Viongozi ndiyo wanaokwamisha mchakato wa mabadiliko, FCC yatoa taarifa leo. Mashabiki na wanachama wa Simba mtadanganywa hadi lini?

Nataka kujua na hii simba Holding in ya nani??

Dah haya mambo haya. Ila kale kamama kaCEO kalikuja ghafla sana inatia shaka

Ila pia kwa upande wa mfanyabiashara namuelewa No huwez kuweka hela za usajili mishahara bila kuweka mtu unayemuamini
Kweli na uteuzi wa huyo mama wengi hasakuupokea vizuri, kingine Barbra nae hawezi pressure ya soka la bongo nasikia hata simu akipigiwa na waandishi wa habari hapokei
 

Umeongee vizuri mkuu kipanta LAKINI je hoja za FCC unazionaje?

Ahsante
 
Wengi wawapi?
Alikuwa MO peke yake,
Inawezekana alikuwa Mo peke yake sababu alishatengenezewa mazingira.
Alishaanza kuwakopesha viongozi pesa za usajili na mishahara.
Kama mnakumbuka baada ya Simba kuingia miataba wa udhamini na sport pesa mo alikuja juu kwanini viongozi wameingia mkataba bila kumshirikisha. Kumbuka haya yote yalifanyika wakati zabuni ya uuzaji hisa haijatangazwa .
Hata bei za hisa zililenga kiasi kilekile ambacho Mo alitangaza kwa maana nyingine hata walioandaa huo mchakato hawakufanya upembuzi yakinifu nini thamani ya Simba.Tunapozungumzia thamani ya timu inaangaliwa na fan base yake. Wataalamu kama watu wa masoko ya hisa hawakushirikishwa badala yake waliokuwa msitari wa mbele ni Mulamu.Ngambi ambaye naye amepewa zawadi ya ujumbe wa bodi. Ukifatilia kauli ya jaji Thomas Mihayo alisema wao upande wao walishamaliza upande uliobaki ni wa viongozi, Ukifatilia kquli ya aliyekuwa mwenyekiti wa Simba Mkwabi alisema Simba isiogope kudai pesa za uwekezaji, ukifatilia mkataba wa uwekezaji mwekezaji alitakiwa kuweka asilimia kumi mwezi wa kwanza na asilimia zilizobaki ndani ya miezi 3. Mo.hakutakiwa kuharakisha kuingia uwekezaji bali alitakiwa kuhakikisha mazingira yamewekwa sawa kabla ya kuongia kwenye mchakato wa kununua hisa lakini kitendo cha yeye kukubali kununua hisa na asilipe kwa kuhoji matatizo anayoyahoji sasa hivi no wazi inaonekana anafanya ubabaishaji.kwa hivyo mchakato ulitengeneza ili mo aweze kuwa mwekezaji pekee.
 

Mosi: Simba imejaa Madudu tupu kuna hafufu ya wizi na Utakatishaji Fedha harahamu kipengele cha (1) inaonyesha kuna Simba 4 ndani ya Simba 1 .


Pili:Kipengele cha (6), 7 na n 8 inaonyesha wazi kuna Vitu Mo dewji anaficha ndio maana akiulizwa anakuwa Mkali, anapaswa kufahamu Simba ni Timu ya Wananchi wanayo haki ya kuuliza kushauri, kuonya na kuelemishwa au kuelemishana sio wakubali kama Mbumbumbu tu!
Tatu- kwa maelezo hayo Bodi ya Wadhamini ya Simba wanpaswa kujiuzulu, CEO anapaswa kujiuzulu hakuchaguliwa kihalali .
Mwisho: - Mo Dewji anyang'anywe Tenda maana tayari kavunja Makubaliano! πŸ‘‡
 
Mo ameifanya Simba imtegemee badala ya Simba kujitegemea. Nia ya kugeuza mfumo ilikuwa kuifanya Simba ijitegemee na kuendeshwa kibiashara, sasa hivi mtu yoyote akihoji mambo ya msingi kuhusu uwekezaji wa Simba wataibuka watu na kuhoji je mo akiondoka utasajili wewe wachezaji au utalipa wewe mishahara ya wachezaji.
Tayari amewateka vichwani wanachama na washabiki bila yeye hakuna Simba ila nawapongeza FCC kwa kusimamia taratibu ziende kisheria
 
Nadhani Simba wengi tunaamini mafanikio ni kwa Mo ,hili ngumu kutuondoa kichwani
 
UKIONA MFANYABIASHARA AMBAYE SIO MZAZI WAKO WA DAMU...

