wazee wetu waliotoa wazo la kuanzisha club ya Simba na wakaianzisha kweli. Nao wamepitwa na Mo.Tangu simba imeumbwa hakuna mtu amefanya aliyofanya Mo
I wish serikali impatie timu bure kabisa
Coz yy hisa zake ni 49 tu na amefanya haya yote je nyie wenye hisa zilizobakia ambazo ni nyingi mmefanya nn?
Sisi wengi tumezaliwa tumeikuta Simba, Yanga na vilabu vingine, kwa mapenzi yetu tukaamua kuchagua vilabu tunavyopenda na wengine wakaamua kuwa wanachama.Mkuu vipi kuhusu Wazee wetu waliotoa wazo la kuanzisha club ya Simba na wakaianzisha kweli. Nao wamepitwa na Mo.
Sasa kwann unasema mo apewe bure timu na wazee walioianzisha wapewe nn mkuuSisi wengi tumezaliwa tumeikuta Simba, Yanga na vilabu vingine, kwa mapenzi yetu tukaamua kuchagua vilabu tunavyopenda na wengine wakaamua kuwa wanachama.
Inabidi tuwape heshima walioanzisha hivyo vilabu kwa sababu bila wao leo hii tusingekuwa tunashabikia hivyo vilabu.
😂😂😂
Hakuna sehemu niliyosema apewe bure nilikuwa naunga mkono hoja ya aliyemjibu mtoa hojaaliyetaka mo apewe timu bureSasa kwann unasema mo apewe bure timu na wazee walioianzisha wapewe nn mkuu
Yanga wanaweza kuwa wako smart kidogo,Iwe case study
Ukienda YouTube utaona akina magori na wenzake wamelezea sana, jinsi mchakato ulivyoanza mpaka ulipo, na akaelezea hizo kampuni nani wamiliki na kwanini wao, watekezaji wengine waliojitokeza zaidi ya Mo, kwa kwanini Mo, kwa kweli jamaa wamejieleza vizuri sana, kiasi kwamba wamejibu maswali yote yenye utata mpaka hizo 20b ziko wapi.Inawezekana alikuwa Mo peke yake sababu alishatengenezewa mazingira.
Alishaanza kuwakopesha viongozi pesa za usajili na mishahara.
Kama mnakumbuka baada ya Simba kuingia miataba wa udhamini na sport pesa mo alikuja juu kwanini viongozi wameingia mkataba bila kumshirikisha. Kumbuka haya yote yalifanyika wakati zabuni ya uuzaji hisa haijatangazwa .
Hata bei za hisa zililenga kiasi kilekile ambacho Mo alitangaza kwa maana nyingine hata walioandaa huo mchakato hawakufanya upembuzi yakinifu nini thamani ya Simba.Tunapozungumzia thamani ya timu inaangaliwa na fan base yake. Wataalamu kama watu wa masoko ya hisa hawakushirikishwa badala yake waliokuwa msitari wa mbele ni Mulamu.Ngambi ambaye naye amepewa zawadi ya ujumbe wa bodi. Ukifatilia kauli ya jaji Thomas Mihayo alisema wao upande wao walishamaliza upande uliobaki ni wa viongozi, Ukifatilia kquli ya aliyekuwa mwenyekiti wa Simba Mkwabi alisema Simba isiogope kudai pesa za uwekezaji, ukifatilia mkataba wa uwekezaji mwekezaji alitakiwa kuweka asilimia kumi mwezi wa kwanza na asilimia zilizobaki ndani ya miezi 3. Mo.hakutakiwa kuharakisha kuingia uwekezaji bali alitakiwa kuhakikisha mazingira yamewekwa sawa kabla ya kuongia kwenye mchakato wa kununua hisa lakini kitendo cha yeye kukubali kununua hisa na asilipe kwa kuhoji matatizo anayoyahoji sasa hivi no wazi inaonekana anafanya ubabaishaji.kwa hivyo mchakato ulitengeneza ili mo aweze kuwa mwekezaji pekee.