ANAKUAMBIA BIASHARA FULANI HAILIPI(HAINA FAIDA) HUKU YEYE AKIENDELEA KUIFANYA ANAINVEST VYA KUTOSHA...

NA WEWE FANYA HIYO HIYO BIASHARA...

MO WALA GSM NI WAFANYABIASHARA,HAWAWEZI POTEZA FEDHA ZAO FOR NOTHING IN RETURN...
 
Tangu simba imeumbwa hakuna mtu amefanya aliyofanya Mo

I wish serikali impatie timu bure kabisa

Coz yy hisa zake ni 49 tu na amefanya haya yote je nyie wenye hisa zilizobakia ambazo ni nyingi mmefanya nn?
 
Tangu simba imeumbwa hakuna mtu amefanya aliyofanya Mo

I wish serikali impatie timu bure kabisa

Coz yy hisa zake ni 49 tu na amefanya haya yote je nyie wenye hisa zilizobakia ambazo ni nyingi mmefanya nn?
Mkuu vipi kuhusu Wazee wetu waliotoa wazo la kuanzisha club ya Simba na wakaianzisha kweli. Nao wamepitwa na Mo.
 
Mkuu vipi kuhusu Wazee wetu waliotoa wazo la kuanzisha club ya Simba na wakaianzisha kweli. Nao wamepitwa na Mo.
Sisi wengi tumezaliwa tumeikuta Simba, Yanga na vilabu vingine, kwa mapenzi yetu tukaamua kuchagua vilabu tunavyopenda na wengine wakaamua kuwa wanachama.
Inabidi tuwape heshima walioanzisha hivyo vilabu kwa sababu bila wao leo hii tusingekuwa tunashabikia hivyo vilabu.
 
Sasa kwann unasema mo apewe bure timu na wazee walioianzisha wapewe nn mkuu
 
Iwe case study
Yanga wanaweza kuwa wako smart kidogo,

Manji alitaka kuikodi Yanga kwa kipindi cha miaka 10 kwa 30b wakakataa japo hatujui masharti mengine yalikuwaje....!

Simba, jamaa hajatupia hata senti anajiita mmiliki. Hata kama angenunua share 49% bado wenye 51% ndo wenye nguvu kuliko yeye.
 
Ukienda YouTube utaona akina magori na wenzake wamelezea sana, jinsi mchakato ulivyoanza mpaka ulipo, na akaelezea hizo kampuni nani wamiliki na kwanini wao, watekezaji wengine waliojitokeza zaidi ya Mo, kwa kwanini Mo, kwa kweli jamaa wamejieleza vizuri sana, kiasi kwamba wamejibu maswali yote yenye utata mpaka hizo 20b ziko wapi.

Ni interview ya masaa mengi sana na kituo kimoja cha redio sijui tv, ila naona kuna ajenda ya kuitaka simba irudi kule nyuma ili yanga nao wapumue, nilipoiskia hii interview tena walikuja na documents ili kila wanachokisema wakione kwenye hizo documents, sasa hizi blah blah, nilitegemea hao jamaa fcc wangekaa na simba.

tatizo la simba ni records kiasi kwamba unashindwa hata kujua thamani halisi ya klabu ni kiasi gani, maana kwa mujibu wa magori thamani ya simba ilikuwa ndogo sana kutokana na kutokuwa na records, nazani ndio maana sasa hivi wanaanza kujenga hiyo database ya fans na wanachama, kupitia mauzo ya card za mashabiki na wanachama,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…